Habari za Punde

Zanlink Ltd Yaadhimisha Siku ya Mama Duniani Kwa Upandaji wa Miti Katika Msitu wa Maumbile Masingini Zanzibar.


Managing Director Zanlink Ltd Sanjay Raja akizunguma kabla ya kuaza zoezi la upandaji wa miti katika msitu wa hifadhi wa masingini Zanzibar kuadhimisha Siku ya Mama Duniani kwa upandaji wa miti hiyo ikiwa ni moja ya kufanya kazi zac Kijamii kuliletea maendeleo Taifa la Zanzibar. Jumla ya miti 3000 imepanda wakati wa zoezi hilo ikiwa ya aina tano Mifenesii, Mipilipili Doria, Embe Sakuwa, Misena na Miti ya Mbao Mkagazi. jumla ya hekta 5 imepandwa miti hiyo wakati wa zoezi hilo.  
Msimamizi Mkuu wa Hifadhi ya Msitu wa Maumbile Masingini Zanzibar Salim Ali Khamis akizungumza wakati wa zoezi hilo la upandaji wa miti hiyo na kutowa maelezi jinsi ya upandaji wake
Mkuu wa Chuo cha Kilimo Kizimbani Zanzibar Dkt. Bakar Asead akizungumza kitaalum jinsi ya upandaji wa miti hiyo kwa Washiriki wa zoezi hilo la upandaji wa miti ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda na mbao katika msitu wa kimaumbile masingini Zanzibar.

Washiriki wa zoezi hilo wakimsikiliza Mtaalamu wa Misitu Dkt Bakari Ased akitowa maelezo ya kitaalamu na faidha ya utunzaji wa mazingira kwa upandaji wa Mati na kuleta faida kwa binadamu.
Wadau wa Ngos mbalimbali wakishirikiana na Kampuni ya Zanlink Ltd katika zoezi la upandaji wa mati katika msiti wa masingini Zanzibar.

Wawakilishi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya World Unite Tanzania wakishiriki katika zoezi hilo la upandaji wa miti katika msitu wa masingini Zanzibar.

Wafanyakazi wa Zanlink Ltd wakishiri katika zoezi hilo la upandaji wa mati katika msitu wa masingini Zanzibar.
Afisa Masoko wa Raha Ltd Tanzania Bi Farida Yunus akishiriki katika zoezi hilo la upandaji wa miti katika msitu wa masingini Zanzibar.
Mfanyakazi wa Zanlink Ltd Issa Kassim Ali akishiriki katika zoezi hilo la upandaji wa miti katika msitu wa masingini Zanzibar kuadhimisha Siku ya Mama Msitu Duniani. 
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.