Habari za Punde

Jang'ombe Boys yabanwa na watoto wa mjini yatoka sare 0-0

Kikosi cha timu ya Kombaini ya Wilaya ya mjini
Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Timu ya Soka ya Kombain ya Wilaya ya Mjini na Jang'ombe Boys zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0 katika mchezo maalum wa kirafiki uliosukumwa jana Jumatano saa 3 za usiku katika uwanja wa Amaan.
Mjini watacheza mchezo mwengine wa kirafiki leo Alhamis kuanzia saa 10:15 za jioni dhidi ya timu ya Gulioni ambayo inashiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini.

Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu moja kwa majukwaa ya kawaida na V.I.P ni shilingi Elfu mbili.Kombain ya Mjini wanajiandaa na Mashindano ya Rolling Stone yanayotarajiwa kuanza July 9 hadi July 19, 2017 huko Mburu Manyara wakati Jang'ombe boys wanajiandaa na kuendelea kucheza hatua ya 8 bora ligi kuu soka ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.