Habari za Punde

Mjumbe wa Baraza la Maulamaa Zanzibar ahimiza taaluma ya ndoa kunusuru wimbi la kuvunjika kwa ndoa

Na Salmin Juma, Pemba

Mjumbe wa Baraza la Maulamaa Zanzibar Mkoa wa Kusini Pemba Sheikh Ali Abdala Awess amewataka Masheikh na Wazazi  kuelimisha Vijana  suala la Ndoa ili kunusuru Wimbi la kuvunjika Ndoa nyingi  mapema.

Amesema wakati huu ndoa nyingi za vijana zinavunjika mapema na kusababisha idadi kubwa ya Wajane na Watoto wasio na malezi bora kutokana na kukosekana kwa Taaluma ya Ndoa kabla .

Sheikh Awess  ameyasema hayo jana Kwenyeskiti wa Ijumaa  Mtambile alipokua akizungumza na Waislam mara baada  ya Swala  ya  Ijumaa.

Amesema Taaluma  ya Mapema  kwa Wanandoa  ni njia pekee itakayowafanya  waishi ndani ya Ndoa yao kwa Mafanikio.

Wakati huo huo Mjumbe  huyo  wa  Baraza  la Maulamaa ameelezea  kusikitishwa  na Tabia   iliyojitokeza  kwa baadhi  ya Misikiti kuisali Sala  ya Ijumaa nje ya wakati  wake.

Amesema imejitokeza baadhi ya Miskiti  inasali  Sala  hiyo  nyakati  za  saa tano  kitendo ambacho hakifai na kiachwe ili kulinda nyakati  za sala

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.