Habari za Punde

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Afungua Ijitimai ya Pili Mkoa wa Kaskazini Unguja

Ustadh Abdallah Othman kutoka Madrasa ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam akisoma Quran wakati wa ufunguzi wa Ijitimai inayofanyika katika Kijiji cha Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja na kuwashirikisha Waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka Nchi za Afrika Mashariki na kuhudhuriwa na Manaibu Mufti wa Nchi za Uganda na Malawi.
Mshereheshaji wa hafla hiyo ya Ufunguzi wa Ijitimai Ust Juma Mmanga akitowa maelezo kabla ya ufunguzi wa Ijitimai hiyo, inayofanyika katika Kijiji cha Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Naibu Amiri wa Fisabililay Markasy Amiri Wakati Hassan akitzungumza makusudio ya mkusanyiko huo kwa Waislami kukumbushana mambo ya Ibada ya Dini ya Kiislam na kuwaasa watoo mada kutowa mada kuhusiana na dini tu wasizungumzie mambo ya siasa.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Vuai Mwinyi akizungumza wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Ijitimai inayofanyika katika Kijiji cha Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katibu wa Markassy Fisabililay Sheikh. Mwalimu Hafidh Jabu akitowa nasaha zake kwa Waumini wa Dini ya Kiislam wanaohudhuria Ijitimai ya Siku Tatu inayofanyika katika Kijiji cha Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amiri Mkuu wa Markasy ya Fisabililay Amiri Ali Khamis Mwinyi akizungumza na waumini wa Dini ya Kiislam wakati wa ufunguzi wa Ijitimai inayofanyika katika markasy ya Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmin Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akiwahutubia waumini wa Kiislam wakati akifungua Ijitimai inayofanyika katika kijiji cha kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja. Na kuwataka waislamu kushikamani katika kuuimarisha uislam kupitia katika makutano kama haya ya Ijitimai ili kukumbushana mema na kuwacha mabaya.


Mkalimali wa lugha za alama akiashiria kwa vitendo wakati wa hutubi ikitolewa na mgeni rasmin kwa wananchi wenye ulemavu wa kutosikia wakati wa hafla hiyo ya Ijitimai.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.