HOTUBA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA OFISI
YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018
---------------------------------------------------
1.0
Mheshimiwa
Spika,
naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako Tukufu lipokee, lijadili na hatimae likae
kama Kamati ya Mapato na Matumizi ili liidhinishe Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
2.0
Mheshimiwa
Spika,
kwanza kabisa naomba kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na
Mwingi wa Rehema kwa kutukutanisha tena katika kikao hiki cha Baraza la
Wawakilishi tukiwa katika hali ya amani, furaha na mshikamano wa hali ya juu
katika nchi yetu. Namuomba Mwenyezi Mungu akipe kikao hiki baraka ili
tukiendeshe na kukimaliza huku tukiwa tumefikia azma yetu tuliyoikusudia. Ni
matumaini yangu kuwa Baraza lako Tukufu litaipokea, kuijadili na hatimae
kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
ili tuweze kupata nyenzo za kuwatumikia wananchi wetu kikamilifu.
3.0
Mheshimiwa
Spika,
kwa dhati kabisa napenda kumpongeza na kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Ali
Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa hekima
na busara anazotumia katika kuiongoza nchi yetu kulikopelekea kupata maendeleo
tuliyonayo sasa ambayo kila mmoja wetu anafaidika nayo. Hakika juhudi na
miongozo yake anayoitoa imeonesha nia na azma njema aliyonayo kwa wananchi wa
Zanzibar na Tanzania kwa jumla juu ya kukuza uchumi wa nchi yetu na kuondokana
kabisa na umaskini. Ni jukumu letu sisi viongozi tunaomsadia na wananchi wote
kwa jumla kuhakikisha kuwa tunamuunga mkono katika kufikia azma yake hiyo.
4.0
Mheshimiwa
Spika,
nachukua fursa hii pia kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya
katika kuwatumikia wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishirikiana na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaaliwa Majaaliwa. Bila shaka Viongozi
wetu hawa wameonesha uwezo mkubwa katika kuongoza mabadiliko ya kiuchumi na
kijamii katika nchi yetu. Namuomba
Mwenyezi Mungu awazidishie uwezo na hekima katika kutekeleza majukumu yao.
5.0
Mheshimiwa
Spika,
sasa naomba uniruhusu kuchukua nafasi hii nikupongeze na kukushukuru wewe
binafsi Mheshimiwa Spika, kwa kuendelea kuliongoza vyema Baraza hili Tukufu kwa
mashirikiano makubwa na wasaidizi wako na viongozi wote wa Baraza hili. Naomba
niwapongeze Wenyeviti wote na Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Baraza kwa kazi
nzuri wanazozifanya za kusimamia utendaji wa Wizara na Taasisi za Serikali.
Uangalizi na usimamiaji wao wa karibu wa utendaji wa Wizara na Taasisi hizo
umeongeza kasi na umakini kwa watendaji wetu katika kutoa huduma bora kwa
wananchi. Kwa namna ya pekee namshukuru sana Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa, Mheshimiwa Omar Seif Abeid,
Mwakilishi wa Wananchi wa Jimbo la Konde, Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Panya
Ali Abdalla, Mwakilishi wa Viti Maalum na Wajumbe wote wa Kamati hiyo kwa
kuyapitia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ya
mwaka 2017/2018 na kukubali yawasilishwe katika kikao chako hiki kitukufu baada
ya kuifanyia kazi miongozo waliyotupatia.
HALI YA SIASA:
6.0
Mheshimiwa
Spika,
hivi sasa ni takriban mwaka mmoja tangu nchi yetu kufanya Uchaguzi Mkuu wa
marudio tarehe 20 Machi, 2016 ambapo Chama cha Mapinduzi kiliibuka na ushindi
mkubwa. Ndani ya kipindi hicho, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iliandaa Taarifa
ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Machi, 2016 kama taratibu za uchaguzi za nchi
yetu zinavyoelekeza na ilimkabidhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi mnamo tarehe 9 Febuari, 2017. Aidha, nakala za taarifa hizo tayari
zimesambazwa kwa wadau wote wa uchaguzi pamoja na maktaba za Taasisi za elimu
ya juu. Naomba sana viongozi na wananchi
waisome taarifa hiyo ili kuelewa kwa kina shughuli zote za uchaguzi huo na
changamoto zilizojitokeza ili kwa pamoja tushirikiane katika kukabiliana na
changamoto hizo.
7.0
Mheshimiwa
Spika,
tangu kumalizika kwa uchaguzi huo kumekuwa na taarifa za kupotosha zinazotolewa
na baadhi ya viongozi wa chama cha siasa ambacho kilisusia uchaguzi huo kwamba
ama uchaguzi huo utarejewa au mmoja wa viongozi wa chama hicho atakabidhiwa
uongozi wa nchi.
8.0
Mheshimiwa
Spika,
nachukua nafasi hii kusisitiza kuwa uchaguzi huo umekwisha na Dk. Ali Mohamed
Shein ndiye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na panapo
majaaliwa yake Mwenyezi Mungu uchaguzi mwengine utakuwa mwaka 2020. Hivyo,
Serikali iliyopo madarakani inaendelea kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia
wananchi kama ilivyoelekezwa na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka
2015 – 2020. Aidha, natoa wito kwa wananchi kuendeleza hali ya umoja, amani na
utulivu iliyopo hivi sasa na tuendelee kufanya shughuli zetu za uzalishaji mali
na tuachane kabisa na “hadithi” hizo za alinacha zinazolenga kuturejesha nyuma
katika kuwaletea wananchi maendeleo.
9.0
Mheshimiwa Spika,
uchumi
wa Zanzibar kwa mwaka 2016 umeendelea kuimarika ambapo ukuaji halisi ni
asilimia 6.8 kutoka asilimia 6.5 ya mwaka 2015. Hali hii ni tofauti na taswira
inayojionesha kwa mwenendo wa ukuaji wa uchumi kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la
Sahara ambapo kasi ya ukuaji wa uchumi imeshuka na kufikia wastani wa asilimia
1.6 kwa mwaka 2016 kutoka wastani wa asilimia 3.4 ya mwaka 2015. Aidha, uchumi
wa Kanda ya Afrika Mashariki kwa mwaka 2016 nao pia umekua kwa kasi ndogo ya
wastani wa asilimia 2.7 kutoka asilimia 3.5 ya mwaka 2015.
10.0
Mheshimiwa
Spika, hali
hiyo ya ukuaji wa uchumi kwa nchi yetu imepelekea pia kuongezeka kwa Pato la Taifa kwa mwaka 2016 ambalo limeongezeka
kufikia thamani ya Shilingi 2,628.4 Bilioni ikilinganishwa na thamani ya Shilingi
2,309.5 bilioni mwaka 2015. Vile vile, wastani wa pato la mtu binafsi
limeongezeka kufikia Shilingi 1,806,000 kutoka Shilingi 1,633,000 mwaka 2015. Kasi ya mfumko wa bei nayo imefikia wastani wa
asilimia 6.7 mwaka 2016 kutoka asilimia 5.7 mwaka 2015 kutokana na mwenendo wa
bei za bidhaa za chakula.
MALENGO MAKUU YA SERIKALI KWA MWAKA
2017/2018:
11.0
Mheshimiwa
Spika, Serikali
bado inaendelea na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2020 ikiwa katika
kipindi cha miaka mitano ya mwisho. Aidha, hivi karibuni Serikali imeidhinisha
awamu ya tatu ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUZA III). Hii inamaanisha kwamba malengo yetu bado
yanadhamiria utekelezaji wa Mipango hiyo mikuu ambayo inalenga katika kukuza
uchumi, kuimarisha huduma za jamii na kuimarisha demokrasia na utawala bora.
12.0
Mheshimiwa
Spika, Serikali
itaendelea kuweka mkazo katika kugharamia uendeshaji wake na kutoa huduma bora
kwa wananchi kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa umakini mkubwa na kuhakikisha
kuwa matumizi yote yanaleta tija kwa umma. Katika kuwezesha azma hiyo, Serikali
itaongeza jitihada kubwa katika ukusanyaji na udhibiti wa uvujaji wa mapato
katika maeneo yote.
Mheshimiwa
Spika, kwa
mwaka wa fedha 2017/2018 maeneo muhimu yatakayopewa kipaumbele katika
kutekeleza mpango wa maendeleo ni pamoja na kuimarisha ubora wa huduma za
kijamii zikiwemo elimu, afya, makaazi na upatikanaji wa maji safi na salama. Kuimarisha miundombinu ya uingiaji nchini
inayojumuisha bandari na viwanja vya ndege pamoja na kuimarisha miundombinu ya
msingi ikiwemo barabara na nishati. Kushajiisha zaidi uwekezaji katika viwanda
vidogo vidogo kwa kuongeza thamani bidhaa na ubora wa vifungashio, kuimarisha
kilimo, kukuza uwezo wa wataalamu katika fani zenye upungufu mkubwa,
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kufanya tafiti zitakazosaidia kutoa
maamuzi katika mipango ya maendeleo yetu.
13.0
Mheshimiwa
Spika, Serikali tayari imeandaa Sera ya Mafuta na Gesi Asilia na Baraza hili Tukufu limeshatunga
Sheria ya kusimamia masuala ya Mafuta na Gesi Asilia. Kutokana na kukamilika kwa hatua hizo, Serikali imeunda Taasisi ya
kusimamia shughuli za Utafutaji na Uendelezaji wa Mafuta na Gesi Asilia (ZPRA)
na Mkurugenzi Mwendeshaji (MD) wa Taasisi hiyo tayari ameshateuliwa. Hivi
karibuni Serikali imekuwa katika utaratibu wa kufanya utafiti wa kubaini maeneo yenye muelekeo wa kuwepo
rasilimali ya Mafuta na Gesi Asilia katika kitalu cha Pemba - Zanzibar kupitia
Kampuni za RAKGAS
na BGP.
14.0
Mheshimiwa
Spika, katika
kuendelea na maandalizi ya kuingia kikamilifu
katika sekta hiyo, Serikali kwa msaada wa Shirika la OfD la Norway, imeanza
kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani kwa kuwapatia mafunzo maalumu ambayo
yatawawezesha kutekeleza kazi zao za kila siku katika sekta hii pamoja na kuwa
na uwezo wa kutathmini rasilimali ya mafuta na gesi iliyopo. Ni matumaini yetu kuwa sekta hii itasaidia sana
kukuza uchumi wetu na pia kuongeza ajira kwa vijana wetu.
