Habari za Punde

Timu ya Negro Yawaacha Wachezaji Wake Zaidi ya 10 Pamoja na Kocha Wao. Wamepania Kuwatangaza Wachezaji Wapya Siku Yao Maalumu ya Negro Day.

Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.
Dirisha la usajili limeshafunguliwa tangu July 17, 2017 kwa timu mbali mbali kuanza kufanya usajili wa wachezaji na zingine zikianza mazoezi, timu ya Negro FC inayoshiriki ligi daraja la Pili Taifa imeweza kuweka wazi majina ya awali ya baadhi ya wachezaji ambao hawataitumikia katika msimu ujao wa 2017/2018.

Negro ambayo msimu uliopita ilikua na kikosi bora kabisa ambacho kwa bahati mbaya kilishindwa kupanda Daraja la Kwanza Taifa na kusalia hapo hapo katika Daraja la Pili Taifa, lakini msimu huu kimepania kufanya kweli.

Kutokana na ripoti ya Benchi la Ufundi iliyowasilishwa mwishoni mwa Mwezi June, 2017 baadhi ya wachezaji hawataitumikia tena Negro kwenye msimu ujao baada ya kuachwa huru, wachezaji hao wapo huru kujiunga vilabu mbalimbali:

Wachezaji hao ni:
1. Abdul razak Omar Mohd (Bile)
2. Ibrahim Khamis Ame (Bura)
3. Vuai Ali Simai
4. Juma Abeid Rajab (Okocha)
5. Omar Othman Omar
6. Abubakar Iddi Myaa
7. Fahim Khalfan Hemed (Dame)
8. Masemo Makungu Masemo
9. Muhidin Thabit

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa timu hiyo Hussein Ahmada hii ni orodha ya awali ya wachezaji ambao hawataitumikia Negro FC msimu ujao, huku zoezi la usajili likiendelea kujaza baadhi ya nafasi zilizopo kulingana na maelekezo ya Benchi la Ufundi, Benchi ambalo kwasasa linaongozwa na kocha Mohammed Salah (Richkard) akichukua nafasi ya kocha ya Hassan Abdul rahman.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.