WAZIRI
asiekuwa na wizara maalum Mhe: Said Soud Said, akiwaambia wananchi wa Mgogoni
kuwa, hakuna uchaguzi mwengine hadi mwaka 2020, mara baada ya kupewa nafasi na
Rais wa Zanzibar, kujitambulisha kwa wananchi, waliohudhuria uzinduzi wa skuli
ya Msingi na kati ya Mgogoni, kazi iliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed Shein
Katibu Mkuu wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar,
Khadija Bakar Juma, akizungumza machache, mara baada ya Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed Shein, kuifungua skuli ya
msingi na kati ya Mgogoni wilaya ya Wete, ikiwa ni sehemu ya zaiara yake ya
siku tano Kisiwani Pemba
WAZIRI wa
Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe: Riziki Pembe Juma, akizungumza kwenye
ufunguzi wa skuli ya mpya ya msingi na kati ya Mgogoni wilaya ya Wete kisiwani
Pemba, ambapo skuli hiyo, ilizinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
baraza la Mapinduzi, Mhe: Dk Ali Mohamed Shein, ikiwa ni sehemu ya ziara yake
ya siku tano kisiwani Pemba
RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed Shein,
akiwasalimia wanafunzi na waalimu wa skuli ya Msingi na kati ya Mgogoni wilaya
ya Wete, mara baada ya kuizindua skuli yao mpya, ikiwa ni sehemu ya ziara yake,
ya siku tano kisiwani Pemba
WANAFUNZI wa skuli
ya Msingi na kati ya Mgogoni wilaya ya Wete, waliohudhuria uzinduzi wa skuli
mpya, kazi iliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe: Dk Ali Mohamed Shein, ikiwa ni sehemu ya zaiara yake ya siku tano Kisiwani
Pemba
Jengo jipya
la skuli ya msingi na kati ya Mgogoni wilaya ya Wete, ambalo Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe:
Dk Ali Mohamed Shein, alilizindua, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tano
kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
No comments:
Post a Comment