Habari za Punde

Kombaini ya Wilaya ya Mjini yaanza vyema mashindano ya Rolling Stone yawafunga wenyeji 4-0

 Kikosi cha timu ya Mbulu
Kikosi cha Kombaini ya Wilaya ya mjini

Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone timu ya Kombain ya Mjini Unguja imeanza vyema kutetea taji lao jioni ya leo baada ya kuwafumua wenyeji wao timu ya Mbulu All Stars mabao 4-0 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Julius Nyerere huko Mbulu Mkoani Manyara.

Mabao ya Mjini yamefungwa na Mohd Vuai “Prince”, Seif Said “Tiote”, Abdul hamid Juma (Samatta) na Fahmi Salum (Migwel).

Mjini watashuka tena Dimbani siku ya Jumanne ya July 11, 2017 kucheza na Kenya saa 8:00 za mchana katika uwanja wa Julius Nyerere huko Mbulu Mkoani Manyara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.