Na. Haji Nassor. Pemba.
WAUMINI wa dini ya kiislamu duniani kote, wanaendelea na mfungo wa mwezi
mtukufu wa ramadhan, ikiwa ni nguzo ya nne kati ya zile tano za kiislamu.
Mwezi huu mtukufu wa ramadhani, huja mara moja kila mwaka,
nao kama ilivyo miezi mengine, huwa na makumi matatu, ingawa ya mwezi huu,
hutaja kuwa ni ya thamani zaidi.
Maana maandiko yasiokuwa na shaka, yanaeleza wazi wazi
kuwa, siku kumi za kwanza huwa ndio za rehma, wakati za pili huwa ndio za
maghufira na mwisho ni touba, (maarufu kama kuachiwa huru na moto).
Hakuna shaka kuwa, ubora wa mwezi huu au tofauti kubwa na
miezi mengine ni kwamba, huu ndio uliotajwa kushushwa maadiko matakatifu ya
ku-ran.
Kumbe, mwezi huu ni mtakatifu na wenye kheir na neema
kadhaa, hadi masheikh na wanazuoni kutuelezwa kuwa, hata ukifanya jambo jema,
basi malipo yake ni mara dufu.
Kama hivyo ndivyo, waislamu wenzetu hasa wanaotumia miuriji
ya uvutaji wa sigara, hawajiskii ovyo na wapotevu kuendelea kurusha moshi ndani
ya mwezi huu mtakatifu?
Tena mchana mzima, kwa maana zaidi ya saa 12 inawezekana
wapo wanaojizuia na uvutaji wa sigara, kwa sababu za kuwa na swaumu, ingawa baada
ya futari huendelea na kazi yao.
Huu muda wa kujiweka mchana pasi na kuvuta sigara kwa saa
kadhaa, kwanini isiwe sababu kwa wavutaji kuacha moja kwa moja, hasa kwa vile
faida yake haionekani.
Chakupendeza zaidi kama sio cha kufurahisha, hakuna dini
hata moja iliorasmi, ambayo inasisitiza na kuhalalisha uvutaji wa sigara, maana
hasa sigara, imebeba magonjwa zaidia 300.
“Utampendeza Muumba wako, wapendwa acheni tujisafishe wenyewe kila unajisi wa mwili.” ( wakorintho 2
7:1) “mtoe miili yenu ikiwa takatifu, yenye kukubalika kwa Mungu.”waroma 12:1.
Ndivyo ukiristo ulivyonadi, juu matumizi ya sigara, lakini hata dini ya
kiislamu nayo, umeshatamka kuwa “ wanakuuliza wamehalalishiwa nini, sema
mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri (Al-Maaidah, 5:4)
Mwezi huu
mtukufu wa ramadhani, ndio adhimu na adimu kwa mwenye kutaka kuacha matumizi ya
moshi wa sigara, na zipo njia na mikakati kadhaa, ambayo kama ukiyafuata basi
waweza kufanikiwa.
NIA: kila jambo kwanza linahitaji nia ya kweli, maana pasi
na kuweka na kuufunga moyo wako na nia wala mvutaji hatoweza, kufikia lengo lake.
Kupanga muda: kwa mfano kwa mwezi huu
mtukufu wa ramadhani, ndio mahasusi na adhimu, maana wavutaji waliowengi na
hasa waislamu, ambao wameshaambiwa kuwa, wanapata madhara, basi ni wakati ndio.
Mwezi huu
mtukufu wa ramadhani, huja mara moja kwa mwaka, na siku zake hazizidi 30, sasa
lazima wanaotaka kuacha moja kwa moja, wajipunguzie dozi, kwa mfano wanaovuta
sigara 12 kwa siku, waanze kupunga mmoja moja.
Au kama
wanakawaida ya kuvuta sigara miongo minne kwa siku, sasa wanze kujivuta kwenye mitatu
na kuelekea miwili, ili ubakie mmoja na kisha kuacha kabisa.
Ingawa, wapo
wataalamu na watafiti, wanapinga suala la kujipunguzia idadi ya sigara kwa
siku, wakisema inaweza kupandisha nikotini juu, na wanashauari baada ya
kujipangia ikifika tarehe ni kuacha moja kwa moja.
Kuimarisha azimio la kucha: kwa mwenye
kuacha sigara hasa ndani ya mwezi huu mtukufu wa ramadhani, ni rahisi kama
ataendelea kuimarisha azimio lake, ikiwa ni pamoja na kumuomba Muungu hasa
nyakati za usiku.
Kukaa na waliofaulu: kwa muachaji
wa sigara inapendeza azimio na kusudio lake na kuacha kutumia sigara, basi
kukaa na wale waliofanikiwa kucha, maana ndio ambao wameanza na kufanikiwa.
Si vyema
kiushauri kwa mwenye kuacha sigara, kubakia na rafiki wa kweli anetumia sigara,
na anapaswa sasa abadili marafiki na kuachana na marafiki watumiaji.
Kujiandaa na madhara mengine: Wataalamu
wanakubali kabisa kuwa asilimi 90 ya wale wanaocha sigara, hupata dalili za ajabu,
mfano hamu ya kutumia nikotini.
