Habari za Punde

Ujumbe wa Zanzibar Waendelea na Ziara Yao Nchini Comoro.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akizungumza na Gavana wa Comoro wakati wa ziara yao Nchini Comoro kuimarisha Uhusiano wa Nchi Mbili hizi Zanzibar na Comoro. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro Mhe Mohammed Bacar Dossari akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Gavu baada ya mazungumzo yao wakati wa ziara yao ya Kiserikali Nchini Comoro kukuza Uhusiano baina ya Zanzibar na Comoro.
Gavana wa Mji wa Ngazija Mhe.Mohammed  Bakar akipokea zawadi ya mlango wa Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Gavu. wakati wa hafla yao yac ziara ya kiserikali kutembelea Nchini Comoro.
Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Comoro baada ya mazungumzo ya pande mbili hizo kukuza ushirikiano Kati ya Zanzibar na Comoro Ujumbe huo wa Zanzibar unaongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Gavu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.