Habari za Punde

SEIFU TIOTE AWAOMBA WADAU WA SOKA KUISADIA KOMBAIN YA MJINI

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Kiungo mshambuliaji wa Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini Seifu Said Seifu (Tiote) amewaomba wadau wa soka Visiwani Zanzibar kuichangia timu yao ili wafanikishe safari yao ya kwenda Mburu Mkoani Manyara kushiriki Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone.

Tiote ameyasema hayo wakati anazungumza na Mtandao asubuhi ya leo huku akisema mazoezi yanaendelea vizuri na wao wachezaji wana hamasa kubwa sana ya kutetea taji lao lakini wadau wa soka waisaidie timu yao ili ifanye vizuri kama msimu ulopita.

“Mazoezi tunaendelea vizuri tuna hamasa kubwa sana mana tunakuja kwa wakati na tunapokea vizuri mafunzo ya walimu wetu lakini nawaomba wadau wa soka Zanzibar watuunge mkono kwa kutusaidia chochote ili tuweze kutetea taji mana hii timu inawakilisha Zanzibar nzima sasa”. Alisema Tiote.

Mashindano ya Rolling Stone mwaka huu yatafanyika Mikoa miwili tofauti Arusha na Manyara kuanzia July 9 hadi July 19, 2017 ambapo kundi la Mjini Unguja ambao ndio mabingwa watetezi limepangwa kuchezwa Manyara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.