Habari za Punde

MARAIS WA FA CECAFA WAKUTANA UGANDA

Marais wa Vyama na Mashirikisho ya mpira wa miguu kutoka kwenye mwavuli wa Baraza la mpira kwa nchi za Afrika Mashariki na kati 'CECAFA' walikutana nchini Uganda kujadili mambo mbali mbali yanayohusu Baraza hilo.

Mkutano huo uliokuwa wa ndani uliitishwa na rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Uganda, Moses Magogo na kuhudhuriwa na marais saba kutoka nchi wanachama kumi na mbili.
Kutoka kushoto kwenda kulia, Ravia Idarous(Zanzibar), Nicholas Mwendwa(Kenya) Ndikuniyo Reverien(Burundi), Moses Magogo(Uganda), Juneidi Tilmo(Ethiopia), Vincent Nzamwita(Rwanda) Jamal Malinzi(Tanzania)              
Marais wa Sudani, Djibout na Sudan ya Kusini waliomba radhi kwa kutohudhuria kwao huku Somalia na Eritrea wakikosa kuonekana ukumbini hapo pasipo taarifa yoyote.
Baada ya kikao hicho kilichodumu takriban masaa manne na ushei viongozi hao waliweza kutoka na maazimio tisa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.
Miongoni mwa maazimio hayo ni:
1. Kuifanyiwa marekebisho katiba ya CECAFA 
2. Kuitisha mkutano mkuu wa CECAFA haraka iwezekanavyo.
3. Kuhakikisha kwamba CECAFA inapata makao makuu ya kudumu.
4. Kuboresha mashindano ya CECAFA na kutilia mkazo ligi na mashindano ya vijana (U-15, U-17 na U-20 ya wanaume na wanawake sambamba na mpira wa ufukweni(Beach Soccer).
5. Kuboresha vitengo vya Waamuzi, Makocha, Utawala na Madaktari wa michezo.
6. Kuboresha kitengo cha Masoko na Mawasiliano.
7. CECAFA kuwasilisha maombi maalum ya kuandaa mashindano ya Africa Nations Cup finals miaka ijayo.
8. Kupeleka mapendekezo kwa FIFA juu ya kupatia msaada wa fedha kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu katika nyanja za Vijana, Wanawake na Mpira wa Ufukweni.
Mwaka uliopita CECAFA ilishindwa kuendesha mashindano yao makubwa ikiwemo Kombe la Challenji pamoja na lile la Kagame.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.