Habari za Punde

Afisa Mdhamini Wizara ya Fedha na mipango atembelea taasisi mbali mbali za Serikali zinazokusanya mapato katika maeneo ya bandarini

 AFISA Mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango Pemba, Mhe:Ibrahim Saleh Juma akizungumza na watendaji wa taasisi mbali mbali za Serikali zinazokusanya mapato katika maeneo ya bandarini, wakati wa ziara yake ya siku moja na kuzungumza na watendaji hao.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MENEJA wa mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Tawi la Pemba, Habibu Saleh Sultani, akizungumza na watendaji wenzake wanaokusanya mapato katika maeneo ya bandarini Wete, wakati wa ziara ya siku moja na kuzungumza na watendaji hao.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MENEJA wa shirika la Bandari Wete Hassan Hamad Ali, akizungumzia juu ya baadhi ya watendaji wa taasisi zinazokusanya kodi bandarini hapo, kutokuwa katika maeneo ya kazi wakati vyombo vyenye mizigo vinapofika.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MENEJA wa bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Said Ali Mohamed, akitoa ufafanuzi juu ya suala la Magendo ya Mafuta yanavyopoteza mapato ya nchi, wakati wa kikao cha taasisi zinazokusanya kodi bandarini, huko katika bandari ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.