Habari za Punde

Mshambuliaji wa Timu ya Jamuhuri Kukosa Mechi Zote za Julai Ligi Kuu ya Zanzibar.

Na.AAbubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Mshambuliaji hatari wa klabu ya Jamhuri Khamis Abdulrahman Hamad “Mburu” atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu.

Nyota huyo atakaa nje ya uwanja kwa wiki tatu kufuatia kuchanika kwa nyama za paja muhuri la kushoto akiuguza jeraha hilo ambapo atakosa zaidi ya michezo 8 katika ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora.

Mburu ataanza kukosa michezo miwili yote timu yake itakayocheza Unguja katika Uwanja wa Amaan ukiwemo wa Jumatatu July 10 kati ya Zimamoto dhidi ya Jamhuri, na mwengine wa Alhamis July 13, 2017 kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Jamhuri ambapo pia akitarajiwa kukosa na michezo mengine ambayo yote itakayochezwa mwezi July.

“Daktari amenambia nitakaa nje zaidi ya wiki 3, ila kwasasa naendelea vizuri afya yangu namshkuru Mwenyezi Mungu, mana paja langu la kushoto lilichanika sana juzi”. Alisema Mburu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.