RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akikata utepe kuzindua Tawi la Benki ya RCDB katika Mji wa Chake chake Pemba leo,(kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB Bw.Ally Hussein Laay wengine (kulia) Mkugenzi Mtendaji wa CRDB Dr.Charles Kimei,[Picha na Ikulu.]
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein (kulia) akipeana mkono wa shukuranmi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB Bw.Ally Hussein Laay mara baada ya kuzindua Tawi la Benki ya RCDB katika Mji wa Chake chake Pemba leo,[Picha na Ikulu.]
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea katika Ofisi za Benki ya RCDB baada ya kuzindua rasmi leo (kulia) Meneja wa Tawi la CRDB Chake chake Pemba Nd,Hamadi Abubakar na (kushoto) Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira poa akiwa kaimu Waziri wa Fedha na Mipango Salama Aboud Twalib,[Picha na Ikulu.]
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Meneja wa Tawi la CRDB Chake chake Pemba Nd,Hamadi Abubakar (katikati) pamoja na Viongozi wengine na Wafanyakazi wa Benki hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Tawi la Benki ya RCDB katika Mji wa Chake chake Pemba uliofanyika leo,[Picha na Ikulu.]
STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Pemba 29.07.2017
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto
zinazowakabili wateja wa Benki nyingi hapa nchini ni msongamano wa wateja pamoja
na ucheleweshaji huduma na kuitaka Benki ya CRDB kuwa na mikakati katika
kupambana na kadhia hiyo.
Dk. Shein aliyasema hayo leo
huko Chake Chake Pemba, katika sherehe ya ufunguzi wa Tawi jipya la Benki ya
CRDB likiwa Tawi la 280 ndani ya mtandao wa benki hiyo kutoka matawi 19
iliyokuwa nayo mara tu baada ya kuanzishwa mnamo mwaka 1996.
Katika hotuba yake, Dk.
Shein alisema kuwa wananchi wanaeleza kwamba, miongoni mwa changamoto
zinazosababisha msongamano ni kuwa benki za hapa nchini bado haziendani na kasi
ya mabadiliko yanayotokea katika sekta ya fedha.
Alieleza kuwa katika Siku
ya Sherehe za Maadhimisho ya Mei Mosi, mwaka huu yaliyofanyika katika viwanja
vya Mahonda, Unguja, Wafanyakazi walipendekeza kuwa Serikali ikae na uongozi wa
benki mbali mbali ili ione namna ya kupunguza kero hii kubwa ya msongamano na
kuchelewa kutolewa huduma, hasa ifikapo mwisho wa mwezi.
“Leo nimeona ni busara nikuleteeni
mawazo hayo ya wafanyakazi, ambao pia, ni baadhi ya wateja wa benki zenu.
Wahenga wanasema ‘Mjumbe hauawi’ ndio maana na mimi nimeufikisha ujumbe kama
nilivyoambiwa”, alisema Dk. Shen.
Aidha, Dk. Shein alieleza
kuwa ni matumaini yake kuwa CRDB, itakuwa na mikakati imara ambayo itaweza
kupunguza msongamano wa ucheweleshaji wa huduma katika matawi yake.
Dk. Shein aliongeza kuwa
miongoni mwa sifa za Watanzania ni kuwa wako mstari wa mbele katika kutafuta
huduma bora sifa ambayo imethibitika juu ya namna walivyozipokea huduma za
uwekaji, upokeaji na utoaji wa fedha kwa njia ya mitandao.
Aliongeza kuwa kwa
matumizi ya huduma hizo, Tanzania ni miongoni mwa nchi iliyopiga hatua kubwa na
kuwa mfano Barani Afrika, hivyo wananchi Pmba watajitokeza kwa wingi kufungua
akauti na kufuata huduma wanazozitoa na kuitaka CRDB kuendelea kutoa huduma
bora.
Pia, alitumia fursa hiyo
kutoa wito kwa uongozi wa benki kuendelea kubuni mipango imara ya utoaji wa
elimu kwa umma kuhusu umhmu wa kutumia benki na kuitaka CRDB kuwapa wateja wao
na wananchi elimu juu ya umhimu wa kuweka akiba, kukopa, kurejesha na kufanya
shughuli za malipo kupitia benki.
