Habari za Punde

Wajumbe wa Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB) ziarani Pemba

 WAJUMBE wa Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB)wakikagua kiwanja cha ZRB kilichopo Gombani nje kidogo ya Mji wa Chake Chake, ambachi wanatarajiwa kujengwa Ofisi ya ZRB Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 WAJUMBE wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) wakibadilishana mawazo baada ya kukagua eneo ambalo wanataka kujenga ofisi ya ZRB Kisiwani Pemba huko katika uwanja wa Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
 MSAIDIZI Meneja wa ZRB Kisiwani Pemba, Ali Omar akiwaonesha wajumbe wa Bodi ya ZRB Mipaka ya Kiiwanja cha Ofisi hiyo, kilichopo nje ya uwanja wa Michezo Gombani ambazo wanatarajia kujenga Ofisi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MENEJA wa ZRB Kisiwani Pemba Said Ali Mohamed, akitoa maelezo ya Ofisi ya ZRB mkoani bandarini kwa wajumbe wa Bodi ya ZRB, wakati walipofanya ziara ya siku mbili Kisiwnai Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MWENYEKITI wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB)Saleh Sadik Osman, akizungumza na watendaji wa ZRB baada ya kumaliza kukagua ofisi ya bodi hiyo bandarini Mkoani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MENEJA wa GAPCO Dipoti ya Mafuta Wesha Kisiwani Pemba, Justice Mkubi akizungumza na wajumbe wa bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) walipotembelea GAPCO hiyo kujuwa Uingizaji na utoaji wa mafuta.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MJUMBE Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Mauwa Abeid Daftari, akichangia katika kikao cha pamoja na meneja wa GAPCO Dipoti Wesha, wakati wa ziara ya siku mbili Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 KAMISHNA wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Amour Hamil Bakar, akizungumza katika kikao cha Pamoja na Meneja wa GAPCO Dipoti ya Wesha, wakati wa ziara ya Siku mbili kwa wajumbe wa bodi hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MJUMBE wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Saleh Mbarouk, akizungumza katika kikao cha pamoja na meneja wa GAPCO Dipoti ya Wesha, wakati wa ziara ya siku mbili ya wajumbe hao.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.