Habari za Punde

Rais Dk Shein mgeni rasmin katika uzunduzi wa Tawi la CRDB Chakechake

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe:Dk Ali Mohammed Shein, katikati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Tawi la Bank ya CRDB Mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe:Dk Ali Mohammed Shein, akiwa katika picha ya Pamoja na wajumbe wa bodi ya Bank ya CRDB Tanzania, mara baada ya kuifungua rasmi benk hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MKURUGENZI Mtendaji wa Bank ya CRDB Tanzania Dkt Charles Kimei, akizungumza na wananchi wa Chake Chake mara, baada ya kuzinduliwa rasmi benk ya CRDB Tawi la Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe:Dk Ali Mohammed Shein, akizungumza na wananchi wa Chake Chake mara baada ya kuifungua rasmi benk ya CRDB Tawi la Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Madungu Mjini Chake Chake, wakiwa katika madawati yaliyotolewa na Uongozi wa Bank ya CRDB Tanzania, ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kauli ya Dk Shein ya Kuchangia madawati kwa maendeleo ya elimu Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Mhe:DK Ali Mohammed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wa Serikali, wakurugenzi wa bodi ya benk ya CRDB na wanafunzi wa skuli ya msingi Madungu Chake Chake mara baada ya kukabidhiwa madawati 150.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe:Dk Ali Mohammed Shein, akimkabidhi madawati 150 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla mara baada ya kukabidhiwa na viongozi wa bank ya CRDB.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akimkabidhi madawati 75 mwalimu Mkuu wa Skuli ya Madungu Msingi, Ghanima Haji Ali mara baada ya kukabidhiwa na uongozi wa bank ya CRDB.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.