Habari za Punde

Semina juu ya mtangamano wa Afrika Mashariki yafanyika kisiwani Pemba

Katibu Mkuu wizara ya Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Salum Maulid Salum, akizungumza kwenye ufungaji wa semina kwa wajasiriamali, juu ya mtangamano wa Afrika Mashariki, iliofanyika uwanja wa Gombani Chakechake Pemba,  na kutayarishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe: Issa Haji Ussi “Gavu’ akizungumza kwenye ufungaji wa semina ya siku nne, kwa wajasiriamali kisiwani Pemba, juu ya mtangamano wa Afrika Mashariki, iliofanyika uwanja wa Gombani Chakechake.
Mshiriki wa semina Othman Bakar Shehe akitoa shukuran kwa niaba ya wajasiriamali wenzake, baada ya kumaliza semina ya siku nne, ya mtangamano wa Afrika Mashariki, iliofanyika uwanja wa Gombani na kuandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe Issa Haji Ussi “Gavu’ zawadi ya mikoba ya kisasa inayotengenezwa na wajasiriamali, hafla hiyo ilifanyika uwanja wMjasiriamali Kauthar Is-haka akimkabidhi a Gombani, baada ya kumaliza semina ya mtangamano wa Afrika Mashariki, 
WA kwanza kulia, ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe: Issa Haji Ussi “Gavu’ akifuatiwa na Katibu Mkuu wake, Salum Maulid Salum samba na Mwenyekiti wa wajasiriamali kisiwani Pemba, Khamis Suleiman wakisikiliza shukura za wanasemina, iliofanyika uwanja wa michezo Gombani juu ya mtangamano wa Afrika Mashariki.
Wajasiriamali, wafanyabiashara na baadhi ya wakuu wa taasisi za serikali kisiwani Pemba, wakisikiliza hutuba ya Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe: Issa Haji Ussi “Gavu’ wakati akifunga semina juu ya mtangamano wa Afrika Mashariki, iliofanyika uwanja wa Gombani Chakechake.(Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.