Habari za Punde

Mkutano wa siku tano wa Tathmini ya utekelezaji wa kanuni za afya ya Kimataifa wafunguliwa katika Hoteli ya Ocean View Kilimani.

 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma akifungua mkutano wa siku tano wa Tathmini ya utekelezaji wa kanuni za Afya ya Kimataifa uliofanyika katika Hoteli ya Ocean View Kilimani, Mjini Zanzibar.

 Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt. Ghirmany Andermichael akitoa hotuba kwa niaba ya Mwakilishi wa Shirika hilo Tanzania katika ufunguzi wa mkutano wa siku tano wa Tathmini ya utekelezaji wa kanuni za afya ya Kimataifa katika Hoteli ya Ocean View Kilimani.

 Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohd Abdalla akitoa maelezo kwa wajumbe wa mkutano wa Tathmini ya utekelezaji wa kanuni za Afya ya Kimataifa jiografia na huduma  za afya zinazopatikana Zanzibar.
 Baadhi ya wajume wa mkutano wa siku tano wa Tathmini ya utekelezaji wa kanuni za Afya ya Kimataifa Zanzibar wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika Hoteli ya Ocean View Mji Zanzibar,
Picha ya pamoja ya wajumbe wa mkutano wa Tathmini ya utekelezaji wa kanuni za Afya ya Kimataifsa na mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano uliofanyika Hoteli ya Ocean View.
Picha Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar

Na Ramadhani Ali/Maelezo 

Zanzibar imekuwa miongoni mwa nchi za mwanzo duniani kufanyiwa tathmini ya utekelezaji wa kanuni za Afya ya Kimataifa ambapo wataalamu kutoka nchi mbali mbali wapo nchini kwa muda wa siku tano kuanzia Aprili  24 kufanya tathmini hiyo inayosimamiwa na Shirika la Afya duniani (WHO).

Lengo kuu la Tathmini za aina hiyo kwa nchi ni kujua mafanikio waliyopata  na kasoro zinazowakabili ili kuweza kuimarisha utoaji huduma kwa jamii.

Timu ya wataalamu wanaosimamia tathmini hiyo watatembelea sehemu mbali mbali za Zanzibar na watafanya mahojiano na wataalamu, wafanyakazi wa sekta mbali ikiwemo afya na wananchi  wa kawaida ili kuona hali ya utekeleza wa huduma za afya na sekta zinazochangia huduma hiyo.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pemba Juma ambae ni Kaimu Waziri wa Afya akifungua mkutano wa wataalamu hao katika Hoteli ya Ocena View Kilimani, alisema Zanzibar imefarajika kufanyiwa tathmini hiyo.

Amesema kwa kipindi kirefu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejiimarisha katika kuweka mikakati ya kuimarisha afya vijijini katika Wilaya zote 11 na kujiweka tayari katika kupambana na majanga yanapotokea.

Ameongeza kuwa kufuatia mikakati hiyo Zanzibar imeweza kufanya vizuri katika zoezi la chanjo ya maradhi mbali mbali na kupata sifa kubwa duniani katika kupambana na maradhi ya Malaria.

Amewahakikishia wajumbe hao kuwa taarifa naq mapendekezo watakayotowa Serikali itayafanyia kazi na kuwashirikisha wadau kutoka Wizara na Taasisi nyengine zinazogusa afya za wananchi.

Amesema kuibuka kwa maradhi ya Ebola katika nchi za Afrika Magharibi imetoa funzo kwa nchi nyengine kuwa Wizara ya Afya pekee haiwezi kulinda athari za afya za wananchi yanapotokea maradhi bila ya kuwa na ushirikiano wa karibu na Mashirika na baadhi ya Wizara hivyo Serikali itazishirikisha taasisi nyengine kujadili taarifa itakayotolewa.

Akitoa taarifa ya Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) Mwakilishi wa  Shirika hilo Zanzibar Dkt. Ghirmany Andermichael alisema matokeo ya tathmini hiyo itakuwa chachu ya hatua nyengine ya maendeleo katika kuimarisha mpango wa Taifa katika usalama wa sekta ya afya Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib amewahakikishia wataalamu wa kimataifa wanaosimamia Tathmini hiyo kuwa Wizara itatoa kila ushirikiano na kuwa wawazi kutoa taarifa wanazozihitaji kufanikisha kazi yao.

Amesema Wizara inaamini kuwa maradhi hayana mpaka yanaweza kumshambulia mtu yoyote na wakati wowote bila taarifa hivyo wamekuwa makini katika kujiandaa kupambana wakati wote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.