Habari za Punde

Mapinduzi Imeibuka Kidedea Ligi Mabingwa ya Wilaya Kwa Kuifunga New Power.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Mapinduzi kutoka Wilaya ya Kusini Unguja imefanikiwa kuondoka na alama 3 muhimu baada ya kuifunga 1-0 New Power kutoka Wilaya ya Kati, kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa wa Daraja la Pili Wilaya pambano lililopigwa katika Uwanja wa Amaan.

Bao pekee la Mapinduzi limefungwa na Ali Ameir dakika ya 77 ya mchezo huo.
Ligi hiyo itaendelea tena kama ratiba ilivyo hapo chini:-
11/7/017 Kianga Int vs Shingwi Heroes
12/7/017 African Boys vs Kwerekwe City
15/7/017 New King vs Super Tiger
16/7/017 Uhuru vs Nyangobo
Mechi zote hizo zitachezwa saa 10:00 alasiri uwanja wa Amaan

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.