MASUALA MTAMBUKA:
Mazingira:
15.0
Mheshimiwa
Spika, suala
la utunzaji wa mazingira linaendelea
kuwa na umuhimu katika ustawi wa maisha yetu hasa tukizingatia azma yetu ya
kuwa na maendeleo endelevu. Mabadiliko ya Tabianchi bado yamekuwa yakileta
athari kubwa katika jamii zetu ikiwemo mmong’onyoko wa fukwe za bahari na
uingiaji wa maji ya bahari katika maeneo ya makaazi na kilimo. Serikali inaendelea
kuchukua hatua madhubuti za kupunguza athari zinazotokana na hali hiyo ili
maisha ya wananchi wetu yaendelee bila ya vikwazo. Bado tunaendelea kutoa wito
kwa wananchi kuendelea kutunza mazingira yetu hasa misitu ya asili sambamba na kupanda
miti kwa wingi maeneo ya wazi ikiwemo fukwe za bahari. Aidha, Serikali inasisitiza sana wananchi kuachana
na tabia ya kuharibu mazingira kwa kukata miti ovyo na uchimbaji holela wa
rasilimali zisizorejesheka ikiwemo mchanga, kifusi na mawe. Suala la kulinda
mazingira siyo la Serikali peke yake bali ni la wananchi pia.
Athari za Mvua za Masika:
16.0
Mheshimiwa
Spika, nchi
yetu imeshuhudia mvua kubwa za Masika ambazo zinaendelea hadi hivi sasa.
Kutokana na hali hiyo, bado tunatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari za
kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo miripuko ya maradhi
yanayosababishwa na uchafuzi wa maji tunayotumia ikiwemo matumbo ya kuharisha
na kipindupindu.
17.0
Mheshimiwa
Spika, itakumbukwa
kwamba mwaka jana (2015/2016) nchi yetu ilikumbwa na maradhi ya kipindupindu
ambapo jumla ya wagonjwa 4,330 walilazwa katika vituo 22 vya matibabu
vilivyofunguliwa Unguja na Pemba. Wagonjwa 2,652 kati yao walilazwa Unguja na
1,678 walilazwa Pemba. Ingawa mripuko huu uliathiri Wilaya na Mikoa yote ya
Zanzibar, zaidi ya asilimia 75 ya wagonjwa wote walitoka Mkoa wa Mjini Magharibi,
Unguja na Mkoa wa Kaskazini Pemba. Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha
kukabiliana na hali hiyo na kufanikiwa kulimaliza gonjwa hilo kabisa.
Tunawashukuru sana wataalamu wetu na wote walioshiriki katika operesheni ya
kukabiliana na maradhi hayo.
18.0
Mheshimiwa
Spika, wito
wangu kwa wananchi ni kuendelea kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalam wetu
wa afya juu ya usafi wa mazingira ikiwemo kunawa mikono mara watokapo chooni na
kabla ya kula, tuache tabia ya kutupa taka ovyo zikiwemo za kinyesi katika
mazingira yetu tunayoishi pamoja na kuchemsha maji ya kunywa au kutia dawa. Kwa
upande wa wafanyabiashara wa vyakula nao waendelee kufuata masharti yaliyowekwa
juu ya biashara zao kwa kuzingatia suala la usafi na ulinzi wa afya zetu ili
kujikinga na maradhi.
19.0
Mheshimiwa
Spika,
usiku wa kuamkia tarehe 30 Aprili, 2017 tumeshuhudia mvua hizi zikileta athari
kubwa kwa wananchi wenzetu wa Mkoa wa Kusini Pemba, hasa katika maeneo ya Chonga,
Kilindi na Vitongoji kwa upande wa Wilaya ya Chake Chake na Uweleni, Mbuyuni,
Mwambe, Chumbageni na Ng’ombeni kwa Wilaya ya Mkoani ambao walikumbwa na
mafuriko na maporomoko ya ardhi (land slide) na kusababisha nyumba nyingi
kubomoka na nyengine kufukiwa na udongo. Tukio hilo pia lilisababisha kifo cha
mtoto Rahika Ramadhan Mohamed wa Chanjaani, Chake Chake mwenye umri wa miaka 8
aliyefariki baada ya kuangukiwa na ukuta ulioboba maji wa Madrasa ya Qur-an. Nachukua
nafasi hii kwa mara nyengine tena kwa niaba ya Serikali kutoa pole kwa wafiwa
na wananchi wote waliopata maafa hayo na kuwataka kuwa na subira katika kipindi
hiki kigumu. Serikali inafanya tathmini ya kina ili kubaini ukubwa wa athari
iliyojitokeza pamoja na waathirika wa tukio hilo ili kuwasaidia wananchi hao
kuweza kurudi katika hali ya maisha yao ya kawaida.
20.0
Mheshimiwa
Spika, bado
tunaendelea kuwataka wananchi kuepuka kujenga katika maeneo hatarishi ambayo
mazingira yake yanaweza kuathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa hasa wakati
mvua kubwa zinaponyesha kama vile mabondeni, kwenye njia za asili za maji na
pembezoni mwa milima hasa Kisiwani Pemba.
Masuala ya Watu Wenye Ulemavu:
21.0
Mheshimiwa Spika, Serikali
inaendelea kuchukua juhudi za dhati katika kuhakikisha kuwa Watu wenye Ulemavu wanapatiwa fursa na
haki katika nchi yetu. Katika kutekeleza azma hiyo Serikali itahakikisha kwamba
vitendo vya udhalilishaji wa Watu wenye
Ulemavu katika jamii yetu
vinatokomezwa ili wenzetu hawa waweze kuishi bila ya kubaguliwa na kudhalilishwa kwa
namna yoyote ile. Aidha, Serikali
inaendelea na juhudi za kuwadhibiti na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika
na vitendo vya ubakaji, upigaji, kuwatelekeza na wanaowaita majina mabaya Watu
wenye Ulemavu.
22.0
Mheshimiwa Spika, Serikali pia inaendelea na jitihada za
kufuatilia kesi za udhalilishaji wa Watu wenye Ulemavu ili kuhakikisha kuwa
kesi hizo zinapatiwa ufumbuzi pamoja na kupatikana kwa ushahidi wa kutosha juu
ya udhalilishaji huo. Hivyo,
naviagiza vyombo vya kusimamia haki na sheria kutimiza wajibu wao ikiwa ni
pamoja na kuzishughulikia kesi kwa haraka na kuwapatia haki Watu wenye Ulemavu
ili kulinda utu wao.
Hali ya Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI:
23.0
Mheshimiwa
Spika,
Tume ya UKIMWI imepewa jukumu la kuratibu muitiko wa Taifa wa UKIMWI
unaozijumuisha sekta zote. Muitiko wa
Taifa wa UKIMWI kuanzia 2016 hadi 2020 unaimarishwa kwa kuhakikisha upatikanaji
wa huduma za msingi kwa watu wote bila unyanyapaa ili kufikia malengo ya
90-90-90 ifikapo 2020 na kumaliza maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI (VVU)
ifikapo mwaka 2030. Tafsiri halisi ya malengo ya 90-90-90 ni kwamba asilimia 90
ya watu walioambukizwa VVU wawe wanajitambua kuwa wanaishi na VVU, asilimia 90
ya wanaojitambua kuishi na VVU wawe wanatumia dawa za ARVs na asilimia 90 ya
watu wanaotumia dawa hizo wawe na idadi ndogo ya VVU mwilini.
24.0
Mheshimiwa
Spika,
Serikali yetu ya Mapinduzi ya Zanzibar inajumuika na nchi nyengine duniani
kuhakikisha kuwa malengo hayo yanafikiwa ili jamii ya Wazanzibari iweze kuishi
bila ya madhara yatokanayo na maradhi haya.
Mapambano Dhidi ya Dawa za Kulevya:
25.0
Mheshimiwa
Spika, suala
la uletaji, usambazaji
na matumizi ya Dawa za Kulevya bado linaendelea kuwa ni tatizo sugu duniani kote
ikiwemo Zanzibar na athari zake zimekuwa ni kubwa kwa vijana wetu na jamii kwa
ujumla. Hali halisi ya athari ya dawa hizi inaonesha kwamba vijana ndio
wanaoathirika zaidi na matumizi ya dawa hizo ambao ni nguvu kazi ya Taifa. Katika kupambana na changamoto hii Serikali
kwa kushirikiana na wadau wote inaendelea kuchukua hatua za kudhibiti na
kupunguza usafirishaji na usambazaji, matumizi na athari zinazotokana na dawa
hizo. Aidha, nachukua fursa hii, kuvitaka vyombo vyote vinavyosimamia udhibiti
wa dawa za kulevya kufanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa zaidi ili kurahisisha
utekelezaji wa mipango ya udhibiti na kutokomeza wa dawa hizo hapa nchini. Pia nawaomba wananchi wote katika maeneo yao kuwa
na kamati za kupambana na dawa za kulevya na tusiwaonee aibu watu wanaofanya
biashara hii katika maeneo yetu, tuwafichue na kuwaripoti katika vyombo husika.
MALENGO
NA UTEKELEZAJI WA KAZI ZA KAWAIDA NA MIRADI YA MAENDELEO KWA KIPINDI
CHA MIEZI TISA (JULAI-MACHI) 2016/2017:
26.0
Mheshimiwa
Spika,
katika kipindi cha miezi tisa
(Julai- Machi) cha mwaka wa fedha 2016/2017, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na
Taasisi zake imechukua juhudi kubwa katika kutekeleza malengo iliyojipangia
katika Programu zake kama ifuatavyo:-
1. Programu
ya Uratibu wa Shughuli za Makamu wa Pili wa Rais (C011)
|
27.0
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2016/2017
Programu hii imetekeleza kazi zifuatazo:-
i.
Ofisi imeratibu ziara mbili (2) za Kiserikali
kwa Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais nje ya nchi katika nchi za India, China
na Falme za Nchi za Kiarabu. Ziara ya nchini India ililenga kukuza na
kuendeleza mashirikiano katika sekta ya kilimo cha mazao ya biashara na viungo;
viwanda vidogo vidogo vya kusindika viungo, uwekezaji na mashirikiano katika
sekta ya afya. Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais alitembelea Jimbo la Kerala na
Chennai Mjini New Delhi. Pia, alikagua
maeneo ya kilimo, viwanda vya mazao ya kilimo na vifungashio (packaging) pamoja
na masoko ya bidhaa za kilimo. Vile vile, Mheshimiwa Makamu alitembelea
Hospitali ya MIOT yenye mahusiano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
kupokea wagonjwa kutoka Zanzibar kwa ajili ya uchunguzi wa afya na matibabu.
