Habari za Punde

Kanisa la Anglikana Zanzibar Laadhimisha Ibada ya Shukrani.

 Askofu Michael Hafidh wa kanisa la Anglikana Zanzibar (kulia) akitoa baraka wakati akiingia kanisani akifuatana na Maaskofu na Makasisi kuanza Ibada ya shukrani kwa kukamilisha ukarabati wa kanisa hilo jana.


Askofu wa Anglikana Zanzibar, Michael Hafidh (wa tatu kulia) akiwa na Maaskofu wenzake baada ya misa hiyo ya shukrani.
Picha na Martin Kabemba

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewahakikishia viongozi wa dini mbalimbali Zanzibar kuwa ipo tayari kutoa msaada pale itakapohitajika bila ya ubaguzi wowote.


    Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Zanzibar,Mhe. Moudline Castico aliyasema hayo jana mjini Unguja wakati akizungumza na waumini wa kanisa la Anglikana kwenye Ibada maalumu ya shukrani baada ya kukamilika kwa ukarabati mkubwa wa kanisa hilo.


    Alisema waumini wa dini zote wanapaswa kushirikiana kuidumisha amani iliyopo nchini, jambo ambalo ni msingi mkuu wa maendeleo.


    Akizungumza wakati wa kumkaribisha Mhe.Castico ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Ibada hiyo, Askofu wa Anglikana Zanzibar, Michael Hafidh aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wahisani wa ndani na nje ya nchi kwa misaada yao iliyouwezesha ukarabati wa kanisa hilo lililojengwa karne ya 19 kama ishara ya kufungwa kwa biashara ya utumwa Zanzibar.



    Nae Askofu Maimbo Mndolwa kutoka Dayosisi ya Tanga alitoa tamko la pongezi kwaniaba ya Maaskofu na Makasisi waalikwa kutoka baadhi ya mikoa Tanzania Bara, alilipongeza kanisa hilo la Zanzibar kutokana na kuwa chachu ya kuenea kwa makanisa mengine ya Anglikana kote Tanzania.



    Aidha Askofu huyo alitoa rai kwa kanisa la Anglikana Zanzibar kushirikiana kikamilifu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuzitumia rasilimali zilizopo nchini ili kuwaletea maendeleo wananchi.



    Ukarabati wa Kanisa hilo uliodumu kwa zaidi ya miaka 9 umegharimu takriban euro laki 9



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.