Habari za Punde

Wateja wa Zantel Kufurahia Huduma za Simu na Internet Zilizoboreshwa Zaidi.

Mkuu wa masuala ya Teknolojia  na Ufundi Zantel, Larry Arthur (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kisiwani Zanzibar hivi karibuni kuhusu uboreshwaji wa mtandao wa Zantel baada ya Kampuni hiyo kupokea vifaa vipya kutoka Ericsson na Huawei Technologies vitakavyotumika kuboresha mtandao huo. Wengine kutoka kushoto ni William Cheng (Wei) wa Huawei Technologies, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa (Baucha) na Mwakilishi wa Kampuni ya Ericsson, Frode Dyrdal.

Ø Mtandao wa kwanza wa Mawasiliano kutoa huduma ya mtandao wa 4G Pemba
Dar es Salaam. Wateja wa Zantel sasa wataendelea kufurahia huduma zenye ubora wa hali ya juu kwenye upigaji wa simu na kunufaika na matumizi ya data yenye kasi. Zantel imekuwa kampuni ambayo imepiga hatua kwa kuboresha huduma yake ya mtandao na kuahidi kuendelea kuleta mabadiliko kwenye sekta ya mawasiliano ili kuendelea kubadili maisha ya mamilioni ya watu nchini Tanzania.

Ofisa Mkuu wa Masuala ya Ufundi na Teknolojia Zantel, Larry Arthur alisema,  “ Tumeanza kuboresha mtandao wetu tangu Septemba ya mwaka 2016  na tulikuwa na lengo la kukamilisha kazi yetu mwezi Juni mwaka huu, lakini kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kipindi cha hivi karibuni, ukamilishaji wa kazi hii umechelewa kufanyika kwa wakati”.

Mchakato wa kuboresha mifumo yetu ya mtandao Zanzibar na Tanzania Bara kwa sasa inakaribia kukamilika  na tunafurahi kuwaeleza wateja wetu kwamba tayari tumeshaanza  kufurahia matunda ya ubora wa usikivu  katika kupiga simu na huduma za data kupitia mtandao wa 4G wa Zantel wenye kasi zaidi.

Kuboresha mfumo wetu wa mtandao kumeimarisha mfumo wa mtandao wa Zantel na kufika maeneo mengi zaidi pia watumiaji wa intaneti wamenufaika na huduma ya haraka ya 4G inayopatikana kwa sasa.
Zantel imekamilisha awamu ya kwanza ya uboreshaji wa mtandao Kisiwani Pemba na Mkoa wa Magharibi Unguja kuweka mfumo wa mtandao wa kisasa. Baada ya kukamilisha awamu hii, inayofuata itakuwa ni kuimarisha miundombinu ya Zantel eneo la Kaskazini na Kusini mwa Unguja. 

Awamu ya pili inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu na mara itakapokamilika kwa maeneo yote, Zanzibar  na Tanzania Bara zitanufaika na huduma bora za intaneti na ubora kwenye upigaji simu.

Kwa jumla mradi wote unatarajiwa kukamilika kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 10 na tayari zimeanza kutumika katika maeneo yote mjini Zanzibar, huku kukiwa tayari kumefungwa teknolojia ya kisasa pamoja kwenye vituo vilivyopo Zanzibar na Tanzania Bara.

Washirika wetu wameanza utekelezaji kwa haraka ili kuhakikisha kwamba mtandao wa Zantel unaenea katika maeneo mengi nchini. Hii inamaanisha kwamba Zantel itaweza kutoa huduma nzuri ya upigaji simu wenye usikivu mzuri pamoja na data kwa watumiaji wake huku ikiwa ni kampuni inayotoa huduma ya mtandao kwa zaidi ya asilimia 85 kwa jamii ya Watanzania huku ikiwa ni Kampuni inayotoa huduma bora ya intaneti kupitia mtandao wake wenye kasi zaidi wa 4G.

“Wakati tukiendelea kufanyia kazi maeneo yaliyosalia kwa Unguja , tunaendelea kuzingatia ubora wa mifumo yetu kupitia taarifa tunazozipata kutoka kwa wateja wetu kwa njia ya mawasiliano tuliyoweka pamoja na vituo  maalumu vya kupokea taarifa ambavyo kwa kiasi kikubwa vimekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha ubora wa mtandao na huduma ya mtandao,” alisema.

Zantel inamkaribisha kila mmoja kujaribu na kufurahia huduma ya mtandao wa 4G kutumia data mahali popote nchini Tanzania, huduma za kifedha kwa njia ya simu, huduma za kibiashara na huduma za kibenki nchi nzima.

KUHUSU ZANTEL
Mtandao wa Mawasiliano wa Zanzibar (Zantel) ni wa kipekee kwa mawasiliano nchini Tanzania unaofungua milango kwa huduma za kimataiafa za simu na data kupitia huduma zake za CDMA, GSM, 3G  na 4G.
Zantel imekuwa ikihudumia wateja wake kwa ubora na huduma ya haraka ya intaneti yenye kasi nchini Tanznia.
Zantel imepokea tuzo mbalimbali kutokana na kutambuliwa kutoa huduma bora na ufumbuzi kwenye sekta ya mawasiliano. Baadhi yake ni pamoja na Tuzo ya GSMA M – Health. Zantel imedhamiria kuwaunganisha watu ulimwenguni ili wawe mstari wa mbele kupata tarifa kwa haraka.
Kwa maelezo zaidi tafadhali, tembelea mtandao wetu…www.zantel.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.