Mheshimiwa pia, alifanya ziara katika Kiwanda cha Matrekta cha Mahendra,
kuangalia teknolojia ya umwagiliaji maji pamoja na kufanya mazungumzo na
wafanyabiashara na wawekezaji wa India.
ii.
Lengo la
ziara ya Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais katika Falme za Nchi za
Kiarabu ilikuwa ni kukuza mashirikiano baina ya Zanzibar na nchi hizo katika
utafiti na uendelezaji wa Sekta ya Mafuta na Gesi, Uimarishaji wa usalama
katika viwanja vya ndege na bandari na kutathmini maendeleo ya uazishwaji wa
Ofisi mpya ya Mamlaka ya Usafirishaji Zanzibar.
- Katika ziara ya China ya Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais ililenga kukuza na kuendeleza mashirikiano katika sekta ya miundombinu ikiwemo gati na uwanja wa ndege; uendelezaji wa mfumo wa e–government, e–health, na e–taxing. Uvuvi wa bahari kuu, na ukuzaji wa sekta ya utalii kwa kuimarisha ujenzi wa mahoteli ya kisasa Visiwani Zanzibar. Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi alikutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Exim ya China; Uongozi wa Zhongxing Telecommunication Equipment (ZTE), Uongozi wa AVIC International Real Estate Limited, Uongozi wa Thermal Bulloon Endomentrial Ablator – China; Beijing Construction Company, Kampuni ya Uvuvi China, China Habour Construction na Beijing Construction Engineering Group.
iv.
Ofisi imeratibu ziara 21 za ndani ya nchi (Unguja,
Pemba na Tanzania Bara) za Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais.
v.
Vikao ishirini
na nane (28) vimefanyika vya Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais na
Mabalozi/Wageni Mashuhuri kwa ajili ya kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na
kibiashara baina ya Zanzibar na nchi, Taasisi
na Mashirika wanayotoka. Aidha, Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais alikutana na
Mabalozi wapya 14 wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi ya Kenya, Uganda, Sudan,
China, Korea ya Kusini, Ubelgiji, Qatar, Ufaransa, Uswiss, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, Brazil, Italia, Uturuki na Oman.
vi.
Ofisi imeendelea kushughulikia malalamiko, kero na
migogoro ya wananchi yanayohusu masuala ya ardhi, nyumba, fidia na kesi za
maeneo ya uwekezaji. Jumla ya malalamiko 53 yamepokelewa
na kuwasilishwa kwa Taasisi zinazohusika na masuala hayo yanayolalamikiwa ili
kupatiwa ufumbuzi. Ofisi inaendelea kufuatilia utatuzi wa malalamiko hayo.
Miongoni mwa malalamiko hayo 28 yamepatiwa
ufumbuzi na Ofisi inaendelea na kufuatilia hatua zinazochukuliwa katika
kuyapatia ufumbuzi malamiko yaliyobakia.
vii.
Ofisi imefanya matengenezo ya kawaida katika nyumba za
makaazi ya Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais za Mazizini Unguja na Dodoma. Matengenezo hayo yalihusisha uzibaji wa nyufa
katika nyumba kuu, marekebisho ya vifaa vya umeme, matengenezo ya jiko na
upakaji wa rangi. Aidha, matengenezo makubwa yamefanyika katika makaazi ya
Mheshimiwa Makamu wa Pili ya Dar es Salaam. Pia, Ofisi imezipatia samani mpya nyumba za
makaazi ya Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais zilizopo Mazizini Unguja na Dar es
Salaam.
viii.
Ofisi imeendelea kuratibu utekelezaji wa ahadi za
Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais katika kusaidia shughuli za maendeleo ya
wananchi zikiwemo madawati katika Skuli za Fujoni, Mangapwani, Kitope na
Mahonda kuipatia mashine ya uchapishaji (Photocopy machine) na Kompyuta katika
Skuli za Sekondari ya Kitope, Mahonda, Kiombamvua na Fujoni. Ujengaji na uingizaji wa vifaa katika maabara
katika skuli za Fujoni na Kitope. Ujenzi wa Banda la Skuli ya Mahonda na Skuli
ya Maandalizi ya Kiombamvua. Kuchangia Jumuiya ya Siti Binti Saad, ZANAB,
Ushirika wa wafuga mbuzi wa Mangapwani na wananchi wa Katavi waliopatwa na
Maafa. Vile vile, kuchangia viyoyozi (AC) katika chumba cha wagonjwa mahututi
(ICU) cha Hospitali ya Mnazi Mmoja na fedha taslim Shilingi 45,000,000.00
zilizotolewa kwa wananchi mbali mbali za kusaidia huduma za kijamii.
2. Programu ya Uratibu wa Shughuli za
Serikali (CO12)
|
28.0
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais kupitia Programu hii imetekeleza kazi zifuatazo:-
i)
Ofisi kupitia Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa
imeratibu na kutoa misaada ya kibinaadamu kwa waathirika wa majanga/maafa
yaliyotokea ambapo jumla ya wananchi wanne (4) Unguja na kumi (10) Pemba
wamepatiwa misaada hiyo.
ii)
Ofisi imeendelea na ujenzi wa Kituo cha Huduma za Mawasiliano
ya Dharura za Kimaafa (Emergency Operation Centre) kilichopo Maruhubi.
iii)
Ofisi imefanya tathmini ya hali ya maafa na kutoa
mafunzo ya kukabiliana na maafa katika Shehia 50 (40 Unguja na 10 Pemba). Aidha,
jumla ya vipindi 18 vya redio na televisheni vinavyoeleimisha masuala ya
kukabiliana na maafa vimerushwa hewani kupitia Shirika la Habari la Zanzibar
(ZBC) na Redio Jamii za Mtegani Makunduchi na Tumbatu.
iv)
Ofisi imeratibu ushiriki wa viongozi na wananchi wa
Zanzibar katika Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara
zilizofanyika Dar es Salaam, tarehe 9 Disemba, 2016. Aidha, Ofisi ilifanikisha
ushiriki wa viongozi na watendaji katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika mjini Dodoma.
v)
Ofisi imeratibu na kusimamia Maadhimisho ya Sherehe za
Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kusimamia shughuli zote zilizopangwa
kutekelezwa katika maadhimisho hayo. Miongoni mwa shughuli hizo ni uwekaji wa
mawe ya msingi na ufunguzi wa miradi ya maendeleo katika Wilaya zote za
Zanzibar, urushaji wa fashifashi na kilele cha Sherehe katika Uwanja wa Amaan.
Katika Sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar jumla ya miradi 19 iliwekewa
mawe ya msingi na miradi 32 ilifunguliwa.
vi)
Ofisi imeratibu Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa
Zanzibar (Karume Day) ambapo viongozi na wananchi walisoma Hitma na Dua ya
kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la
Mapinduzi, Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na Waasisi na Viongozi
wengine wa Zanzibar waliotangulia mbele ya haki.
vii)
Ofisi
imekusanya taarifa za utekelezaji ya miezi kumi na nane (18) ya Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 kutoka Wizara na Taasisi za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
viii)
Ofisi imeendelea kuratibu utekelezaji wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jimbo kwa kufuatilia marejesho ya matumizi ya fedha za mwaka
2015/2016 pamoja na kufuatilia miradi iliyotekelezwa kupitia fedha za Mfuko
huo. Ofisi pia imetoa mafunzo juu ya sheria na uendeshaji wa Mfuko wa Maendeleo
ya Jimbo kwa Wajumbe wa Kamati zote za Mfuko huo wakiwemo Wakurugenzi wa
Halmashauri zote za Zanzibar ambao pia ni Makatibu wa Kamati hizo. Vile vile,
Ofisi imesimamia malipo kwa kipindi cha Julai – Machi cha mwaka 2016/2017 kwa
Majimbo 46 ya Unguja na Pemba.
ix)
Ofisi inaendelea na uimarishaji wa tovuti ya Serikali
kwa kutoa habari za maendeleo ya kijamii na kiuchumi pamoja na kuendelea
kuziunganisha Taasisi za Serikali katika tovuti hiyo.
x)
Ofisi imeratibu utoaji wa vibali 61 kwa watafiti kwa
ajili ya kufanya tafiti zilihusu maeneo ya mazingira, ustawi wa jamii, elimu,
historia, maji, ardhi, utalii, uvuvi, vyombo vya habari pamoja na uchumi. Ofisi
pia imeratibu kikao cha Kamati ya Kisekta ya Utafiti ya Zanzibar ambacho
kilijadili kwa upana mwenendo wa shughuli za utafiti na kupitia maombi mapya ya
utafiti yaliyowasilishwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
xi)
Ofisi imeratibu na kushiriki katika vikao vya masuala
ya Muungano ikiwemo Kikao cha Mawaziri wa SMZ na SMT na Kikao cha Kamati ya
Pamoja ya SMZ na SMT. Aidha, Ofisi imeratibu na kushiriki vikao kumi (10) vya
mashirikiano baina ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na
Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT).
xii)
Ofisi imeshiriki katika vikao 18 vya Wizara, Taasisi na
Mashirika ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi za Kibalozi
za nchi za nje au Mashirika ya Kikanda na Kimataifa.
xiii)
Ofisi imeratibu vikao Tisa (9) vya kujadili masuala ya Muungano
ambavyo vilianza na ngazi ya Wataalamu (Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja ya SMZ
na SMT), Makatibu Wakuu wa SMZ na SMT, Mawaziri wa SMZ na SMT pamoja na kikao
kimoja cha Kamati ya Pamoja ya SMZ na SMT kinachoongozwa na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
xiv)
Ofisi imesimamia Programu ya TASAF III ambapo malipo
kwa Kaya masikini yamefanyika katika Shehia 204 (126 Unguja na Pemba 78) na
jumla ya Shilingi 5,052,368,000
zimelipwa kwa wastani wa Kaya masikini 32,700. Aidha, jumla ya Shilingi 397,412,400 zimelipwa kwa Kaya 11,682
katika utekelezaji wa Miradi ya Ajira za Muda kwa Walengwa kupitia Programu
hiyo.
xv)
Katika kusimamia miradi ya
Muungano, Ofisi imefanya ziara ya kutembelea miradi ya Muungano iliyopo
Zanzibar ili kuona utekelezaji wa miradi hiyo na changamoto zinazojitokeza ili
kuchukua hatua zinazostahiki. Baadhi ya miradi hiyo ni Mpango wa Kunusuru Kaya
Masikini wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III), Mradi wa Kutengeneza
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mradi wa Kuimarisha Huduma za Mifugo (ASDPL), na
Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya Masoko, Kuongeza Thamani na Huduma za Fedha
Vijijini (MIVARF).
