Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya JKU na Taifa ya Jangombe Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya JKU Imeshinda 2-0.

Kipa wa Timu ya Taifa ya Jangombe akiruka bila mafanikio kuokoa mpira huo ulikwenda hadi golini kwa kuandika bao la kwanza kwa timu ya JKU wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar hatua za nane Bora uliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda mchezo huo kwa mabao 2-0 na kuwa kinara wa Ligi Hiyo kwa kuongoza katika raundi ya nane ya ligi hiyo inayotegemewa kuendelea kesho katika uwanja wa Amaan na Gombani Kisiwani Pemba. 
Mashabiki wa mchezo wa mpira Zanzibar wakifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora kati ya JKU na Taifa ya Jangombe uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Wachezaji wa Timu ya JKU wakishangilia bao lao la pili na la ushindi lililofungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Janja kwa kuunganisha krosi.

Mshambuliaji wa Timu ya JKU Janja akifurahia bao lake la ushindi kwa Timu yake ya JKU, katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.