Habari za Punde

Yanga kucheza na Mlandege ya Zanzibar

Baadhi ya wachezaji wa kizanzibari wanaochezea Timu ya Yanga wakiwa katika Selfie

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu soka ya Tanzani Bara timu ya Yanga Sports Club wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mabingwa wa zamani wa Zanzibar timu ya Mlandege Sports Club mchezo ambao utasukumwa Jumapili Agost 13, 2017 saa 2:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan.

Yanga ambao wanatarajia kuweka kambi Kisiwani Pemba watalazimika kukaa siku moja Kisiwani Unguja kwaajili ya mchezo huo kisha kuendelea na safari ya kwenda Pemba kujiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya mpinzani wao wa Jadi Simba.

Akizungumza na Mtandao huu Katibu wa Soka Wilaya ya Mjini Yahya Juma Ali ambae yeye ndie mratibu wa mchezo huo amesema Yanga watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege na matayarisho ya mchezo huo yanaendelea vizuri kwani tayari washawatafutia Hoteli ya kuiweka Yanga siku moja itakapokaa Unguja.

“Yanga watacheza na Mlandege Jumapili usiku katika uwanja wa Amaan, matayarisho yapo vizuri sana kwani mpaka Hoteli tushawaekea Yanga kwa siku moja watakayokaa Unguja kisha wataenda Pemba kwaajili ya kambi”. Alisema Yahya.

Simba na Yanga zitakutana katika mechi ya Ngao ya Jamii Agosti 23, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salam mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.