xvi)
Ofisi imeendelea kuratibu shughuli za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar huko Dar es Salaam kwa kuhudhuria mikutano/vikao 45 vya
majadiliano na mashirikiano baina ya Wizara na Taasisi za SMZ na SMT na Taasisi
nyengine za Kibalozi na Washirika wa Maendeleo huko Dar es Salaam.
xvii)
Ofisi imeendelea kuratibu shughuli za SMZ Dar es Salaam
kwa kuhudhuria mikutano/vikao 45 vya majadiliano na mashirikiano baina ya
Wizara na Taasisi za SMZ na SMT na Taasisi nyengine za Kibalozi na Washirika wa
Maendeleo huko Dar es Salaam.
xviii)
Ofisi imeratibu vikao vitatu (3) vya
Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu na vikao vitatu vya maafisa waratibu wa
masuala ya Watu wenye Ulemavu wa Wizara kwa lengo la kujadili changamoto na
maendeleo ya Watu wenye Ulemavu.
xix)
Ofisi imeratibu Mafunzo kwa vikundi 14 vya Watu wenye Ulemavu
katika azma ya Serikali ya kuvijengea uwezo vikundi hivyo ili viweze kuzalisha
kwa tija kuweka misingi imara ya kujiari wenyewe. Aidha, wajasiriamali wenye
ulemavu wameshiriki katika maonesho ya kibiashara ili kuwajengea uwezo wa
kujiamini katika kuzalisha bidhaa bora na kuzitafutia masoko ya ndani na nje ya
nchi.
xx)
Jumuiya tano (5) za Watu wenye Ulemavu zimepatiwa
ruzuku ili ziweze kusaidia katika shughuli zao za kiutendaji.
xxi)
Ofisi imefuatilia kesi sita (6) za udhalilishaji wa
Watu wenye Ulemavu zilizoripotiwa katika maeneo mbali mbali ya Unguja (5) na
Pemba (1) ambazo tayari zimeshapatiwa ufumbuzi.
xxii)
Ofisi imewapatia Watu wenye Ulemavu wa Unguja na Pemba
visaidizi 234 vikiwemo, fimbo nyeupe, mafuta ya kulainisha ngozi (lotion) na
viti vya magurudumu mawili.
xxiii)
Ofisi pia imeendelea kukuza uelewa wa
jamii juu ya masuala ya watu wenye ulemavu kwa kurusha vipindi 22 (20 radio na
2 TV) na igizo moja “Talk show” na pamoja na kuendesha mikutano ya uhamasishaji
kwa makundi mbali mbali ya kijamii.
3. Programu
ya Usimamizi wa Shughuli za Upigaji Chapa (C013)
|
29.0
Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Programu hii imetekeleza
yafuatayo:-
Ofisi kupitia
Wakala wa Serikali wa Uchapaji imeendelea kutoa huduma za uchapaji kwa kazi
zote zilizowasilishwa na Wizara/Taasisi za Serikali na watu binafsi. Miongoni
mwa kazi hizo ni Hansard za Baraza la Wawakilishi, Miswada ya Sheria, majarida,
mabango ya matangazo, vitabu vya risiti, kalenda za ukutani na za mezani na
“Cash books” na “Log books”.
4. Programu ya
Mipango na Utawala (C014)
|
30.0
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Programu hii imetekeleza kazi zifuatazo:-
i.
Ofisi imesimamia shughuli za uendeshaji wa Ofisi za
kila siku kwa kufanya malipo ya huduma za kiofisi na uendeshaji, kuimarisha
huduma za usafiri za ofisi kwa kufanya matengenezo ya vipando (gari na vespa).
Vile vile, Ofisi imelifanyia matengenezo jengo la Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais, Vuga ikiwa ni pamoja na kulipaka rangi. Aidha, Ofisi ilitoa mafunzo ya
matumizi ya vifaa vya uzimaji moto na kuweka vifaa vya huduma ya kwanza (first
aid kit) kwa ajili ya dharura.
ii.
Ofisi imeratibu na kuandaa makisio ya mishahara na
maposho ya watumishi pamoja na Mpango wa Rasilimali Watu wa miaka mitano (5)
kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 hadi 2021/2022. Vile vile, Ofisi imefanya malipo ya baada ya
saa za kazi, posho la kukaimu kwa wafanyakazi waliostahiki. Ofisi pia
imewalipia wafanyakazi ishirini na mbili (22) ada na gharama nyengine za masomo
ya muda mrefu.
iii.
Ofisi kupitia Kitengo kinachosimamia Programmu za
Kukabiliana na Malaria, UKIMWI na Kifua Kikuu Zanzibar zinazofadhiliwa na Mfuko
wa Dunia (ZGFCCM) imeendesha vikao vitatu vya kawaida vya robo mwaka na vikao 4
vya dharura vya Kamati vilivyojadili utekelezaji wa shughuli za mfuko huo na
kuandaa maombi ya fedha ya mwaka 2018 – 2020 kwa miradi ya Malaria, UKIMWI na
Kifua Kikuu. ZGFCCM pia imepitisha Mpango Kazi na bajeti yake ya miaka mitatu
(2017 – 2019).
iv.
Ofisi imeandaa taarifa za utekelezaji wa miradi ya
maendeleo ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais za kila mwezi pamoja na taarifa za
utekelezaji wa kazi za kawaida na miradi ya maendeleo kwa kila kipindi cha robo
mwaka 2016/2017 pamoja na kutayarisha bajeti ya mwaka 2017/2018.
v.
Ofisi imefanya ziara ya ufuatiliaji na tathmini kwa
miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Idara na Taasisi za Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais. Katika ziara hiyo Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kukabiliana na Maafa,
Programu ya TASAF III, Mradi wa Afya ya Uzazi Mradi wa Kupunguza Madhara
Yatokanayo na Matumizi ya Dawa za Kulevya na Miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya
Jimbo ilikaguliwa na kuona hatua zilizofikiwa za utekelezaji wake ikiwemo
mafanikio na changamoto zinazoikabili.
BARAZA LA WAWAKILISHI:
Programu
1: Kutunga
Sheria, Kupitisha Bajeti na Kusimamia Taasisi za Serikali (CO21)
|
Programu 2: Uongozi na Utawala wa Baraza la
Wawakilishi (CO22)
|
31.0
Mheshimiwa Spika,
Kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Baraza la Wawakilishi kupitia
Programu hizi limetekeleza yafuatayo:-
i.
Afisi ya Baraza la Wawakilishi imeratibu kazi za Kamati
zote saba za Kudumu ambapo Kamati hizo zilizipitia Taasisi mbali mbali za
Serikali na kuwasilisha ripoti zao katika Mkutano wa
Tano wa Baraza hili uliofanyika mwezi wa Februari, 2017.
ii.
Baraza la Wawakilishi lilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa
Bunge la Afrika ya Mashariki (East African Legislature Assembly– EALA)
uliofanyika kuanzia tarehe 10 Oktoba, 2016 hadi tarehe 20 Oktoba, 2016. Mkutano
huo ulipata baraka ya kuhutubiwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.
iii.
Afisi ya Baraza la Wawakilishi iliratibu Mikutano minne
(4) ya Baraza la Wawakilishi ambapo katika mikutano hiyo jumla ya Miswada kumi
na tano (15), Hoja za Wajumbe nne (4) pamoja na ombi la wananchi (Petition)
moja (1) iliwasilishwa. Aidha, jumla ya
maswali 274 ya msingi na 676 ya nyongeza yaliulizwa na kujibiwa.
iv.
Afisi ya Baraza iliratibu ziara na mikutano ya viongozi
wa Baraza katika Nchi za Mauritius, Cuba na Iran ambazo Mheshimiwa Spika
aliongoza ujumbe wa baadhi ya Wajumbe wa Baraza na watendaji katika ziara na
mikutano hiyo. Miongoni mwa mikutano
hiyo ni Mkutano wa Kamati Tendaji ya Umoja wa Jumuiya ya Mabunge (CPA) Kanda ya
Afrika uliofanyika Dar-es-Salaam, Tanzania.
Mkutano ambao ulijumuisha na mikutano mengine kama vile Jumuiya ya Umoja
wa Makatibu Mezani (SoCAT) uliohudhuriwa na Katibu wa Baraza.
TUME YA UCHAGUZI
YA ZANZIBAR
:
Programu
1: Uendeshaji wa Shughuli za Uchaguzi
|
Programu
2: Usimamizi wa Kazi za Utawala za
Uendeshaji wa Shughuli za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
|
32.0
Mheshimiwa Spika, hadi mwezi wa Machi mwaka wa fedha
2016/2017, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ilitekeleza Programu hizo kama
ifuatavyo:-
i.
Katika kuendeleza Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
Ofisi kupitia Tume ya Uchaguzi imeshughulikia mashauri 1,522 juu ya masuala ya
wapiga kura ambapo miongoni mwao 298 ni maombi yanayohusu shahada zilizopotea, 335
ni masuala juu ya uhamisho wa wapiga
kura, 290 ni masuala yanayohusu masahihisho ya taarifa za wapiga kura na
mashauri 599 yanayohusu uchukuaji wa shahada za kupigia kura.
ii.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iliendesha Uchaguzi Mdogo
katika Wadi ya Ndagoni tarehe 18 Februari, 2017 ili kujaza nafasi iliyoachwa
wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa Diwani wa Wadi hiyo, Mheshimiwa Juma Ali
Kombo. Jumla ya Shehia tatu zilihusika katika uchaguzi huo ambazo ni Ndagoni,
Wesha na Michungwani. Vyama viwili vya CCM na ADC vilishiriki katika uchaguzi
huo ambapo mgombea wa CCM alishinda katika uchaguzi huo kwa asilimia 94.7.
iii.
Tume ya Uchaguzi imefanya mapitio ya Daftari la Kudumu
la Wapiga kura ambapo jumla ya wapiga kura 6,743 kutoka Wilaya zote za Unguja
na Pemba waliopoteza sifa ya kupiga kura wameondolewa katika daftari hilo.
iv.
Tume ya Uchaguzi imewasilisha Ripoti ya Uchaguzi Mkuu
wa Zanzibar wa Oktoba, 2015 na Uchaguzi
wa Marudio wa Machi 2016 kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi. Jumla ya nakala
elfu moja na mia moja (1,100) za ripoti hiyo zilichapishwa na kusambazwa kwa
wadau wa uchaguzi wakiwemo Taasisi za Serikali na zisizokuwa za Serikali na
maktaba za Taasisi za Elimu ya Juu za Zanzibar.
v.
