Habari za Punde

Zoezi la uhamisho na usajili kuanza rasmi July 17

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Chama cha Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” kimetangaza rasmi tarehe ya kuanza zoezi la uhamisho na usajili kwa msimu wa mwaka 2017-2018 ambao unatarajiwa kuanza July 17, 2017 na kumaliza Agost 17, 2017.

Katibu Mkuu wa ZFA Mohd Ali Hilaly“Tedy” amevitaka vilabu kufata tarehe iliyowekwa ili kurahisisha zoezi hilo.

“Baada ya kupata vilabu 12 vya ligi 1 na 16 vya  ligi 2 sasa tunatangaza Zoezi la uhamisho na usajili kuanza July 17 na kumalizika Agost 17, hivyo naviomba vilabu kufuata taratibu zilizowekwa ili kurahisisha zoezi hili”. Alisema Tedy.

Jana ZFA imepata rasmi timu 12 zitakazoshiriki ligi kuu soka ya kwa msimu wa mwaka 2017-2018 ambapo wameamua timu zilizomaliza nafasi ya 1-6 kwa kila kanda, yani Unguja na Pemba ndizo zitakazocheza ligi kuu wakati huo huo Bingwa atapata nafasi ya kuwakilisha Zanzibar katika Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika.

Timu 16 kati ya 28 zilizosalia ambazo hazijashuka daraja zitacheza ligi two ambapo Bingwa wa ligi hiyo atapata nafasi ya kuwakilisha Zanzibar kwenye kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Timu hizo 12 zilizofanikiwa kucheza ligi kuu msimu mpya wa mwaka 2017-2018 ni JKU, Jang’ombe Boys, Zimamoto, Taifa ya Jang’ombe, Polisi, KMKM kwa upande wa Unguja na Pemba ni Jamhuri, Kizimbani, Mwenge, Okapi, Chipukizi na New Stars.

Kwa upande wa timu 16 zitakazocheza ligi 2 msimu mpya wa mwaka 2017-2018 kati ya hizo 8 za Unguja na 8 za Pemba ambapo za Unguja ni Mafunzo, KVZ, Black Sailors, Chuoni, Kilimani City, Kipanga, Miembeni City na Charawe wakati za Pemba ni Dogomoro, Wawi Star, Shaba, Young Islander, FSC, Hardrock, Chuo Basra na Opek.

Timu 4 za mwisho za ligi 1 zitashuka darajan la ligi 2, na timu 4 za juu za ligi 2 zitapanda daraja la ligi 1.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.