Habari za Punde

Kesho Rasmin Dirisha la Usajili Zanzibar Linafunguliwa.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Dirisha la Usajili rasmi linafunguliwa kesho ambapo Makocha na Viongozi wengine wa Vilabu wanakuwa bize kutafuta wachezaji wanaowahitaji ili kuziboresha timu zao katika msimu mpya wa mwaka 2017-2018.
Hivi karibuni Chama cha Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” kilitangaza rasmi tarehe ya kuanza zoezi la uhamisho na usajili kwa msimu wa mwaka 2017-2018 ambao unatarajiwa kuanza kesho July 17, 2017 na kumaliza Agost 17, 2017.
Tayari ZFA imepata timu 12 zitakazoshiriki ligi kuu soka ya kwa msimu wa mwaka 2017-2018 ambapo wameamua timu zilizomaliza nafasi ya 1-6 kwa kila kanda, yani Unguja na Pemba ndizo zitakazocheza ligi kuu wakati huo huo Bingwa atapata nafasi ya kuwakilisha Zanzibar katika Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika.

Timu 16 kati ya 28 zilizosalia ambazo hazijashuka daraja zitacheza ligi two ambapo Bingwa wa ligi hiyo atapata nafasi ya kuwakilisha Zanzibar kwenye kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Timu hizo 12 zilizofanikiwa kucheza ligi kuu msimu mpya wa mwaka 2017-2018 ni JKU, Jang’ombe Boys, Zimamoto, Taifa ya Jang’ombe, Polisi, KMKM kwa upande wa Unguja na Pemba ni Jamhuri, Kizimbani, Mwenge, Okapi, Chipukizi na New Stars.

Kwa upande wa timu 16 zitakazocheza ligi 2 msimu mpya wa mwaka 2017-2018 kati ya hizo 8 za Unguja na 8 za Pemba ambapo za Unguja ni Mafunzo, KVZ, Black Sailors, Chuoni, Kilimani City, Kipanga, Miembeni City na Charawe wakati za Pemba ni Dogomoro, Wawi Star, Shaba, Young Islander, FSC, Hardrock, Chuo Basra na Opek.

Timu 4 za mwisho za ligi 1 zitashuka darajan la ligi 2, na timu 4 za juu za ligi 2 zitapanda daraja la ligi 1.
Attachments area

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.