Habari za Punde

Ali Bushiri afutwa rasmi ukocha timu ya Mwadui FC ya Shinyanga

Aliekuwa Kocha mkuu wa Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Ali Bushir “Bush”
Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.
Kocha mkuu wa Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Ali Bushir “Bush”amefutwa rasmi kazi kuwa kocha wa timu hiyo baada ya kuongoza timu hiyo kwa nusu msimu na kuisaidia kubakia kwenye ligi kuu soka Tanzania bara.

Taarifa hizo tumezithibitisha kupitia ukurasa wake mwenyewe mwalimu huyo wa Facebook ambao ameandika kuwa amefutwa rasmi kazi huku pia akielezea sababu iliyopelekea kuondoshwa.

“Shortlly ni kua NIMEFUTWA rasmi kazi ya kuwa kocha Mkuu wa timu ya Mwadui Fc kwa kipindi kifupi cha nusu mwaka niliokua nikiihudumikia. 

"Ukweli hakuna Mtanzania hata mmoja ambae ni mdau wa soka ndani ya nchi yetu asiyejua ni kwa vipi nliisaidia timu hio katika kazi ambayo walinichukulia kuifanyia timu hiyo na naam niliifanya na lakini si kwa ujanja wangu tuu bali na Mungu alinisaidia katikz kuifanikisha kazi hio. 

Kuna vitu vitatu ambavyo viliniponza hadi kufikia kuipoteza kazi yangu hio. 
La kwanza ni haki zangu {financially}, la pili ni kuhusu usajili na la tatu ni kuhusiana na chuki na choyo kutoka kwa msaidizi kocha niliyekua nae  kwa vile yeye ndie niliemkuta pale. 

So Paaalllsss kwa maelezo yangu zaidi fuatilieni magazeti ya kesho kwa vile kuna gazeti la michezo mtaikuta story hio.

Lakini all above all mii si mwalimu mkuu tena wa Mwadui fc”. 
Aliandika Bush katika ukurasa wake wa  Facebook na kuendelea

“Any way! Who knows? Just wait nione wapi nitakapoelekea hukohuko katika ligi kuu ya Vodacom na Insha Allaah nitawajuulisha tuu Paaallllssss wangu.

Na tayari nimeshapata mialiko kadhaa ila tuu bado sijaamua ni wapi nielekee. 

Paaalllss nimeamua kuwaambia ukweli wangu katika hili ili tuu msikilize ya watu mitaani, ukweli ni huo.. Gd9t Paaaalllss...!!!!”.

Katikati ya msimu uliopita Bushir alichukua mikoba ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kujiunga na Mwadui FC ambapo aliikuta timu hiyo ipo nafasi ya tatu kutoka chini na kufanya kazi kubwa mpaka kuisadia kuinusuru kushuka daraja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.