Habari za Punde

Mashindano ya vyuo vya mafunzo ya amali kufanyika Zanzibar


Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mamlaka ya Mafunzo ya Amali imeandaa mashindano ya mpira wa miguu ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi siku ya kesho Jumaatatu Agost 14, 2017 ambapo yatazinduliwa rasmi kwenye viwanja vya Amani nje kwa kushirikisha vyuo 12 vilivyopo chini ya mamlaka hiyo.

Akizugumza na Mtandao huu mwenyekiti wa kamati ya mashindano hayo Mwalimu Mkubwa Ibrahim Khamisi amesema kwa kuamini michezo ni ajira ndio maana wakafanya hivyo na lengo nikupata washiriki kwenye mashindano ya elimu bila malipo.

“Michezo ni ajira ndo mana tumeanzisha mashindano haya, tunajua vipaji vipo vingi sana Zanzibar, hivyo tunawaomba wadao wa soka kujitokeza kuangalia vipaji”. Alisema Mkubwa.

Katika Mashindano hayo ambayo yamejumuisha jumla ya Vyuo 12 ambapo vimepangwa katika Makundi 2 tofauti yani kundi A na B.

Kundi A kuna chuo cha Institute of Business and Social Study, Zanzibar Commercial Institute, Zanzibar Mosquito Net, Chuo cha Wazazi cha Forodhani na Chuo cha Mwanakwerekwe wakati kundi B kuna chuo cha Melisha, Mwenge, Stone Town Youth Center, Microtech, Mkokotoni na Chuo cha Ufundi cha Polisi.   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.