Tume ya Uchaguzi imeendelea kutoa elimu ya wapiga kura
katika ngazi ya Shehia ambapo jumla Masheha na Wajumbe wa Baraza la Masheha wa Shehia
132 sawa na asilimia 34 za Unguja na Pemba wamepatiwa elimu hiyo.
vi.
Ofisi imewapatia mafunzo wafanyakazi watatu (3) katika ngazi
ya Shahada ya Kwanza na ya Pili ili kuleta ufanisi katika kazi.
TUME YA KITAIFA YA KURATIBU NA
UDHIBITI WA
Programu 2: Uendeshaji na Uratibu wa Tume ya Dawa
za
kkulevya
Programu 1: Udhibiti wa Dawa za Kulevya:
|
DAWA ZA KULEVYA:
Programu
2: Uendeshaji na Uratibu wa Tume ya Dawa za Kulevya:
|
33.0
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Tume ya
Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya Zanzibar ilitekeleza
Programu hizo kama ifuatavyo:-
i.
Kutoa mafunzo juu ya udhibiti wa dawa za kulevya kwa
wadau katika Shehia zenye bandari rasmi na zisizo rasmi juu ya kuweka wazi
mbinu mbali mbali zinazotumiwa na wahalifu katika kupitisha dawa za kulevya.
Jumla ya Shehia 94 zenye bandari rasmi na zisizo rasmi zilipatiwa mafunzo hayo
ambayo yalihusisha washiriki 186.
ii.
Kufanya mkutano minne (4) ya Kamati ya Kitaalamu ambayo
iliweka na kupanga mikakati ya udhibiti wa dawa za kulevya pamoja na
uimarishaji wa kinga dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.
iii.
Kuzisaidia Nyumba za Upataji nafuu (Sober Houses)
ambapo jumla ya nyumba tisa (9) zimepatiwa ruzuku kwa lengo la kuzijengea
mazingira bora ya kazi ili ziweze kukabiliana na changamoto zake.
iv.
Ofisi kupitia Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti
Dawa za Kulevya imeendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya athari za Dawa za
Kulevya ambapo jumla ya vipindi 10 vya redio na vitatu (3) vya TV vilirushwa
hewani, kufanya ziara za utoaji taaluma katika Skuli 53 ambapo jumla ya
wanafunzi 5,321 (Wanawake 2,834 na Wanaume 2,487) walipatiwa taaluma hiyo. Pia ziara kama hizo zimefanyika katika Shehia
36 za Unguja na Pemba.
v.
Ofisi kupitia Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti
wa Dawa za Kulevya ilifanya mkutano maalum na wazazi wa vijana walioathirika na
dawa za kulevya (Family therapy) katika Skuli ya Fujoni. Lengo ni kuwakutanisha
wanaotumia na walioacha kutumia dawa za kulevya, wazazi, walimu na viongozi wa
Shehia ili kuwasaidia vijana hao waweze kujiunga na nyumba za marekebisho ya
tabia.
TUME YA UKIMWI ZANZIBAR:
Programu 1:
Kuratibu Muitiko wa Taifa wa UKIMWI(C051)
|
Programu 2: Utawala
na Uendeshaji wa Tume ya UKIMWI(C052)
|
34.0
Mheshimiwa Spika, kazi za Programu hizi
zimetekelezwa na Tume ya UKIMWI kama ifuatavyo:-
i.
Ofisi kupitia Tume ya UKIMWI imeandaa mpango wa utekelezaji wa Mkakati wa Tatu wa Taifa wa
UKIMWI, Mkakati wa Makundi maalum na mpango wake wa utekelezaji (Action Plan),
Programu ya Mipira ya Kinga (condom programming), Muongozo wa UKIMWI kwa
Muitiko wa Jamii (HIV Guidelines for Community Response) na Mpango wa UKIMWI wa Vijana.
ii.
Ofisi imewapa mafunzo ya uelimishaji rika vijana 60
wenye umri baina ya miaka 10-24 juu ya masuala ya UKIMWI na afya ya uzazi ili
wawafundishe vijana wenzao katika shehia12 zilizoko Wilaya za Kaskazini A,
Unguja na Micheweni Pemba. Vijana hao waliweza kuwafikia vijana wenzao 2,374
ambapo Unguja ni 910 na Pemba 1,464 wakiwemo wanawake 1,040 na wanaume1,334.
iii.
Ofisi ilitoa mafunzo kwa wadau 213 juu ya ukondoeshaji
wa masuala ya UKIMWI na afya ya uzazi katika shughuli zao za kila siku. Jumla ya wafanyakazi 52 wa sekta za Serikali,
31 wa Asasi za Kiraia na Viongozi wa Dini 130 walipata mafunzo hayo.
iv.
Ofisi imeendelea kuratibu programu za makundi maalum
ambapo jumla ya watu 1,100 walifikiwa kwa kupatiwa huduma mbali mbali za kinga
ikiwemo elimu juu ya UKIMWI na maradhi ya kujamiiana, upatikanaji wa huduma za
afya, kuhamasishwa kupima VVU na kuzitumia huduma za tiba kwa wanaoishi na VVU.
v.
Ofisi ilisambaza vipeperushi 3,000 na kurusha hewani
vipindi 84 vinavyohamasisha masuala ya UKIMWI na afya ya uzazi vilivyorushwa
katika redio 4 za jamii (Tumbatu, Makunduchi, Micheweni na Mkanyageni) na ZBC,
Hits FM na Zenji FM.
vi.
Tume ya UKIMWI imefanya ufuatiliaji kwa Taasisi za
Serikali na zisizo za Serikali kwa ajili ya kupata taarifa za utekelezaji wa
shughuli zao kwa kipindi cha mwaka mmoja (Januari hadi Disemba, 2016) ili
kupima utekelezaji wa muitiko wa Taifa dhidi ya UKIMWI na kuandaa ripoti ya
pamoja itakayoonyesha hatua zinazochukuliwa na wadau hao katika mapambano dhidi
ya UKIMWI.
vii.
Ofisi
ilitoa mafunzo ya Sheria Nam. 18 ya Kukinga na Kusimamia Masuala ya UKIMWI ya
mwaka 2013 kwa washiriki 163 wakiwemo wataalamu wa afya 55, viongozi wa dini
25, wawakilishi wa sekta za Serikali 43 na wasaidizi wa sheria 40. Mafunzo hayo
yalitolewa kwa kushirikiana na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar. Aidha, Ofisi imewapa mafunzo wafayakazi 25 wa
vituo 7 vya huduma za tiba na vituo rafiki juu ya ujumuishaji wa huduma za
UKIMWI na afya ya uzazi katika vituo vyao.
viii.
Ofisi
imefanya mikutano 8 ya kuratibu muitiko wa UKIMWI kwa sekta za Serikali, Asasi
za Kiraia, Taasisi za Kidini na Taasisi zinazofanya kazi na makundi maalum.
UTEKELEZAJI KIFEDHA:
35.0
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa
fedha 2016/2017 Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kupitia Programu zake 12 na
Programu Ndogo 24 iliidhinishiwa kutumia jumla ya Shilingi 26,142,549,000 kwa kazi za kawaida na hadi kufikia Machi
2017 imetumia Shilingi 16,934,374,410 ambazo ni sawa na asilimia 65.
Ofisi pia iliidhimishiwa jumla ya Shilingi
9,849,526,000 kwa kazi za Maendeleo
na hadi kufika Machi 2017 imetipatiwa Shilingi
7,472,505,100 ambazo ni sawa
na asilimia 76 (Angalia Kiambatanisho Nam. 1 na 2).
36.0
Mheshimiwa Spika, Ofisi vile vile imekusanya Shilingi 546,950,772
ambayo ni asilimia 68 ya Shilingi 806,126,000 ilizopangiwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 (Angalia
Kiambatanisho nam.3).
BAJETI KWA MWAKA
WA FEDHA 2017/2018:
37.0
Mheshimiwa Spika, Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais pamoja na taasisi zake kwa mwaka 2017/2018 itaendelea
kusimamia na kutekeleza programu kuu kumi na mbili (12) na programu ndogo
ishirini na nne (24). Kupitia Programu hizo, Ofisi imepanga kutekeleza
kazi zifuatazo:-
Programu ya kwanza: Uratibu wa Shughuli za Makamu wa Pili wa Rais (C011)
|
38.0
Mheshimiwa Spika, lengo la
Program hii ni kuimarisha utendaji wa kazi kwa Ofisi ya Faragha ya Makamu wa
Pili wa Rais. Matarajio ya muda mrefu ni kuimarika kwa Ofisi hii na kutoa
huduma bora kwa Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018, Ofisi kupitia Programu ya Uratibu
wa Shughuli za Makamu wa Pili wa Rais imepanga kufanya
yafuatayo:
a)
Kuratibu
ziara 40 za Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais za ndani ya nchi na ziara mbili
(2) za nje ya nchi;
b)
Kuimarisha
mashirikiano na mahusiano mema ya Kitaifa na Kimataifa kwa kukutana na Mabalozi
pamoja na Wageni Mashuhuri;
c)
Kuratibu
na kufuatilia utekelezaji wa ahadi za Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais
zinazolenga kuleta maendeleo katika jamii;
d) Kuyafanyia kazi malalamiko,
migogoro na kero za wananchi kwa kushirikiana na Taasisi husika;
e)
Kufanya
matengenezo makubwa katika makaazi ya Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais yalioko
Dodoma na kufanya matengenezo ya kawaida katika makaazi ya Dar es Salaam na
Zanzibar;
f)
Kuendelea
kuwapatia mafunzo wafanyakazi sita (6) wa Ofisi ya Faragha kwa kiwango cha
Stashahada na Cheti pamoja na kuwapatia stahiki za likizo wafanyakazi.
Programu ya Pili: Uratibu wa
shughuli za Serikali (C012)
|
39.0
Mheshimiwa Spika, programu hii
lengo lake kubwa ni kuweka mfumo imara na endelevu kwa Uratibu wa Shughuli za
Serikali, ambapo matarajio ya muda mrefu ni kutoa huduma bora za Serikali kwa
jamii.
Programu hii ina
programu ndogo tano ambazo ni:-
i.
Kukabiliana na Maafa;
ii.
Sherehe na Maadhimisho ya
Kitaifa pamoja na Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa;
iii.
Shughuli za SMZ, SMT, Utafiti na Masuala ya Muungano;
iv.
Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dar es
Salaam;
v.
