Habari za Punde

Timu za Taifa ya Jangombe na Mwenge Zinasua sua Katika Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora.

Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.
Hatua ya 8 bora ya ligi kuu soka ya Zanzibar ni ligi ya heshima tu kwaajili ya kuwatafuta Wawakilishi wa Zanzibar watakaoshiriki Mashindano ya Kimataifa ambapo Bingwa atawakilisha kwenye Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika na mshindi wa pili atawakilisha kwenye Kombe la Shirikisho Barani humo ambapo msimu uliopita Zimamoto na KVZ waliwakilisha Zanzibar katika Mashindano hayo.

Lakini pia timu zote 8 zilizofanikiwa kutinga hatua hiyo zimepata fursa ya kucheza ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu ujao wa mwaka 2017-2018 ambapo msimu huo ligi hiyo itakuwa na jumla ya timu 12 tu.

Yote tisa lakini kumi Timu ya Taifa ya Jang’ombe na Mwenge haziwahi kupata ushindi hata mchezo mmoja katika michezo 6 yao yote waliyocheza kwenye ligi hiyo nakupelekea kuwa katika nafasi ya 7 na 8 kwenye ligi hiyo.

Taifa ya Jang’ombe inashika nafasi ya 7 kwa alama zake 3 kufuatia kwenda sare 3 na kupoteza 3 ambapo mpaka sasa katika ligi hiyo hawana furaha ya ushindi.

Mwenge nafasi ya 8 baada ya kwenda sare mchezo 1 na kupoteza michezo 5 akiwa na alama yake 1 pekee nae anaungana na Taifa kwa kutoshinda hata mchezo 1 kwenye ligi hiyo.

Wawili hao yani Taifa na Mwenge  kesho Ijumaa wanakutana kwa pamoja kwenye Mzunguko wa saba wa ligi hiyo mchezo ambao utapigwa saa 10  jioni katika uwanja wa Gombani huku Mashabiki wengi wakisubiri nani ataonja furaha ya ushindi kwa mara ya kwanza au watatoka sare na kuendeleza historia yao mbovu katika ligi hiyo ya kutoshinda hata mchezo mmoja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.