Aidha
wajielewa kuwa wanaoacha sigara, pia wanaweza kukumbwa na dalili za kuchefua
chefua moyo, kujiskia mgonujwa, kichwa kuuma au hata kutokwa na subra.
Dalili hizi
hutajwa kujitokeza kutokana na mwili, kukosa nikotini iliokuwa ya kawaida
mwilini kwa mvutaji wa sigara, ambapo hujitokeza ndani ya saa 12 hadi saa 24,
baada ya kucha, ambpo ni ndani ya wiki mbili hadi sita.
Usikate tamaa: Inawezekana ndani ya
mwezi huu mtukufu wa ramadhani, mvutaji akashindwa kuacha kwa sababu moja ama
nyengine, basi sio vyema kukata tamaa.
Wapo wanaokata
tamaa mara moja, hasa wanaposhindwa kwa mara ya kwanza, hali hiyo haishuriwi na
inatakiwa kuendelea kung’ang’ania kuacha.
Kwa mwezi huu
pekee, ndio rahisi kwa wavitaji wa sigara au watumiaji wengine wa vilevi,
kuacha kutokana na waliowengi mchana mzima kutotumoa viburudishaji hivyo kwao.
Maana Khamis
Haji Makame wa Wawi Chakechake, yeye sasa anatimiza miaka 12 tokea alipoacha
sigara, ingawa alishautumia miaka kama hiyo.
Yeye anasema
alishauriwa kuacha sigara mwezi kama huu mwaka 2005, na alikaribia kushindwa
hasa kwa vile alipata magonjwa kadhaa, ikiwa ni pamoja na kichwa kuuma sana.
“Mimi nia ya
kuacha sigara ndio ilionifanya, leo nisherehekee miaka 12 ya kuihasimu sigara,
sasa kila aliweke nia ya kweli ya kucha basi atafanikiwa”,alishauri.
Hassina Haji
Mohamed wa Kengeja, anasema yeye alitumia nguvu kiasia fulani mwezi kama huu,
mwaka juzi kwa kuzitupa sigara za mumewake, na sasa anatimiza miaka miwili bila
ya kutumia.
“Tuligombana
sana na mume wangu juu ya matumizi ya sigara, lakini kwa vile alinikubalia,
sasa ameshaacha kwa msaada wangu na yeye kutaka”,anasema.
Mume huyo
ambae kwa sasa yuko Unguja kwenye shughuli zake za biashara ya ndizi, Kombo
Omar Kombo akizungumza na ukurasa huu anasema nia ya kuacha matumizi ya sigara,
alishaijaribu mara nne bila ya mafanikio.
“Mimi mke
wangu ndie mwalimu wangu wa mimi kuacha sigara, maana ndani ya ramadhani ya
mwaka juzi, namuuliza sigara zanguza ziko wapo, akanijibu amezitupa tena kwa
ukali, lakini leo nimeashanikiwa kuihasimu sigara”,anaeleza.
Hali
ya kiafya ya watu ambao wanavuta sigara inazidi kuwa mbaya baada ya Shirika la
Afya Duniani (WHO), kutoa ripoti ambayo inaonyesha, hivi karibuni kutakuwa na
watu milioni nane (8), ambao watakuwa wanakufa kila mwaka kwa sababu ya uvutaji
sigara.
Vifo hivyo vimeripotiwa kuwa, vitakuwa vikitokana na
magonjwa ambayo watumiaji wa sigara wanakuwa nayo kutokana na matumizi ya
sigara, kuonekana kuongezeka ambapo kwasasa inakadiriwa kuwa zaidi ya dola trilioni
moja, kutumika kila mwaka kwa ajili ya kununua sigara.
“Vifo vya watu ambao wanatumia
bidhaa ambazo zinatokana na tumbaku itapanda kutoka watu milioni sita, hadi
milioni nane ifikapo mwaka 2030, nchi ambazo zitaathirika zaidi ni zenye uchumi
mdogo na wa kati,” ilisema ripoti hiyo.
Wataalamu wa afya wanasema kuwa bidhaa za tumbaku ni moja ya
vitu hatari kwa afya, na ambavyo vimekuwa vikisababisha vifo vya watu wengi,
lakini bado idadi ya watumiaji wake inazidi kuongezeka kwa kasi katika maeneo
mbalimbali duniani.
Kuvuta moshi wa sigara inayotumiwa na mtu mwingine
kumechangia pakubwa, katika mjadala juu ya madhara na udhibiti wa bidhaa za
tumbaku.
Tangu mapema miaka ya 1970, sekta ya tumbaku imekuwa na
wasiwasi kuhusu kuvuta moshi wa sigara, inayotumiwa na mtu mwingine kama tishio
kubwa kwa maslahi ya biashara yake.
Aidha taarifa hiyo, ikaenda mbali na kwamba, sigara moja inakemikali
zaidi ya 480,069 kati ya hizo zinasababisha kansa ingawa pia asilimia 69 ya
wavuta sigara, wanatamani kuacha kabisa, ingawa wameshindwa.Taarifa inaeleza kuwa, sigara billion 15 huvutwa kila siku dunia kote ikiwemo hapa Zanzibar, ingawa bwana Adolf Hitler wa Marekeani ndio mtu wa kwanza, kuanzisha kampeni ka kuzuia uvutaji sigara katika historia ya hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment