Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jingo la
Mkombozi Saccos lililpo Kizimkazi Dimbani wakati wa Sherehe za Siku ya Kizimkazi
Viongozi na Wageni mbali mbali walijumuika kula chakula cha asili cha Wakizimkazi wakati wa sherehe ya Siku ya Wakizimkazi.
Mashindano ya kukuna nazi yawa kivutio wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi.
Mashindano ya kusokota kamba
Vijana kutoka Kusini mwa Kizimkazi wakivuta kamba wakishindana na vijana wa kaskazini wakati wa sherehe za Siku ya Wakizimkazi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Sherehe za Siku ya
Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini
mkoa wa Kusini, Unguja.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Bw. Sudi Simba ambaye alifika Kizimkazi kutambulisha huduma ya bima ya Afya ya Afya Wote wakati wa Sherehe za Siku ya
Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini
mkoa wa Kusini, Unguja.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vipeperushi vyenye taarifa ya huduma ya bima ya Afya ya Afya Wote
wakati wa Sherehe za Siku ya
Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya
Kusini
mkoa wa Kusini, Unguja.
Wakazi wa Kizimkazi wakiangalia ngalawa 15 zikichuana vikali ikiwa sehemu ya sherehe ya siku ya Wakizimkazi
Wananchi wakimpokea mshindi wa pili katika mashindano ya Ngalawa kijana Ahmed Yusufu Hassan ambaye ngalawa yake ameipa jina la Ndio Mambo
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pongezi kijana aliyeshinda kwenye mashindano ya Ngalawa Bw. Ali Khamisi Mgeni akiwa na chombo chenye jina la Sea Never Dry.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan amewahimiza wakazi wa Kizimkazi kujiandikisha Bima ya Afya kwani ndio mfumo
ambao utawawezesha kupata matibabu haraka na kwa gharama ndogo.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa Sherehe ya
Siku ya Wakizimkazi ambapo siku hiyo wakazi hao hukutana na kupeana
taarifa za maendeleo na kupanga mipango ya baadae kasha kula chakula cha asili
pamoja na michezo ya asili.
Mhe. Samia aliwaeleza wananchi hao kuwa hakutokuwa na mjomba
atakayekuja kuwaletea maendeleo na alihimiza kwa kusema “Maendeleo ya Kizimkazi
yataletwa na Wakizimkazi wenyewe”.
Katika Sherehe hizo Makamu wa Rais alifungua jengo la Ofisi
ya Saccos ya Mkombozi lililopo Kizimkazi Dimbani na Kukagua maendeleo ya Ukumbi
wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi.
Mchezo wa Kuvuta ,kusokota kamba, kukuna nazi na mbio za
Ngalawa zilionekana kuvutia watu wengi.
Makamu wa Rais alihimiza wanamichezo kujitokeza kwa wingi
mwakani kwani michezo hudumisha umoja na
kuleta mshikamano katika jamii.
No comments:
Post a Comment