Habari za Punde

Kikosi cha Kombaini ya Mjini Kukipiga Jioni Hii Mchezo wa Fainali Kutetea Taji Lake na Timu ya Fire Boys Michuano ya Rolling Stone

Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone timu ya Mjini Unguja  leo watatetea taji lao kwa kucheza fainali dhidi ya Fire Boys ya Karatu mchezo utapigwa saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Julious Nyerere huko Mbulu Mkoani Manyara.

Timu hizo zilikutana katika hatua ya makundi ambapo Mjini Unguja iliwafunga Fire Boys mabao 2-0 kwa bao za Ibrahim Abdallah "Imu Mkoko" na Abdul hamid Juma "Samatta".

Ikumbukwe kuwa Mjini Unguja ndio mabingwa watetezi wa Mashindano hayo kombe ambalo walilichukua tarehe 9 July, 2016 siku ya Jumamosi timu hiyo ya ilipotwaa ubingwa huo wa Rolling stone kwa mara ya Kwanza ndani ya miaka 15 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya DAREDA ya Mkoani Manyara katika uwanja wa SHEIKH AMRI ABEID mjini Arusha.

Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Vijana waliochini ya umri wa miaka 17 Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Rolling Stone, Mwaka huu 2017 yanafanyika katika Mikoa Ya Arusha na Manyara huku Manyara wakipata fursa ya Kuandaa Mashindano Hayo Kwa Mara ya Kwanza na kupewa Vituo Vitatu vya Mbulu,Babati na Mererani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.