Na Bi Hekima
Hizi kavu kavu zinadorora si
kwa sababu hakuna ya kuyaandikia au kuyasemea. Yapo mengi. Lakini hakika huwa
nazidiwa na kiwango cha ujutar, ulimbukeni, ukavu, ukaidi, usugu, utovu wa
adabu ninao ushuhudia kila siku nasawijika na kuishiwa nguvu...inataka stamina
kweli si tu kuyahimili lakini pia kuyakabili yote haya....
Nataka kurudia suala
nililoliandikia mara ya mwisho kwani ni sugu na linatuumiza kwa namna tofauti.
Katika Ramadhan za mwisho
nlijaaliwa kusali taraweh moja Msikiti wa Mwembe Shauri.
Tulipoendelea na sala
nilibaini kuwa sala nilojumuika kuisali si tena taraweh bali ni witr maana kuna
rakaa tumesalishwa moja tukatoa salamu au tatu tukatoa salamu na kuendelea na
mbili.
Baadhi ya maamuma walisimama
wakitaraji kuendelea na sala wengine walikaa walipofahamu inayosomwa ni
tahiyyatu si suratul fatiha tena.
Watu wakifuata tu ingawa ilikua wazi kuwa kuna
tatizo. Ilipotokea mara ya pili nkauliza kama ni mimi nlosinzia au kama kweli
tumesali rakaa kasoro?
Nikaambiwa naam na si mara ya kwanza Imam kupitikiwa usiku huo.
Nkataka kujua kwa
nn hajatahadharishwa?
Nkaambiwa mara ya kwanza alitanabahishwa. Ila kadri
alipokosea watu wakaenda naye tu.
Nlijaribu kupiga kofi kwa
upande wetu lakini watasikia wapi wanaume waliojitenga mbele na vipaza sauti?
Nikaamua siwezi kuendelea na sala. Nkatoka kujaribu kuwapata waumini wanaume
karibu na imam wasawazishe mambo lakini haijawezekana. Nkaamua kuondoka
Hivyo kubwa kwangu tena ni namna tusivyoweza
kuzuia au kurekebisha jambo likiharibika hata tukaacha litudhuru sote.
Pili ni kwa yuke
anayewaponza wenzako ndo kweli hawezi kujiambia? Kama umechoka au huko 100%
tabu gani ukaomba msaada ukae pembeni?
Tatizo jengine ni kuwa mara
nyingi hakuna wakumpokea yule anayeonekana ndo 'kiongozi'.
Haiwezekani Imam
kakosea au tuseme kazirai yule alosimama pembeni yake asiwe na ujuzi au ufahamu
wa kuongoza sala kutokana na dharura. Lakini inavyoelekea watu wanaunga safu
bila kuzingatia ujuzi na uwezo wao. Alimradi kasimama katika mstari na kaja
kusali!
Hakika kuna mafunzo mengi
hapa mengine hata sijayagusia na inafaa tutafakari tumesimama wapi na
tumesimama vipi!
Tuzinduane na tuelekezane mambo ya msingi si mambo
yasiotuongezea thamani yoyote katika ufahamu au uzingatiaji wetu.
No comments:
Post a Comment