Habari za Punde

HAJIBU Aanza Makali Yake Mjini Zenj, Afanya Vitu Si Mchezo Yeye na KAMUSOKO

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.


Mshambuliaji mpya wa Yanga, Ibrahim Hajib jana ameonesha kiwango cha hali ya juu kabisa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege uliopigwa saa 2 za usiku katika uwanja wa Amaan ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mbali ya kuonesha uhodari wake wa kuuchezea mpira Ajibu pia alifungua akaunti yake ya mabao baada ya kufunga bao lake la kwanza dakika ya 50 katika historia ya klabu yake hiyo mpya tangu ajiunge nayo akitokea Simba.

Bao hilo la Hajib ni msaada mkubwa wa Kiungo wa wakimataifa wa Zimbabwe Thabani Kamusoko ambae alipiga shuti kali na Ajib akamalizia.

Bao jengine la Yanga lilifungwa na Emanuel Martin dakika ya 73 ambapo ni bao lake la pili katika msimu huu kuanza kufuatia kushinda bao la ushindi Yanga walipoifunga Singida United 3-2.

Kikosi cha Yanga kimeondoka  kisiwani Unguja asubuhi ya leo Jumatatu kwa Ndege na kwenda Kisiwani Pemba kuweka kambi kujiandaa na pambano na mtani wake, Simba katika mchezo wa Ngao ya Hisani utakaopigwa Agost 23, 2017 kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.