Habari za Punde

Kocha Kwerekwe City aelezea siri ya mafanikio ya timu yake, apania kuipandisha daraja

 Kocha mkuu wa timu ya Kwerekwe City Suleiman Mohammed “Moo-Mani Gamera”

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kocha mkuu wa timu ya Kwerekwe City Suleiman Mohammed “Moo-Mani Gamera” amesema siri kubwa ya timu yake ni umoja wao kati ya Wachezaji, Walimu, Viongozi pamoja na Mashabiki.

Amesema umoja ndo silaha kubwa kwao kwani wachezaji wao wana ari kubwa ya kuipandisha timu yao daraja la Pili Taifa ili msimu ujao wa mwaka 2017-2018 wacheze daraja hilo.

“Siri kubwa ya kufanya vizuri timu yetu ni umoja wetu kwa pamoja sote Walimu, Wachezaji, Mashabiki na Viongozi lakini pia ari ya Wachezaji wangu, nawapenda kwa vile wanapenda mazoezi, mpira mazoezi najivunia sana kwa hili naamini kwa asilimia kubwa tutapanda daraja”. Alisema Gamera.

Kwerekwe City juzi walianza vyema katika mchezo wa ligi ya Mabingwa Wilaya Daraja la Pili baada ya kuifunga Afrikan Boys mabao 4-0.

Mabao ya City siku hiyo yalifungwa na Saleh Massoud dakika ya 12 na 63, Abdallah Omar dakika ya 50 na Ally Mohd "Vially" dakika ya 90.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.