Habari za Punde

FC Muembe Beni waanza vyema kutetea taji lao central league, Real Kids hoi kwa Schalke 04

Kikosi cha Timu ya Muembe Beni


Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mabingwa watetezi wa ligi za madaraja ya Vijana ndani ya Wilaya ya Mjini kwa upande wa daraja la Central timu ya FC Muembe beni imeanza vyema kampeni zake za kutetea taji lao baada ya kuifunga King Boys mabao 2-0 kwenye mchezo wa 4 bora uliopigwa leo Jumapili July 9, 2017 kwenye dimba la Amaan saa 5 za asubuhi.

Mabao ya Muembe beni yamefungwa na Mselem Ali dakika 15 na Othman Arafat dakika ya 89.

Mchezo mwengine umepigwa majira ya saa 7 za mchana ambapo Real Kids watoto wa Kikwajuni wakafundishwa soka na watoto wa Muembe Makumbi ambao ni Schalke 04 baada ya kufungwa mabao 2-1.

Mabao ya Schalke 04 yamefungwa na Iliyasa Suleiman dakika 6 na 18 wakati bao pekee la Real Kids limefungwa na Abdul halim Mohd dakika ya 39.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.