Habari za Punde

Mjini Unguja na JKU Academy watinga robo fainali mashindano ya Rolling Stone

Wachezaji wa kikosi cha kombaini ya Wilaya ya Mjini

Na: Said Salim “Hazard” kutoka Mbulu, Manyara.

Wawakilishi wa wawili wa Zanzibar katika Mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki na kati ya Rolling Stone timu ya Mjini Unguja na JKU Academy watacheza hatua ya robo fainali leo mkoa wa Manyara na Arusha ambapo michezo yote minne ya hatua hiyo itapigwa saa 10:00 za jioni.

Kituo cha Mbulu Mkoani Manyara katika uwanja wa Julias Nyerere kutapigwa mchezo kati ya mabingwa watetezi Wilaya ya Mjini ya Zanzibar dhidi ya Lindi academy kutoka Lindi.

Na huko katika kituo cha Babati mkoani Manyara kutapigwa mchezo mmoja katika uwanja wa Babati kati ya Singi Academy dhidi ya Fire boys kutoka Karatu.

Na katika Mkoa wa Arusha kutapigwa robo fainal katika vituo viwili tofauti katika kiwanja cha Sheikh Amry Abeid mjini humo kutapigwa mchezo mmoja kati ya JKU academy kutoka Zanzibar dhidi ya Arusha central vijana kutoka hapo hapo Arusha.

Na huko katika kituo cha Mererani kutakua na mchezo mwengine wa robo fainali kati ya Saint Patrick dhidi ya Middle age.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.