STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 06.05.2017
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein anaondoka nchini leo kwenda Jamhuri ya
Djibouti kwa ziara ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Ismail
Omar Guelleh.
Ziara hiyo ya Dk. Shein inatarajiwa
kuanza kesho tarehe 7 na kumaliza tarehe 9 nchini humo ambapo ataanza ziara yake
kwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Djibout Ismail Omar Guelleh.
Aidha, katika ziara yake
hiyo, Dk. Shein atatembelea miradi mbali mbali ya maendeleo nchini humo ambapo
miongoni mwa miradi hiyo atakayoitembelea ni Bandari ya Doraleh, Bandari ya Ziwa Assal, Maeneo Huru ya
Uchumi pamoja na Kampuni ya Simu na Mawasiliano “Djibouti Telecom Haramous”.
Katika
ziara hiyo, Dk. Shein amefuatana na viongozi mbali mbali akiwemo Mke wa Rais wa
Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafiri, Balozi Ali Abeid Karume, Waziri wa Afya
Mahamoud Thabit Kombo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afika
Mashariki Dk. Susan Alphonce Kolimba.
Wengine
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi
Zanzibar (ZIPA) Salum Khamis Nassor, Mshauri wa Rais Masuala ya Ushirikiano wa
Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa pamoja na
watendaji wengine wa Serikali.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa
kurejea nchini Jumaatano Mei 10, 2017.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment