Habari za Punde

Balozi Seif akagua miradi mbali mbali ya kimaendeleo katika Wilaya ya Magharibi

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifanya mzaha na Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Fuoni  Jimbo la Dimani baada ya kulikagua Jengo jipya la Skuli hiyo litakalosaidia kupunguza idadi kubwa ya Wanafunzi  madarasani.

 Balozi Seif na Baadhi ya Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Serikali wakikagua shughuli za uwezekaji wa Jengo jipya la Skuli ya Msingi Fuoni linalojengwa kwa nguvu za Wananchi ambapo aliahidi kukamilisha ujenzi wake.

  Balozi Seif Kati kati akiwa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud Kushoto yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed wakikagua ujenzi wa Nyumba za Makaazi katika Mradi wa Bakhresa Group Fumba.

 Balozi Seif akibadilishana mawazo na Uongozi wa Timu ya CPS Live Bwana Johan Vanden Abeele na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bibi Katrin Dietzold wanaoendesha Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makaazi katika  ukanda wa Maeneo huru ya Uwekezaji Fumba Wilaya ya Magharibi “B”.

 Pango la Maji safi na salama linalotoa Huduma za Maji na salama na kusambazwa katika Vijiji vilivyomo ndani ya Jimbo la Dimani.

 Mhandisi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar {ZAWA} Nd. Hussein Hassan Njuma  wa kwanza kutoka kulia akimuelezea Balozi Seif   aliyepo Kulia yake tatizo linalolikumba pango hilo la kupunguza kiwango cha idadi ya Lita zinazosambazwa kwa Wananchi kutokana na maji yake kuchanganyika na Chumvi baadhi ya wakati. 

Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Ardhi, Maji Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud.

 Balozi Seif na Ujumbe wake akimaliza kulikagua Jengo Jipya la Soko la Samaki  lililojengwa kwa nguvu za Wauvi  wenyewe wa Pwani ya Kichangani.

 Haiba nzuri inayoonekana ya Jengo Jipya la Skuli ya Bwefum Jimboni Dimani linalojengwa na Muwekezaji Mzalendo ambalo kukamilika kwake litatoa huduma za kitaaluma kwa Wanafunzi wa Wilaya Nzima ya Magharibi “B”.

 Meneja Mkuu wa Kiwanda cha uzalishaji wa maziwa Maeneo huru ya Uwekezaji Fumba Bwana  Adson Fagundes Kulia akimtembeza Balozi Seif na Ujumbe wake ndani ya Kiwanda hicho kujionea uzalishaji wa Bidhaa hiyo muhimu kwa afya za Wanaadamu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Viongozi wa Shehia zilizomo ndni ya Jimbo la Dimani katika Mkutano wake wa majumuisho ya ziara yake Jimboni humo hapo Skuli ya Kombeni.

Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.