Habari za Punde

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein Akiendelea na Ziara Yake Kisiwani Pemba.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Viongozi na Wananchi wa Wilaya Wete Pemba alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Benjamin Mkapa kuzungumza na Wananchi na Viongozi wa Vikundi vya Kinamama.  
Wanafunzi wa Madrasatal Jabal Hiral Wete Pemba wakipiga dufu kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, alipowasili katika ukumbi wa Benjamin Mkapa Wete Pemba kuzungumza na Wanavikundi vya Ushirika vya Wilaya ya Wete Pemba na kukabidhi zaawadi kwa vikundi hivyo.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe Mwanajuma Majid wakiwa katika ukumbi wa mkutano baada ya kuwasili katika ukumbi huo. 
Mwanafunzi wa Madrasatul Jabar Hiral Ust Yahya Hilal akisoma Quran kabla ya kuaza kwa hafla hiyo katika ukumbi wa Benjamin Mkapa Wete Pemba. 
Katibu wa UWT Wilaya ya Wete Pemba Bi Mary Saimon akitowa maelezo ya Wilaya yake kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa mkutano huo na Wanawake wa Vikundi vya Ushirika katika Wilaya yake uliofanyika katika ukumbi wa Benjamin Mkapa Wete Pemba.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Bi Tunu Kondo akitowa maelezo na kuutambulisha Ujumbe wa Mama Mwanamwema Umoja wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi zaawadi kwa Wanawake wa Vikundi vya Ushirika Wilaya ya Wete Pemba. 
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe Mwanajuma Majid akizungumza wakati wa hafla hiyo na kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kuzungumza na Wanawake wa Vikundi vya Ushirika Wilaya ya Wete Pemba katika ukumbi wa Benjamin Mkapa.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wanawake wa Vikundi vya Ushirika Wilaya ya Wete Pemba, katika ukumbi wa Benjamin Mkapa.  
Wananchi wa Wilaya ya Wete Pemba wakimsikiliza Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman wakati akitowa nasaha zake, katika ukumbi wa Benjamin Mkapa Pemba.  
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,akifurahia jambo wakati wa mkutano wake na Wanawake wa Wilaya ya Wete Pemba katika ukumbi wa Benjaman Mkapa Pemba.
Wananchi wa Wilaya ya Wete wa Vikundi vya Ushirika wakimshangilia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati akiwahutubia na kutowa nasaha zake kwao kabla ya kuwakabidhi zawadi kwa vikundi hivyo. vya Wilaya ya Wete Pemba.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wanawake wa Wilaya ya Wete na kutowa nasaha zake kwa wanavikundi hivyo na kuwakabidhi zawadi kwa ajili ya kuendeleza vikundi vyao kujiongezea kipato. hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Benjamin Mkapa Wete Pemba.


Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi mapazia na mabusati Kiongozi wa kikundi cha Kheri Minalaah cha Bopwe Jimbo la Gando Pemba. wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Benjamin Mkapa Wete Pemba.  
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Charehani na jora la vitambaa Kiongozi wa Kikundi cha Tujikwamuwe cha Kizimbani Jimbo la Gando Pemba. wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Benjamin Mkapa Wete Pemba.  
Viongozi wa Meza Kuu wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi zawadi kwa vikundi vya ushirika vya wanawake wa Wilaya ya Wete Pemba. katika ukumbi wa Benjamin Mkapa.
Wananchi wa Wilaya ya Wete Pemba wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa Wanawake wa Vikundi vya Ushirika mbalimbali katika ukumbi wa Benjamin Mkapa Wete Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.