Habari za Punde

Upepo Uliovuma kwa Muda Mchache Katika Mitaa ya Nyarugusu Zanzibar umeharibu Zaidi ya Nyumba 80.

Mmoja ya Nyumba katika eneo la mitaa ya nyarugusi ikiwa imeezuliwa paa lote na upepo wa ajabu uliotokea kwa dakika chache na kuleta maafa karibu nyumba 80 zimekumbwa na upope huo kwa kubomoka kwa ukuta wa nyumba hizo.
Wananchi wa maeneo ya nyarugusu jimbo la Kijitoupole Zanzibar wakikusanya mabati ya nyumba zao yalioezuliwa kwa upepo huo.
Moja ya nyumba hii ikiwa ni mojawapo ilioezuliwa na upepo huo. 
Naibu Waziri wa Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mihayo Juma N'hunga, akizungumza na Maofisa wa Idara ya Maafa Zanzibar kuhusiana na zoezi la kufanya tathimini ya Nyumba zilizoharibika kwa upepo huo wa muda mfupi na kuleta athari kubwa. kwa Wananchi wa maeneo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Kijitoupele Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha akitembelea maeneo ya Wananchi wa Jimbo lake kuwafariji kwa janga la kupata maafa ya upepo wa kimbunga cha muda mfupi na kuleta madhara makubwa kwa wananchi wake.
Wananchi wa maeneo ya Nyarugusu wakiwa nje ya nyumba zao kuangalia baadhi ya nyumba zilizopata majanga hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akitembelea maeneo yaliopata maafa ya upepo katika maeneo ya Nyarugushu Jimbo la Kijitoupele Zanzibar na kuwafariji kwa janga hilo.
Baadhi ya mabaki ya majengo ya nyumba za nyarugusu zilizoharibika kwa upepo mkali uliovuma kwa muda mchache na kuleta maafa kwa wananchi wa eneo hilo.
Wanafamilia wakiwa katika eneo la nyumba yao inayomilikiwa na Mzee Ali Suleiman ni mmoja ya nyumba zilizopata majanga hayo kwa kuanguka kwa kuta zake na kuezuliwa kwa paa la nyumba hiyo.
Mwananchi akimfariji Mzee Ali Suleiman kwa kuangukiwa kwa nyumba yake kutokana na upepo huo unaozaniwa ni wa kimbunga na kuleta maafa kwa wakaazi wa maeneo hayo ya nyarugusu.
Wananchi wakiwa katika maeneo ya nyumba zilizotokea maafa ya upepo uliovuma kwa muda mchache na luleta madhara kwa baadhi ya nyumba katika eneo hilo.






No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.