Habari za Punde

Ufunguzi wa Mafunzo ya Siasa na Uongozi ya Wanawake wa UWT.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Dkt. Abdulla Juma Saadalla “Mabodi” akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum  Wanawake (CCM)  (MNEC) Bi. Khadija Hassan Aboud pamoja  na  viongozi  mbali mbali wa UWT Mkoa wa Mjini  Zanzibar mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkoa wa Mjini CCM uliopo Amani Unguja.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Dkt. Abdulla Juma Saadalla “Mabodi” akiwahutubia  mamia  ya wanachama na viongozi  wa UWT Mkoa wa Mjini  Unguja, mara baada ya kufungua mafunzo ya Wanawake na Uongozi katika siasa huko  Ukumbi wa Mikutano wa Mkoa wa Mjini CCM uliopo Amani Unguja.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mjini, Bi. Waridi Juma Othman akizungumza  na viongozi na wanachama  hao kabla ya kumkaribisha mgeni  rasmi afungue  mafunzo hayo  Ukumbi wa Mikutan    o wa Mkoa wa Mjini CCM uliopo Amani Unguja
Mbunge wa Viti Maalum  Wanawake (CCM)  (MNEC) Bi. Khadija Hassan Aboud akitoa maneno ya shukrani kwa mgeni rasmi  Dkt. Abdulla Juma Saadalla “ Mabodi”  kabla ya kuanza mafunzo hayo.
Katibu wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi  Bi. Waride  Bakar  Jabu  akiwapungia na kuwasalimia  washiriki wa mafunzo hayo  ambao ni viongozi na wanachama wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja.
Mkufunzi  wa Mafunzo  hayo  Bi. Emiley Nelson Fwambo  akizungumza na washiriki wa mafunzo  ya Wanawake  na Uongozi  katika siasa.
Baadhi ya Viongozi na wanachama wa UWT walioudhuria katika mafunzo hayo wakifuatilia kwa umakini nasaha za mgeni rasmi  Dkt. Abdulla Juma Saadalla “Mabodi”  wakati  akizungumza mara baada ya kufungua  mafunzo hayo.
(Picha na Afisi Kuu Zanzibar.).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.