Usimamizi wa masuala ya Watu wenye Ulemavu;
Programu ndogo C0121 Kukabiliana
na Maafa:
40.0
Mheshimiwa Spika, Programu ndogo
ya Kukabiliana na Maafa ina lengo la kujenga uhimili wa jamii katika
kukabiliana na maafa kabla na baada ya kutokea. Huduma ambazo zinazotarajiwa
kutolewa ni Uratibu wa shughuli za Kukabiliana na Maafa ikiwemo kutoa mafunzo
kwa jamii, kuwahudumia waathirika wa majanga na maafa pamoja na kuandaa na
kutoa miongozo inayosimamia utekelezaji wa kazi za maafa.
41.0
Mheshimiwa Spika, katika mwaka
wa fedha 2017/2018, Programu ndogo (C0121) imepanga kufanya yafuatayo:-
a)
Kuanzisha
Mfumo wa Tahadhari za Mapema pamoja na kuimarisha Mfumo wa Mawasiliano Wakati
wa Dharura;
b)
Kutayarisha
na kurusha vipindi vya Redio 20 na Televisheni 12 vya kujiandaa na kukabiliana
na maafa;
c)
Kununua
vifaa vya huduma za kibinadamu Unguja na Pemba;
d)
Kuainisha maeneo yaliyo katika hatari ya kukumbwa na majanga/ maafa baharini na nchi kavu;
e)
Kuratibu shughuli za uokozi
na utoaji wa huduma za kibinadamu;
f)
Kufanya
tathmini kwa jamii juu ya uelewa wa masuala mbali mbali ya kukabiliana na maafa;
g)
Kuandaa
midahalo na makongamano kwa wanafunzi wa Skuli za Sekondari na Vyuo Vikuu kwa
lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana
na maafa;
h)
Kufanya
ukaguzi wa majengo yanayotoa huduma kwa jamii juu ya uzingatiaji wa kujikinga
na kukabiliana na majanga/maafa;
i)
Kuwapatia
mafunzo ya muda mrefu na mfupi wafanyakazi
wawili (2) wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa.
Programu
ndogo C0122: Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja na Kuwaenzi Viongozi
wa Kitaifa:
42.0
Mheshimiwa
Spika,
Programu ndogo ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja na Kuwaenzi Viongozi
wa Kitaifa ina lengo la kuwa
na sherehe zenye hadhi na kuwaenzi Viongozi Wakuu wa Kitaifa. Huduma ambazo
zinatarajiwa kutolewa ni uratibu wa shughuli za Sherehe na Maadhimisho
ya Kitaifa pamoja na kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa.
43.0
Mheshimiwa
Spika,
katika mwaka wa fedha 2017/2018, Programu ndogo (C0122) imepanga kufanya
yafuatayo:-
a)
Kuandaa
mazingira mazuri ya Ofisi na utendaji kazi kwa kununua vitendea kazi na
kuendelea kulipia gharama za masomo kwa wafanyakazi watatu (3);
b)
Kuratibu
Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar;
c)
Kuratibu
Hitma na Dua ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na viongozi wengine
waliotangulia mbele ya haki;
d)
Kuratibu
ushiriki wa viongozi na wananchi wa Zanzibar katika maadhimisho na sherehe za Kitaifa
zitakazofanyika nje ya Zanzibar;
e)
Kuliyafanyia
matengenezo eneo lililopo kaburi la Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume lililopo
Kisiwandui na eneo lililopo kaburi la Marehemu Dk. Omar Ali Juma lililopo Wawi,
Pemba;
f)
Kuendelea
kuchangia katika mapato ya Serikali kwa ukodishaji wa vifaa vya sherehe.
Programu ndogo (C0123): Shughuli
za SMZ, SMT, Utafiti na Masuala ya Muungano:
44.0
Mheshimiwa
Spika, katika
mwaka wa fedha 2017/2018 Programu ndogo ya
Uratibu wa Shughuli za SMZ, SMT, Utafiti na Masuala ya Muungano (C0123) imepanga kufanya yafuatayo:-
a)
Kuendelea kuratibu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya
Chama Tawala (CCM) ya 2015 – 2020;
b)
Kuratibu shughuli za Muungano na Miradi ya Muungano
ndani ya Zanzibar;
c)
Kuratibu vikao vya Mashirikiano kati ya Wizara na Taasisi
za SMZ na SMT;
d)
Kuratibu shughuli za utafiti nchini;
e)
Kuratibu, kusimamia na kuendesha Mfuko wa Maendeleo ya
Jimbo;
f)
Kuratibu shughuli za Serikali katika ngazi za Taifa,
Mikoa na Wilaya ikiwemo uratibu na ufuatiliaji wa utekelezaji wa ahadi za
Viongozi Wakuu wa Kitaifa na kusaidia kuyatafutia ufumbuzi malalamiko ya
wananchi;
g)
Kusimamia uendeshaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
Zanzibar kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF III);
h)
Kuwapatia mafunzo ya muda
mrefu na mfupi wafanyakazi watatu (3) wa Idara.
Programu Ndogo
C0124: Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dar es Salaam
45.0
Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Shughuli
za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dar es Salaam ina lengo la kuimarisha
utoaji wa huduma kwa Taasisi za SMZ kwa upande wa Tanzania Bara pamoja na
kukuza na kuimarisha ushirikiano kati ya Taasisi/Wizara za SMZ na SMT, Washirika wa Maendeleo, Ofisi za Kibalozi na Asasi
nyengine za Kimataifa.
46.0
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2017/2018, Ofisi kupitia
Programu ndogo CO124 imepanga kufanya yafuatayo:-
a)
Kuratibu
utekelezaji wa shughuli za SMZ zilizopangwa kufanyika Tanzania Bara ikiwa ni
pamoja na kuziwakilisha Taasisi na Wizara za SMZ katika mikutano na vikao na
kuratibu na kushiriki ziara za Wizara na Taasisi za SMZ Tanzania Bara;
b)
Kuratibu
mashirikiano baina ya Wizara/Taasisi za SMZ na SMT, Ofisi za Kibalozi na
Taasisi za Kimataifa;
c)
Kuweka
mazingira mazuri ya kazi za ofisi kwa kuhakikisha upatikanaji wa maslahi ya
wafanyakazi, vifaa na huduma muhimu za kiofisi;
d)
Kuwapatia
mafunzo wafanyakazi wawili (2) ili kuwaongezea utaalamu;
e)
Kufuatilia
utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na Ofisi za kibalozi na mashirika ya
Kimataifa ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa.
Programu Ndogo C0125: Usimamizi
wa Masuala ya Watu Wenye Ulemavu:
47.0
Mheshimiwa
Spika, Programu ndogo ya Usimamizi wa Masuala ya Watu wenye Ulemavu
lengo lake kuu ni kuhakikisha kuwa haki na fursa kwa Watu wenye Ulemavu
zinapatikana bila ya vikwazo. Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Programu ndogo
hii imepanga
kutekeleza yafuatayo:-
a)
Kufanya mapitio ya usajili wa Watu wenye Ulemavu katika
Mkoa wa Kaskazini Unguja na Mkoa wa Kaskazini Pemba;
b)
Kusimamia upatikanaji haki na fursa sawa kwa Watu wenye
Ulemavu;
c)
Kuratibu ukondishwaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu
na kuwajengea uwezo Watu wenye Ulemavu pamoja na Taasisi zao;
d)
Kufanya uhamasishaji wa jamii juu ya masuala ya Watu wenye
Ulemavu;
e)
Kuimarisha mazingira ya kazi na kuwajengea uwezo
wafanyakazi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi.
Programu ya Tatu: Usimamizi wa Shughuli za Upigaji Chapa (C013)
|
48.0
Mheshimiwa
Spika, Programu hii lengo lake ni kukiimarisha Kiwanda cha Upigaji Chapa
cha Serikali ili kutoa huduma bora za machapisho na kwa ufanisi. Katika mwaka
wa fedha 2017/2018 programu hii imepanga kutekeleza yafuatayo:-
a) Kutoa huduma za machapisho ya Gazeti Rasmi la Serikali, Miswaada ya Sheria, Sheria
na Nyaraka mbali mbali
za Serikali;
b) Kutoa machapisho
mbali mbali na huduma ya kuuza vifaa vya ofisini na kuandikia kwa Taasisi/Wizara
za Serikali na sekta binafsi yatakayokidhi mahitaji ya uchapishaji na kukuza
mapato ya Wakala;
c) Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wanne (4) Wakala
Serikali wa Uchapaji pamoja na kuwapatia stahiki zao;
d) Kuimarisha ubora wa mitambo ya uchapaji kwa
kuiweka katika mazingira mazuri na kuifanyia matengezo ya mara kwa mara kila
itakapohitajika;
e) Kufanya utafiti kwa ajili ya kuimarisha ufanisi
wa machapisho na ukuzaji
wa soko la uchapaji ndani na nje ya nchi.
Programu ya Nne: Uendeshaji na Uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais (C014)
|
49.0
Mheshimiwa
Spika, lengo
la Programu hii ni kuimarisha mazingira bora ya wafanyakazi,
usimamizi wa mipango na shughuli za Ofisi. Matokeo yanayotarajiwa ni kuimarika
mipango na utendaji kazi na kutoa huduma bora kwa wafanyakazi na wadau mbali
mbali wa Ofisi hii. Programu hii ina programu ndogo tatu (3) ambazo ni:-
i.
Uongozi na Utawala
ii.
Mipango, Sera na Utafiti
iii.
Ofisi Kuu Pemba
Programu ndogo (C0141): Uongozi
na Utawala:
50.0
Mheshimiwa
Spika,
Programu hii ndogo ina lengo la kuimarisha mazingira
bora ya kufanyia kazi na usimamizi wa shughuli za Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais. Matokeo yanayotarajiwa ni matumizi bora ya rasilimali, wafanyakazi wenye
ujuzi na uzoefu ili kuongeza ufanisi na tija katika utendaji kazi.
51.0
Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka
wa fedha 2017/2018 programu ndogo ya
Uongozi na Utawala imepanga kutekeleza kazi zifuatazo:-
a. Kusimamia shughuli za
uendeshaji wa Ofisi za kila siku ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya
kufanyia kazi vikiwemo Kompyuta tatu, mashine ya ‘photocopy’, vifaa vya kuandikia, vifaa vya usafi, umeme, maji,
mawasiliano, mafuta, huduma za usafiri pamoja na matengenezo ya vifaa na
vipando;
b. Kuendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu
kwa wafanyakazi wanne (4) wa Idara pamoja na kuratibu mafunzo ya wafanyakazi 37 wa Idara za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
pamoja na kuratibu kupatiwa mafunzo ya awali (Induction Course) kwa wafanyakazi
wapya;
c. Kufanya semina ya Sheria na Kanuni za
Utumishi wa Umma pamoja na mafunzo yanayohusiana na masuala ya UKIMWI na
maradhi yasiyoambukiza;
d. Kufanya matengenezo madogo madogo ya miundoumbinu
ya Ofisi ikiwemo umeme pamoja na njia ya watu wenye mahitaji maalumu katika
Jengo la Ofisi, Vuga;
e. Kuimarisha Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu
za Ndani na Kitengo cha Mawasiliano na Habari kwa kuvipatia vitendea kazi.
