Habari za Punde

Timu ya Taifa ya Jangombe Itafufua Matumaini ya Kupanda Ndege Kwa Kuwakilisha Zanzibar ?, Leo Usiku Inakipiga na Kizimbani Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Taifa ya Jang’ombe “Wakombozi wa Ngambo” kesho Jumapili July 9, 2017 watashuka dimbani kucheza na timu ya Kizimbani kwenye mchezo wa mzunguko wa nne hatua ya 8 bora Ligi kuu soka ya Zanzibar mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1:00 za usiku katika uwanja wa Gombani.

Mchezo mwengine kesho utasukumwa katika uwanja wa Gombani majira ya saa 10:00 za jioni kati ya Mwenge na Jang’ombe Boys.

Mpaka ligi hiyo inakwenda mapumziko kupisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kila timu imecheza michezo mitatu ambapo  Jamhuri ndie kinara akiwa na alama 9 akipata ushindi michezo yote kwa asilimia 100, nafasi ya 2 inakamatwa na JKU yenye alama 6 huku Zimamoto ikiwepo nafasi ya 3 kwa alama 5 wakati Jang’ombe boys wapo nafasi ya 4 kwa points zao 4, wakati huo huo Okapi ikishika nafasi ya 5 na alama zao 4 ambapo Kizimbani wapo nafasi ya 6 kwa alama 3 huku Mwenge akiwa nafasi ya 7 kwa point yake 1 sawa sawa na Taifa ya Jang’ombe iliyopo nafasi ya 8 kwa alama yao 1.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.