Habari za Punde

Semina kwa Masheha Uwasilishaji wa Rasimu ya Sheria za Usajili wa Nyaraka

Mwenyekiti Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, Jaji Mshibe Ali Bakar, akizungumza kwenye mkutano wa kuwasilisha rasimu za sheria za usajili wa nyaraka, uharibifu wa mazao na urithi wa ardhi endelevu, kwa masheha wa Mkoa wa kaskazini Pemba, uliofanyika ofisi ya Mkuu wa mkoa huo
Mwanasheria kutoka Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Mwita Khamis Haji, akiwasilisha rasimu za sheria za usajili wa nyaraka na urithi endelevu wa ardhi, mbele ya masheha wa Mkoa wa kaskazini Pemba, wakati tume hiyo chini ya Mwenyekiti wake Jaji Mshibe Ali Bakari, ilipokutana nao ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo mjini Wete.
Masheha wa shehia za Wete na Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, wakijadili rasimu za sheria za uharibifu wa mazao, usajili wa nyaraka na urithi wa ardhi endelevu, wakati Tume ya kurekebisha sheria, ilipokutananao kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, kuzijadili sheria hizo.(Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.