Programu ndogo
(C0142): Mipango, Sera na Utafiti:
52.0
Mheshimiwa
Spika, Programu hii ndogo ina lengo la kuandaa na kusimamia Mipango na
Bajeti na kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais. Matokeo yanayotarajiwa ni kuwa na mipango endelevu na yenye
kuleta matokeo bora na endelevu.
53.0
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018,
Programu ndogo hii imepanga kutekeleza kazi zifuatazo:-
- Kuandaa Bajeti na kutayarisha Miradi ya
Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2018/2019;
- Kufanya ziara nne (4) za ufuatiliaji na
tathmini ya utekelezaji wa Programu/Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na
Idara/Taasisi zilizomo katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais;
- Kuratibu na kusimamia tafiti zinazofanywa na
Idara na Taasisi zilizomo katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais;
- Kuratibu Sera, Sheria na Miongozo
inayotayarishwa kwa ajili ya shughuli zinazotekelezwa na Ofisi ya Makamu
wa Pili wa Rais;
- Kuwajengea uwezo wafanyakazi watatu (3) wa
Idara ya Mipango, Sera na Utafiti kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi na
muda mrefu;
- Kusimamia ujenzi wa nyumba ya makaazi ya
Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais Pemba;
- Kuratibu utekelezaji wa Miradi ya Kupambana na
UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria kupitia Mfuko wa Dunia (Global Fund).
Programu ndogo (C0143): Ofisi Kuu Pemba:
54.0
Mheshimiwa Spika, lengo kuu la Program hii ndogo ni kuimarisha mazingira bora ya
kufanyia kazi na usimamizi wa shughuli za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,
Pemba. Matokeo yanayotarajiwa ni utendaji na utekelezaji wa kazi za Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais Pemba kwa ufanisi.
55.0
Mheshimiwa Spika, katika mwaka
wa fedha 2017/2018 Ofisi Kuu Pemba
itatekeleza lengo la kuratibu shughuli
za Idara na Taasisi zilizomo katika
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba kama ifuatavyo:-
a)
Kuimarisha mazingira bora ya kufanyia kazi na kusimamia
shughuli za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais;
b)
Kuwapatia
mafunzo ya muda mrefu wafanyakazi 3;
c)
Kuandaa mipango ya Ofisi na bajeti kwa mwaka wa Fedha
2018/2019;
d) Kuimarisha
kazi za usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Programu na Miradi ya Maendeleo iliyo chini
ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Pemba;
e)
Kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa shughuli za
Serikali Pemba;
f)
Kutangaza huduma za Wakala wa Serikali wa Uchapaji
Zanzibar kwa ajili ya kuongeza idadi ya
wateja na mapato;
g)
Kuratibu shughuli za kukabiliana na maafa na kutoa
elimu kwa jamii juu ya kujikinga na kukabiliana na maafa;
h)
Kuratibu shughuli za Watu wenye Ulemavu na kutoa elimu
kwa jamii juu ya haki zao za msingi.
56.0
Mheshimiwa
Spika,
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais pia inaratibu shughuli za Baraza la
Wawakilishi, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na
Udhibiti wa Dawa za Kulevya na Tume ya UKIMWI, ambazo zina Programu Kuu na
Programu Ndogo kama ifuatavyo:-
BARAZA LA
WAWAKILISHI:
57.0
Mheshimiwa Spika,
Baraza
la Wawakilishi linatekeleza Program kuu mbili (2) ambazo ni:
Programu ya tano: Kutunga Sheria, Kupitisha Bajeti na Kusimamia
Taasisi za Serikali
|
58.0
Mheshimiwa
Spika, Programu
hii ina jukumu la kuhakikisha haki na
utawala wa sheria unatelekelezwa Zanzibar, ambapo matarajio yake ya muda mrefu ni kukua kwa demokrasia na uwakilishi wa wananchi. Huduma zinazotolewa ni kujadili, kurekebisha na kupitisha miswada ya
Sheria, kusimamia utendaji wa Taasisi za Serikali na kujadili na kupitisha
bajeti ya Serikali.
Programu ya sita: Uongozi na Utawala wa Baraza la Wawakilishi
|
Mheshimiwa Spika, Programu hii ina jukumu la kuweka mazingira mazuri ya kazi, kuwajengea uwezo Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi na wafanyakazi wa Afisi ya Baraza, ambapo matarajio yake ya muda
mrefu ni kuongezeka kwa ufanisi katika kutekeleza
majukumu ya Baraza na Ofisi.
59.0
Mheshimiwa
Spika,
kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 Baraza la
Wawakilishi kupitia Programu hizi limepanga kutekeleza mambo yafuatayo:-
a) Kufanya mikutano minne (4) ya Baraza la Wawakilishi;
b) Kuziwezesha Kamati za Kudumu za Baraza la
Wawakilishi kufanya kazi zake kwa ufanisi;
c) Kuendelea kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa
watumishi wa Baraza la Wawakilishi;
d) Kuendelea kutoa
mafunzo kwa Wajumbe ili waweze kutekeleza majukumu yao;
e)
Kuendeleza mahusiano na vyombo vyengine vya
Mabunge vya Kanda ya Afrika na ngazi za Kitaifa;
f) Kuendelea kuweka mazingira mazuri ya majengo na Kumbi za Mikutano
pamoja na kutoa huduma bora kwa Wajumbe katika kutekeleza majukumu yao ya
kikatiba.
TUME YA UCHAGUZI
YA ZANZIBAR:
60.0
Mheshimiwa Spika, Tume ya
Uchaguzi inasimamia Programu kuu mbili zifuatazo:-
Programu ya Saba: Uendeshaji wa Shughuli za Uchaguzi
|
61.0
Mheshimiwa Spika, Programu hii
ina jukumu la kukuza demokrasia na umoja wa Kitaifa
ambayo
matarajio yake ya muda mrefu ni kuwa na uchaguzi huru na wa haki na wenye kufuata misingi ya kisheria.
62.0
Mheshimiwa
Spika; katika
mwaka wa fedha 2017/2018 Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kupitia programu hii
imepanga kutekeleza yafuatayo:-
a)
Kuandikisha Wapiga Kura wapya
waliotimiza sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura;
b)
Kuendeleza Daftari la Kudumu
wa Wapiga Kura;
c)
Kuendelea kutoa elimu ya
wapiga kura kwa makundi mbali mbali;
d)
Kuimarisha majengo na kufanya
michoro ya majengo mapya ya Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar;
e)
Kuendelea Kufanya mapitio ya
Sheria ya Uchaguzi Nam. 11 ya mwaka
1984 kwa kuifuta Sheria hiyo na kuanzisha Sheria ya Usimamizi wa Shughuli za
Uchaguzi;
f)
Kutoa elimu ya Uchaguzi kwa Wajumbe na Watendaji wa Ofisi ya Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar.
Programu ya Nane: Usimamizi wa Kazi za Utawala na Uendeshaji wa
Shughuli za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
|
63.0
Mheshimiwa Spika, Programu hii
ina jukumu la kuimarisha usimamizi wa mwenendo wa
shughuli za uchaguzi,
ambayo matarajio yake ya muda mrefu ni uendeshaji bora wa kazi za Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Programu hii inasimamia programu ndogo mbili nazo ni:-
i.
Usimamizi wa kazi za Utawala
na Uendeshaji wa Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
ii.
Usimamizi wa kazi za Utawala
na Uendeshaji wa Ofisi Ndogo ya Tume ya Uchaguzi Pemba.
64.0
Mheshimiwa
Spika,
kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 Tume ya Uchaguzi kupitia programu hii imepanga
kutekeleza mambo yafuatayo:-
a)
Kununua vifaa mbali mbali vya kufanyia kazi za
Ofisi.
b)
Kuwapatia mafunzo ya muda mrefu wafanyakazi
watano (5) katika ngazi na fani mbali mbali za elimu.
c)
Kufanya ununuzi wa gari
mbili kwa ajili ya shughuli za Ofisi.
TUME YA KITAIFA YA KURATIBU NA
UDHIBITI WA DAWA ZA KULEVYA:
65.0
Mheshimiwa
Spika, Tume
ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ina jukumu kuu la
kuratibu mapambano dhidi ya biashara, usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya; kutoa taaluma kwa jamii
juu ya athari za dawa za kulevya pamoja na tiba na ushauri nasaha kwa
waathirika wa dawa hizo. Taasisi hii imepangiwa kusimamia Program Kuu mbili
kama ifuatavyo:-
Program ya Tisa: Udhibiti wa Dawa za Kulevya
|
66.0
Mheshimiwa
Spika, shughuli
zilizopangwa kutekelezwa katika programu hii ni:-
a.
Kuzijengea
uwezo nyumba za upataji nafuu (sober houses);
b.
Kudhibiti uingizaji na
usafirishaji wa dawa za kulevya katika bandari rasmi na zisizo rasmi;
c.
Kuratibu na kuendeleza
mapambano juu ya uingizaji, usambazaji na usafirishaji wa Dawa za Kulevya;
d.
Kuangamiza Dawa za Kulevya
zilizokamatwa;
e.
Kuitisha mikutano ya wadau
waliomo kwenye mapambano ya Dawa za Kulevya;
f.
Kupunguza matatizo ya athari
za utegemezi wa Dawa za Kulevya.
Programu ya Kumi: Utawala na Uendeshaji wa Tume ya Kitaifa ya
Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya.
|
67.0
Mheshimiwa
Spika,
lengo kuu la programu hii ni kuweka mazingira mazuri ya kazi za ofisi. Huduma
zinazotarajiwa ni upatikanaji wa huduma na vitendea kazi, kujenga uwezo wa
wafanyakazi na usimamizi wa matumizi ya fedha pamoja na kukuza uwajibikaji.
Programu ina program ndogo mbili ambazo ni:
i.
Utawala wa Tume ya Kitaifa ya
Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya,
ii.
Uratibu wa Masuala ya Dawa za
Kulevya
Pemba.
68.0
Mheshimiwa
Spika, shughuli
zilizopangwa kutekelezwa katika programu hii ni:-
a)
Kuweka mazingira mazuri ya
kazi na kusimamia utekelezaji wa majukumu ya
kazi;
b)
Kujenga uwezo wa wafanyakazi
katika mapambano ya dawa za kulevya;
c)
Kuwapatia mafunzo ya muda mrefu
na mfupi wafanyakazi wa Tume.
