Habari za Punde

Milele Zanzibar Foundation Supports Professionalism in Rural Healthcare!Vijana Viongozi wa Mradi wa “Champions in Health”Watayarishwa Kujitolea Katika Vituo Vya Afya Vijijini 
Mbweni, Zanzibar, 6 Agasti 2017

Ili kuboresha utoaji wa huduma bora za afya vijijini Zanzibar, Asasi ya Milele la Zanzibar Foundation (MZF) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Skuli ya Sayansi ya Afya na Tiba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wizara ya Afya, inawasaidia wanafunzi 98 kutoka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) na Skuli ya Sayansi ya Afya na Tiba kwa kuwalipia ada za masomo, Mafunzo maalumu ya Uongozi na Stadi za maisha, fedha za kujikimu wanapokwenda katika mafunzo ya vitendo vijijini kupitia mipango ya mradi wa “Champions in Health”

Katika sherehe hii mapema leo, Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya, Dk Fadhil M. Abdallah aliwatunukia “Champions”vyeti vya ushiriki na kukamilisha mafunzo ya uongozi, maadili, na mafunzo yakujiandaa kujishirikisha kwa wanajamii na kuwapa maeneo yao wataoenda kujitolea katika vituo vya afya vijijini. Wanafunzi 48 watakwenda kujitolea katika vituo 16, 10 Unguja na 6 Pemba, kwa muda wa mwezi. Huu ni mwaka wa tatu ambao wanafunzi hao wa Champions wanakwenda kujitolea na kujenga uzoefu na hamu ya kuboresha huduma za afya katika maeneo ya vijijini.

“Champion” wataunga mkono shughuli za afya za jamii ili waweze kuelewa vizuri matatizo na changamoto za utoaji wa huduma za afya za vijijini, na pia kujenga taaluma, uzoefu na ujuzi utaoweza kuwasaidia kukumbana na matatizo mbalimbali ya utoaji wa huduma za afya vijijini"anaelezea Mkuu wa Programu za Milele Zanzibar Foundation, Khadija Shariff 

Katika maandalizi ya kuanza kazi yao ya kujitolea, “Champion” wamekamilisha wiki moja ya kujenga taalamu ya “ujuzi laini”. Mafunzo na warsha zililenga kuimarisha uongozi na ushiriki wa wanajamii kwa njia ya mawasiliano, kutatua matatizo, kujenga umoja wa wafanyakazi (team building), usimamizi wa uandaaji wa miradi, na ujuzi wa huduma bora kwa wateja.


"Mafunzo yamewapa “Champion” utaalamu na ujuzi wa kutumikia jamii na kubuni miradi rahisi kwa kushirikiana ili kuweza kutatua masuala yanayohusiana na afya. Ni mafunzo muhim sana kuwafundisha vijana wa leo, ili waweze kuwa wafanyakazi na viongozi bora wa baadae. Tunaishukuru sana Milele Zanzibar Foundation kwa kutoa fursa hii kwa vijana wetu na kwa jamii kwa ujumla.". anaeleza Bi Amina, Mkuu wa Chuo, ZA) Chuo cha Sayansi ya  Afya na Tiba.

Mafunzo yaliwezeshwa na mtaalamu wa Uongozi na Usimamizi Yahya Khatib Haji, Mr. Edson LassyNyingi, Mshauri wa Ufuatiliaji & Tathmini kutoka Dar-es-Salaam, na Khadija Abbas Mohamed, Afisa Muguzi wa Afya ya Umma, mafunzo hayo yaliimarisha utaalamu wa kazi, kujitolea, na ujuzi wa uongozi unaohitajika kukabiliana na changamoto za afya zinazojitokeza vijijini pamoja  na taaluma mahsusi za afya kwa ujumla mbazo zitawasaidia kushiriki kikamilifu kwa wanajamii, kuelimisha na kuwa mawakala wa mabadiliko katika jamii za vijijini

Mafunzo yalijumuisha, mambo yafuatayo, kujitambua, kufanya kazi kwa pamoja(team work), ujuzi wa uongozi, kujitolea, maadili, vipimo vya ubora wa utoaji wa huduma, ukarimu wakati wakutoa huduma kwa wagonjwa, usanifu wa miradi, mipango ya maendeleo, na kutathmini mahitaji ya jamii.

ENGLISH

For Immediate Release

Young “Champions in Health” Leaders Prepare for Medical Assignments in Rural and Marginalized Areas

Mbweni, Zanzibar, 6 August 2017 -To improve the quality of health service delivery in rural Zanzibar, Milele Zanzibar Foundation in partnership with State University of Zanzibar (SUZA) School of Health and Medical Sciences and the Revolutionary Government of Zanzibar Ministry of Health, is supporting 98 studentsfrom SUZA School of Health and Medical Sciences with scholarships, training, and internships in rural regions through the “Champions in Health”(Champions) program.

At a ceremony earlier today, Ministry of Health, Director of Prevention, Dr. Fadhil M. Abdallah presented the Champions with certificates of completion for leadership, ethics, and community engagement training and assigned them their locations for their month-long volunteer “Fieldwork” in rural Zanzibar. 

“The Champions will support community health activities so that they can better understand the issues and challenges of rural based healthcare service delivery, as well as develop professional skills necessary to solve various health related issues,” explains Head of Programs at Milele Zanzibar Foundation, Khadija Shariff.

In preparations to commence their volunteer fieldwork, Champions have completed a week long professional development“soft-skills” training. The trainings and workshops focused on strengthening leadership and community engagement through communication, problem solving, team building, program cycle management and customer service skills.

”The trainings have provided the Champions with skills and knowledge to better serve the communities and design simple participatory projects to solve health related issues. These skills will help develop the youth into better quality service providers and leaders of tomorrow. We thank Milele Zanzibar Foundation for creating this opportunity for these youth as well as for the community at large.”  explains Professor Amina, Dean of School of Health and Medical Sciences.

Facilitated by Leadership and Management Consultant Yahya Khatib HajiMr. Edson LassyNyingi, a Monitoring & Evaluation Consultant from Arusha, and Khadija Abbas Mohamed, Zonal Public Health Nursing Officer, the trainings strengthened professional, volunteerism, and leadership skills needed to deal with challenges in rural health care specifically and the healthcare profession in general so that they may engage, educate and be active agents of change in rural communities.

The trainings focused on, among other things, self-awareness, team-work, leadership skills, volunteerism, ethics, dimensions of quality service delivery, customer care, project cycle management, development planning, and assessing community needs.

For More Information Contact: Zuhirah Khaldun-Diarra, +255 779639889 zkhaldun@gmail.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.