Habari za Punde

UVCCM Zanzibar yaendelea kutimiza ahadi


Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ZANZIBAR imeendelea kutimiza ahadi zake mbali mbali ilizoweka wakati wa ziara ya Kaimu Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Nd Abdulghafar Idirissa.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa kutoka Wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini Pemba Nd Abdalaah Mohd (kidishi) jana alikabidhi mifuko ishirini (20) ya saruji yenye thamani ya shilingi laki tatu na alfu kumi (310,000) kwa niaba ya Kaimu Naibu Katibu Mkuu UVCCM ZNZ Nd. Abdulghafar Idrissa ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa 02/03/2017 Alipokuwa ziarani Pemba wilaya ya mkoani katika Tawi la Mkungu alipokuwa akikaguwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm na agizo la Mwenyekiti wa Chama Taifa kutaka chama kipelekwe kwa wanachama ambapo alikagua ujenzi wa tawi hilo jipya ambao uliazishwa kwa nguvu na michango ya vijana wa CCM ambapo aliona hatuwa nzuri iliyofikiwa nae akaahidi kutoa mifuko hiyo 20 ya saruji kama mchango wa UVCCM kusaidia katika ujenzi huo.

Nd. Abdallah kidishi (MNEC) wakati akikabidhi mifuko hiyo kwa niaba ya Naibu katibu mkuu UVCCM ZNZ alimpongeza sana Naibu kwa kuwa muungwana hasa baada ya kuahidi na kutekeleza ahadi yake kwa ukamilifu na kwa wakati.

"CCM ikipata viongozi bora kama hawa wanaojuwa shida za wanaowaongoza na kuzitatuwa haitaondoka madarakani milele, binafsi nitowe wito kwa viongozi wengine tuige mwenendo wa Naibu wa vijana tukiwaahidi wenzetu tusiwakimbie turudi kutekeleza tulichowaahidi" alisema Mh Abdalah.


Nae Katibu UVCCM Wilaya ya Mkoani Pemba Nd MOHD aliwataka viongozi wa chama wa tawi hilo la Mkungu kuwa karibu na uongozi wa UVCCM wa tawi hilo kwa kuwapa mashirikiano ya kutosha wanapotaka kufanya jambo la kukijenga chama hasa ukizingatia wao ndio walezi na kusema kua alichokifanya Naibu ni kitendo cha kupongezwa maana kimetengeza heshima kwa UVCCM wilaya ya Mkoani.

Nae Mwenyekiti wa CCM Tawi hilo la Mkungu Alipokea saruji hiyo na kuwataka vijana waitumie saruji hiyo kwa malengo yaliyo kusudiwa na kuwakumbusha kuwa kipindi walicho nacho ni mvuwa sio kipindi rafiki kwa saruji waitumie haraka kukamilisha ujezi wa tawi hilo pia aliwakumbusha vijana kuwa sasa ni wakati wa uchaguzi wajitokeze kwa wingi kuchukuwa fomu za uongozi wa chama na jumuiya zake

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.