Habari za Punde

Timu ya Prisons inayoshiriki Ligi Kuu Bara kujjipima nguvu na Ngome keshoNa: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Tanzania Prisons ambayo imeweka kambi visiwani Zanzibar kesho Jumanne Agost 15, 2017 itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ngome mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Fuoni kuanzia saa 10:00 za jioni.

Kiingilio katika mchezo huo ni Shilingi Elfu moja tu.

Prisons ambayo inafundishwa na kocha Mzanzibar Abdallah Mohd “Bares” ipo kambi visiwani hapa kwa kujiandaa na ligi kuu soka ya Tanzania bara msimu mpya ambapo mchezo wao wa kwanza wa ligi hiyo watacheza Jumamosi Agost 26, 2017 dhidi ya timu mpya iliyopanda daraja ya Njombe Mji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.