TUME YA UKIMWI:
69.0
Mheshimiwa
Spika, Tume
ya Ukimwi ina jukumu la kuratibu masuala ya UKIMWI hapa Zanzibar, ambapo
imepangiwa kusimamia Programu Kuu mbili kama ifuatavyo:-
Programu ya Kumi na Moja: Uratibu wa Muitiko wa Taifa wa UKIMWI
|
70.0
Mheshimiwa
Spika, Programu
hii ina programu ndogo mbili ambazo ni:
i.
Uratibu wa muitiko wa Taifa wa UKIMWI.
ii. Mawasiliano
na Utetezi wa Masuala ya UKIMWI.
71.0
Mheshimiwa
Spika, shughuli
zilizopangwa kutekelezwa katika programu hii ni:-
a)
Kuandaa Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano na Utetezi na
nyaraka za Mfuko wa UKIMWI;
b)
Kuzisaidia Asasi za Kiraia kuandaa mapendekezo ya mradi;
c)
Kuendelea kutoa elimu juu ya Sheria Nam.18 ya Kukinga
na Kusimamia masuala ya UKIMWI ya mwaka 2013 kwa wadau mbali mbali;
d)
Kutoa mafunzo ya ukondoeshaji wa masuala ya UKIMWI kwa Taasisi
mbali mbali;
e)
Kutoa uelewa wa Mkakati wa Tatu wa Taifa wa UKIMWI na
kuwasilisha matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya UKIMWI wa 2016/17 kwa wadau na
kuwajengea uwezo wa namna ya kuyatumia matokeo hayo katika programu zao;
f)
Kufanya mijadala ya kuibua mila na mitizamo ya jamii
ambavyo ni vikwazo kwa vijana kufikia huduma za kuwakinga na maambukizi ya VVU;
g)
Kuhamasisha utekelezaji wa programu za UKIMWI katika
shemu za kazi Serikalini na sekta binafsi;
h)
Kufanya uhamasishaji na utetezi juu ya hatua za
kudhibiti mazingira na tabia hatarishi katika mamlaka za Mikoa, Wilaya na
Shehia na kupitia Viongozi wa Dini;
i)
Kufanya mikutano ya kuratibu muitiko wa Taifa wa UKIMWI;
j)
Kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji na tathmini wa shughuli
za UKIMWI;
k)
Kutekeleza programu ya makundi maalum, vijana na rika
baleghe juu ya UKIMWI na afya ya uzazi;
l)
Kutoa elimu kwa njia za vielelezo, redio, tv, tovuti na
simu juu ya kupiga vita unyanyapaa wa watu wanaoishi na VVU na kuhamasisha
upimaji wa VVU na matumizi ya huduma za tiba.
Program ya Kumi na Mbili: Utawala na Uendeshaji wa Tume ya UKIMWI
|
72.0
Mheshimiwa
Spika, lengo
kuu la programu hii ni kuweka mazingira mazuri ya kazi za Ofisi. Programu hii
imepangiwa kusimamia programu ndogo mbili ambazo ni:-
i.
Uratibu wa Masuala ya UKIMWI Pemba
ii.
Utawala na uendeshaji Unguja.
73.0
Mheshimiwa
Spika, shughuli
zilizopangwa kutekelezwa katika programu hii kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ni:-
a)
Kufanya uratibu wa muitiko wa UKIMWI Pemba;
b)
Kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa wafanyakazi
ili kuongeza ufanisi na umakini wa kazi;
c)
Kuupitia muongozo wa fedha, kufanya ukaguzi wa kifedha, kusimamia utekelezaji na uwajibikaji
wa kifedha;
d)
Kulipia huduma, kununua vifaa vya ofisi, pamoja na
kufanya matengenezo ya majengo na gari;
e)
Kutekeleza programu ya afya kwa wafanyakazi na familia
zao.
MGAO WA FEDHA
KWA PROGRAMU:
74.0
Mheshimiwa Spika, mgao wa fedha kwa Programu kumi na mbili (12) za
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Taasisi zake ni kama ifuatavyo:-
Programu
ya Kwanza: Uratibu wa Shughuli za Makamu wa Pili
wa Rais. Programu hii imepangiwa kutumia jumla ya Shilingi 1,024,217,282
kwa kazi za kawaida.
Programu
ya Pili: Uratibu wa Shughuli
za Serikali:
Programu hii imepangiwa kutumia jumla ya Shilingi 5,507,508,060 kwa kazi za kawaida
na Shilingi 13,863,777,000
kwa kazi za maendeleo ambapo Shilingi 726,000,000 kwa fedha za
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Shilingi 13,137,777,000 ni
mchango wa Wahisani.
Programu ya Tatu:
Usimamizi wa Shughuli za Upigaji Chapa.
Programu hii imepangiwa kutumia jumla ya Shilingi 2,068,089,200 kwa
matumizi ya kazi za kawaida.
Programu ya Nne: Mipango na Utawala. Programu hii imepangiwa kutumia Shilingi 2,068,774,658 kwa kazi za kawaida na Shilingi 500,000,000 kwa kazi za maendeleo kwa fedha za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Programu ya Tano: Kutunga Sheria, Kupitisha Bajeti na Kusimamia Taasisi za Serikali.
Programu hii imepangiwa kutumia Shilingi 6,595,520,000 kwa
kazi za kawaida.
Programu ya Sita: Uongozi na Utawala wa Baraza la Wawakilishi. Programu hii
imepangiwa kutumia Shilingi 12,066,180,000 kwa
kazi za kawaida.
Programu ya Saba: Uendeshaji na Usimamizi wa Shughuli za Uchaguzi. Programu hii fedha
zake zinatoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali.
Programu ya Nane: Usimamizi wa Kazi za Utawala na Uendeshaji wa Shughuli za Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar. Programu hii imepangiwa kutumia Shilingi 1,695,500,000 kwa kazi za kawaida.
Programu ya Tisa: Udhibiti wa Dawa za Kulevya. Programu hii imepangiwa kutumia Shilingi 151,777,000 kwa kazi za kawaida.
Programu ya Kumi: Utawala wa Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya.
Programu hii imepangiwa kutumia Shilingi 447,123,000 kwa
kazi za kawaida.
Programu ya Kumi na Moja: Kuratibu Muitiko wa Taifa wa UKIMWI. Programu hii
imepangiwa kutumia Shilingi 235,044,000 kwa
kazi za kawaida.
Programu ya Kumi na Mbili: Utawala na Uendeshaji wa Tume ya UKIMWI. Programu
hii imepangiwa kutumia Shilingi 611,756,000 kwa
kazi za kawaida.
75.0
Mheshimiwa Spika, jumla ya makisio kwa Programu zote 12 za Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ni Shilingi
44,769,177,000 ambapo Shilingi 30,405,400,000 kwa kazi za
kawaida na Shilingi 14,363,777,000 kwa kazi za maendeleo (Angalia Kiambatisho Nam. 4 na 5).
UKUSANYAJI
MAPATO:
76.0
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa
fedha 2017/2018, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais imepangiwa kukusanya mapato ya
jumla ya Shilingi 32,521,000 kupitia
kodi ya milango ya maduka na vifaa vya Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya
Kitaifa.
77.0
Mheshimiwa
Spika, baada
ya kueleza hayo, sasa naomba kuchukua fursa hii kumshukuru kwa dhati Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed na Naibu
Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Mihayo Juma Nhunga kwa
juhudi zao kubwa wanazozichukua katika kuendelea kunisaidia kutekeleza majukumu
yangu kwa ufanisi mkubwa. Aidha, nawashukuru pia watendaji na wafanyakazi wote
wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Taasisi zilizo chini ya Ofisi hii
wakiongozwa na Katibu Mkuu Ndugu Joseph Abdallah Meza na Naibu Katibu Mkuu
Ndugu Ahmad Kassim Haji kwa juhudi zao katika kutekeleza majukumu yaliyo mbele
yetu.
78.0
Mheshimiwa
Spika, kwa mara nyengine tena natoa
shukurani zangu za dhati kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, na shukurani
maalumu kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Kusimamia Ofisi za
Viongozi Wakuu wa Kitaifa kwa mashirikiano, ushauri na maelekezo waliyotupa katika kukamilisha bajeti yetu ya mwaka ujao
wa fedha 2017/2018. Aidha, napenda kuwashukuru sana Washirika wa Maendeleo
(Development Patners) na nchi marafiki ambazo zinaendelea kuchangia katika
kufanikisha utekelezaji wa malengo ya Ofisi yangu na ya nchi kwa jumla katika
mwaka wa fedha 2016/2017. Miongoni mwao ni: Benki ya Dunia, Clinton Foundation,
China, FAO, Finland, Norway, India, Japan, Marekani, Mfuko wa Dunia wa
Kupambana na Kifua Kikuu Malaria na UKIMWI (Global Fund), Oman, UNAIDS, USAID,
UNDP, UNICEF, UNFPA, WHO, WFP na WIPO. Vile vile naishukuru sana Ofisi ya
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa
ushirikiano wao mkubwa na Ofisi yangu. Pia nazishukuru Taasisi zisizo za
Kiserikali, Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima kwa kuendelea
kuisaidia Serikali katika kutoa huduma za jamii na kuleta maendeleo katika nchi
yetu.
79.0
Mheshimiwa Spika, nawashukuru
sana wananchi wangu wote wa Jimbo la Mahonda kwa kuendelea kushirikiana nami
katika kutekeleza majukumu yangu kwao nikiwa Mwakilishi wao katika Baraza hili
na katika kutekeleza majukumu yangu ya kitaifa nikiwa Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar. Nawashukuru pia wananchi wote ambao wamefuatilia na kuisikiliza
hotuba yangu hii.
80.0
Mheshimiwa Spika, baada ya
maelezo hayo, sasa naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe jumla ya 44,769,177,000 kwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na
Taasisi zake kwa ajili ya kutekeleza Programu nilizozielezea hapo awali.
Mchanganuo halisi wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:-
i.
Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais Shilingi 22,964,277,000
ii.
Ofisi
ya Baraza la Wawakilishi Shilingi 18,661,700,000
iii.
Tume
ya Uchaguzi ya Zanzibar Shilingi 1,695,500,000
iv.
Tume
ya Kitaifa ya Kuratibu na
Udhibiti wa Dawa
za Kulevya Shilingi 598,900,000
v.
Tume
ya UKIMWI Zanzibar Shilingi 846,800,000
Jumla: Shilingi 44,769,177,000
81.0
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
No comments:
Post a Comment