Habari za Punde

Ninja wa Yanga Apewa Vifaa na Raza Lee Kwa Ajili ya Kuwaaga Mashabiki Wake Siku ya Ijumaa.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, 
Mlinzi mpya wa Yanga Abdallah Haji Shaibu "Ninja" amezawadiwa vifaa vya soka na Mohammed Ibrahim “Raza Lee” ambae ni mdau wake mkubwa.

Vifaa hivyo vikiwemo Viatu vya kucheza soka pamoja na jezi full ambavyo amepewa mchana wa leo katika Duka la Raza Lee ambapo linauza Vifaa vya Michezo liliopo Darajani Mjini Unguja.

Akizungumza na Mtandao huu Raza Lee baada ya kumzawadia Ninja vifaa hivyo, amesema amefurahi sana kumuona Ninja amesajiliwa Yanga huku akisema kuwa ndie mchezaji wake namba moja anaemkubali katika soka la Tanzania.

“Niliposikia Ninja kasajiliwa Yanga nilifurahi sana nikasema sasa mchezaji wangu anazidi kufanikiwa kisoka, mimi Ninja nampenda sana na ndio mana hapa Dukani tangu hajasajiliwa Yanga huwa nampa vifaa kama kumpa hamasa, sasa na leo nimempa vifaa vya kuvaa katika mchezo wake wa mwisho Ijumaa wa kuagwa Taifa ya Jang’ombe”. Alisema Raza Lee.

Jumatano iliyopita Ninja amesajiliwa Yanga akitokea Taifa ya Jang’ombe ya Zanzibar ambapo amefunga mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo na siku ya Ijumaa ya June 23 Saa 3:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan mchezaji huyo atawaaga Mashabiki wake katika mchezo maalum kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi Mlandege SC.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.