Wananchi wakishiriki katika mchezo wa ngombe wakati wa Bonaza la Tamasha la Weekend Pemba lililofanyika kwa michezo mbalimbali kisiwani humo. Na kurushwa moja kwa moja na Kituo cha TV cha Azam. Moja
kati ya wachezaji wa mchezo wa Ng’ombe akikosea hatua ya kupiga ngea na
kujikuta akigaragazwa na Ng’ombe mwenye hasira
Baadhi
ya Wananchi Kisiwani Pemba wakifuatilia mchezo wa resi za ngalawa wakiwa katika ufukwe wa pwani ya vumawimbi kujionea burudani mbali
mbali
Mshindi wa kwanza wa mchezo wa mbio za baskeli wakati wa Tamasha hilo la Bonaza Kisiwani Pemba Ndg .Othman
Said Khamis Mshindi wa kwanza wa mchezo wa resi za baiskeli aliejinyakulia Tsh
500,000/=
Viongozi waalikwa waunga mkono juhudi za Rafiki Network.
Washindi na washiriki wa michezo mbali mbali wazawadiwa.
AZAM TV washangwazwa na ukubwa wa matukio.
Na.Ali Othman Ali
Tamasha kubwa la kimichezo Kisiwani Pemba lijulikanalo kwa jina la Pemba weekend Bonanza limefikia kilele chake leo katika Fukwe za
vuma wimbi ambako washindi na
washiriki wa michezo mbali mbali wame kabidhiwa
zawadi.
Akikabidhi zawadi zilizoandaliwa na Kampuni ya
Rafiki Network kwa washindi 30 wa mchezo wa resi za baiskeli ambao waliingia
hatua ya fainali na kupambana kishujaa
kutafuta mshindi wa kwanza, wapili na
watatu ambao waliahidiwa kuzawadiwa 500000/=, 300000/= na 200000/=
kwa
mpangilio, Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mheshimiwa Rashid Ali
Juma ameahidi kwamba mbali na zawadi hizo Wizara yake itawapatia fedha taslim Tsh 50000/= washiriki wengine 27.
Aidha Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh.Mmanga Mjengo Mjawiri ametoa fedha taslim
Tsh 20000/= kwa waogeleaji wote walioshiriki mashindano ya kuogelea
mara
baada ya kukabidhi Ts 300000/= kwa mshindi wa kwanza 200000/= kwa mshindi wa
ili na 100000/= kwa mshindi wa tatu kutoka kwa kamuni ya Rafiki Network.
Mchuano mkali wa resi za Ngalawa ulichomoza katika usawa wa bahari ya vumawimbi kutokea bandari ya Tumbe na kusababisha taharuki
na hamu yakutaka kujua nahodha gani ataibuka mshindi wa michuano hiyo ya
kihistoria abapo Ngalawa ijulikanayo kwa jina “Tutaonana juu” ikiongozwa na
nahodha Hassan Abdallah kutoka makangale iliibuka mshindi nakujinyakulia fedha
Taslim Tsh 300000/=.
Kwaunde mwengine Meneja wa Ufundi na Uzalishaji wa
AZAM TV Nd. Said Meb amesema hakutegemea kwamba tukio la Pemba weekend Bonanza
lingekua na ukubwa alioushuhudia nakwamba amesikitishwa na maandalizi yake
akidai kwamba hayakuweza kukidhi ukubwa wa tukio hilo.
“Kabla nilijua ni matukio machache na madogo lakini
hali imekua tofauti kwani ni shughuli kubwa ambayo ingehitaji tuchukue zana na
vifaa zaidi ya tulivyokuja navyo” amesema
bwana Meb
Tamasha hili lilizinduliwa rasmi siku ya Ijumaa ya
28 Julai katika viwanja vya skuli ya Chwale
Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini pemba ambapo mamia ya mashabiki
waliohudhuria walishuhudia wataalamu wakionesha umahiri wa kupiga ngea.
Hili nitamasha la kwanza kufanyika likiandaliwa na
Kampuni ya Rafiki Network na linatarajiwa kuwa endelevu kwa kufanyika kila
mwishoni mwa wiki ya mwisho ya mwezi Julai kila mwaka.
No comments:
Post a Comment