JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
![]() |
Simu: +255-26-232-2484/232-4560
Barabara ya Reli na Mahakama,
Nukushi: +255-26-232-1955, S. L. P. 980,

24 Aprili, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU AKAGUA MAANDALIZI
YA SHEREHE ZA MUUNGANO
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya
ukaguzi wa miundombinu kwa ajili ya sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na
kusema kuwa maandalizi yake yako pazuri.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
mchana (Jumatatu, Aprili 24, 2017) mara baada ya kupokea taarifa ya maandalizi
na kukagua Uwanja wa Jamhuri ambapo sherehe hizo zitafanyika na uwanja wa
Nyerere Square ambako zitafanyika burudani mbalimbali kama sehemu ya
maadhimisho hayo.
“Nilikuja kuangalia maandalizi ya
sherehe hizo yamefikia wapi, najua kutakuwa na maonyesho ya kijeshi zikiwemo
michezo na burudani kutoka Tanzania Bara za Visiwani,” alisema.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo
kuwakaribisha wakazi kutoka wilaya zote za mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani
wafike kwenye maonyesho hayo ambayo kwa mara ya kwanza katika historia ya
Tanzania yanafanyika mkoani humo.
“Tunatarajia wageni wengi kutoka
nje ya mkoa huu wakiwemo viongozi wastaafu wa kitaifa, waheshimiwa mabalozi na
wake wa waasisi wa Taifa hili, Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume. Pia
tutawatambulisha rasmi ndugu zetu waliochanganya udongo wa Tanganyika na
Zanzibar mwaka 1964,” alisema.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba sehemu zilizobakia
zitakamilika kabla ya kesho.
(mwisho)
IMETOLEWA
NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATATU, APRILI 24, 2017.
No comments:
Post a Comment