Dk. Shein alieleza
kufurahishwa kwake na Benki ya CRDB kwa kuwa na utaratibu na mfumo wa kutoa
huduma zake kupitia simu za mkononi, mfumo ambao unawaondolea wananchi ulazimu
wa kwenda kwenye matawi ya benki ili kupata huduma na badala yake hupata huduma
zote kupitia simu za mikononi.
Kwa niaba ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wote wa Unguja na Pemba Dk. Shein alitoa
shukurani za dhati kwa Benki ya CRDB kwa kuchangia madawati 150 yenye thamani
ya TSZ milioni 20 kwa ajili ya skuli za msingi za Chake Chake pamoja na
michango kadhaa waliyowahi kuitoa sambamba na waliyoahidi kuitoa.
Pamoja na hayo, Dk. Shein
alieleza kuwa uzinduzi wa Tawi hilo ni kielelezo cha juhudi za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibatr katika kushajiisha wawekezaji wa ndani na nje kuja
kuwekeza katika sekta ya fedha kwa kutambua kuwa huduma za benki ni msingi
muhimu katika mabadiliko ya kweli katika sekta zote za kiuchumi na kijamii.
Alieleza kuwa CRDB ni miongoni
mwa Benki kubwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo, kufunguliwa kwa
Tawi la Benki hiyo kisiwanai Pemba ni habari njema, Pia ni benki yenye
kuaminika yenye ubunifu na kuendesha shughuli zake kwa umakini na umahiri
mkubwa tangu ilipoanzishwa mwaka 1996.
Aliongeza kuwa kukua kwa
sekta ya Benki kisiwani Pemba kutachochea ari na mwamko wa wananchi wa kuwa na
utamaduni wa kuweka fedha na amana zao Benki huku akitoa wito kwa wananchi
kujiunga na SACCOS ili wapate kuongeza nguvu za uzalishaji na kuirejesha mikopo
kwa wakati ili na wenzao waweze kufaidika.
Dk. Shein alieleza azma ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya uvuvi sambamba na
hata zilizofikiwa ili wavuvi pamoja na sekta hiyo izidi kuimarika na kuleta
tija kwa wavuvi pamoja na Taifa kwa jumla.
Mapema Kaimu Waziri wa
Fedha na Mipango Salama Aboud Talib ambaye ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na
Mazingira alieleza kuwa Serikali ya Mapindzi ya Zanzibar itaendelea kutoa
ushirikiano wake na Benki hiyo huku akisisitiza haja kwa benki hiyo
kushirikiana na ZSTC katika kuimarisha zao la karafuu.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Ally Hussein Laay, alisema kuwa takwimu zinaonesha
kuwa kisiwa cha Pemba kimeendelea
kujenga uchumi imara na hivyo kuongeza umuhimu wa kuwa na mfumo thabiti wa
fedha na ndio maana CRDB ikaamua kuanzisha tawi hilo huko Pemba.
Alieleza kuwa katika tawi
hilo jipya pamoja na uwepo wa huduma zote za kibenki ikiwemo akauti, mikopo,
bima na ushauri wa fedha na uwekezaji, benki hiyo pia, imo mbioni kuazinsha
huduma maalum inayozingatia sheria na misingi ya dini ya kiislamu “Islamic
Banking”.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei alisema kuwa ukubwa wa amana za benki hiyo
tayari umeshafikia TZS trilioni 4.1 hadi mwezi Juni mwaka huu 2017 na tayari
imeshafungua matawi katika nchi ya Burundi.
Aidha, alitoa pongezi zake
kwa Dk. Shein kwa mashirikano makubwa inayoyapata Benki hiyo kutoka Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar huku akieleza kuwa mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka jana
benki ya CRDB ilitoa mikopo yenye thamani ya shilingi trilioni 3.3 kwenye sekta
za kilimo, usafirishaji, utalii, viwanda na ujenzi wa miundombinu.
Alieleza kuwa baadhi ya
miradi mikubwa iliyofaidika na mikopo hiyo ni ujenzi wa uwanja wa ndege wa
kisasa wa Dar-es-Salaam (terminal 3), mradi mkubwa wa umeme vijijini (REA),
Ujenzi wa Soko kuu la Mwanjelwa-Mbeya na mingineyo mingi ikiwemo ya watu
binafsi.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment