Mwandishi Haji N. Mohamed Pemba.
“Jina langu ni Chen Er Dong,
nimezaliwa mwaka 1975 kijiji cha Nan Jing nchini China”.
Tokea niko skuli
nilikuwa napenda niwe daktari, hivyo baada ya kumaliza masoma, kwa vile
nilikuwa na sifa za kusomea udaktari, nilifanikiwa na kujiunga na chuo nchini
China.
“Chuo
nilichosoma kinaitwa ‘Nan Jing Medical College’ na mapema mwaka 2002
nilimazalia masomo yangu ya udaktari, na hapo nikaanza kazi kwenye hospitali ya
‘Nan Jing First Hospital”,
Dr.Chen,
anasema aliamua kujitupa kwenye fani ya udakatari kutokana na mahaba na kupenda
kwakwe kuihudumia jamii moja kwa moja, badala ya kuwa mhandishi ujenzi au kazi
ya uwalimu kama alio nayo mama yake mzazi.
“Mama yangu yeye
ni mwalimu wa lugha ya kichina na baba ya anajishughulisha kazi zake binafsi,
ingawa mimi sikupenda kazi za wazazi wangu, niliamua niwe daktari na sasa ndio
mimi nimekuwa’’,anasema.
Anasema
maisha ya China nayo sio mepesi sana kama wasiokuwa wachina wanavyofikiria,
bali ni kupambana kama ilivyosehemu nyengine duniani.
“Kila kitu
ni mapambano, na kila eneo ulilozaliwa lina mapambano yake ya kimaisha kwa
mujibu wa mahitaji ya anaepambana na maisha, hata China unabidi upambane ili
upate maisha”,anasema.
Ukurasa huu
wa makala, ulimuuliza Dr. Chen, iwapo taaluma ya shahada ya pili ya koo, pua na
skio, ‘Master Degree’ alionayo kama alisomeshwa na Serikali ya watu wa China,
hilo alililipinga.
“Tena
afadhali nyinyi huku Tanzania na Zanzibar, nasikia mna bodi za mikopo ya elimu
ya juu, ambayo wanafunzi wanaomba na kisha kukukopeshwa fedha za kusoma, lakini
mimi China hiyo sijaona na hakuna”,anaeleza.
Hivyo Dr. Chen, ambae kwa sasa ndio kiongozi wa madaktari saba waliopo kwenye Hospitali
ya Mkoa wa Abdalla Mzee Mkoani kisiwani Pemba, anasema alisomeshwa na familia
yake (baba na mama).
“Kwetu mtoto
mmoja kwa familia moja, na pengine ndio faida ya wazazi wangu kumudu
kunisomesha hadi leo hii, kuwa daktari ninaetambulika na serikali ya watu wa
China na hata Zanzibar’,anafafanua huku akicheka.
Sera ya
mtoto mmoja nchini China, ambayo ipo kwa baadhi ya miji, anaamini ni mwarubaini
kwa familia yengine nchini humo, kuwapatiwa haki nzuri ya malezi, elimu na hata
uangalifu wa kina kwa mtoto wao.
Chen anasema,
hakutarajia kwenye maisha yake kupanda ndege kutoka nje ya jiji la China lenye
wakaazi zaidi ya billion moja, ingawa mwaka huu wa 2017, ulimuwezesha kutua
Tanzania na kisha Zanzibar.
Daktari huyu
ambae na yeye ameshatekeleza sera ya kuwa na mtoto mmoja mwenye umri wa miaka
mitatu sasa, anasifia sana visiwa vya Zanzibara na hasa Pemba anakofanyia kazi
kwa muda wa ammoja ujao.
“Juzi
nilikwenda Unguja, nikakaa kwa siku kadhaa, lakini baada ya kurudi Pemba, hapa
ni patamu sana na kama sio utaratibu wa nchi yangu, basi natamani nishi na
familia yangu milele”,anaeleza.
Chen,
kilichomvutia kisiwani Pemba, ni mambo kadhaa moja ni utulivu, pili ukarimu wa
watu uliopindukia mipaka, tatu ni wananchi waliopo kupenda wageni na hasa
wanapokuwa wanazunguruka mitaani.
Binafsi,
anasema hutamani sana muda wa kazi ufike ili akutane na wananchi wa Pemba,
ambao anasema wanaonyesha moyo wa tabasamu hata kama, wanaugua.
“Kufanya
kazi sehemu yenye utulivu, amani na wenyeji waliopo kupenda wageni, ni jambo
jema, na hapa nafikiria siku ambayo nitamaliza muda wangu, sujiui ntakuwa na
majonzi kiasia gani moyoni’’,ananisimulia.
Msaidizi
wake Dr. Chen, dk He, anasema Chen ni miongoni mwa watu waliokuwa na furaja na
furaha, baada ya kupata taarifa ya kwenda Zanzibar kwa ajaili ya kutoa huduma
za matibabu.
“Unajua,
Chen alikuwa haamini kuwa atafika Zanzibar tena hap Pemba, na baada ya kufika
hutamani hata siku zake za mapunziko yeye aweko kazini, maana anawapenda sana
watu wa Zanzibar kwa ukarimu na upole wao”,ananieleza Dr.He.
Muda
aliofika kisiwani Pemba, kutokana na kujichanganya kwakwe na wazawa, tayari dk Chen
anasema anayo maneno zaidi ya 30 ya Kiswahili anayoyajua, ikiwa ni pamoja na
“nzuri sana, jambo, hakuna matata, karibu tena.
Maneno
mengine ambayo ameshaweka kwenye akili yake ni, wimbo mzima wa malaikaaa….
nakupenda malaikaaa…. hata neno kusema rais za Zanzibar na mengine kadhaa.
Kwa sasa
anajiamini kuzungumza sentesi zaidi ya 10 za Kiswahili, anachokiona ni fasaha,
mbele ya watu na anasema anajitahidi kila siku ahakikishe ameingiza neno jipya
la kiswahili kwenye akili yake.
Dr. huyo,
pamoja na wenzake saba, watakuwa kisiwani Pemba kwa siku zisizodi 360, yaani
miezi 12, ingawa Chen mwenyewe wala hatamani kuwa, saa 8640 zinazobeba siku za
mwaka ziishe na kurudi kwao.
Ingawa kwa
timu nyengine za madaktari hao kutoka China tokea walipoanza waka 1972,
walikuwa wakikaa miaka miwili, lakini bahati kwa Dr. Chen imekuwa mbaya, maana
sasa wanakaa kipindi cha mwaka mmoja tu.
Chen na
kundi lake la madaktari wataalamu, linaunda timu ya 27 tokea uhusiano wa China
na Zanzibar ulipoanza miaka 45 sasa wa kupokea madaktari, kumbe wakati uhusiano
huu unaanza hata Dr. Chen mwenyewe hajazaliwa.
Ndoto zake
za kuwa daktari kwa lengo la kuisaidia jamii yake na nyengine, zimeshaanza kudhihirika
ndani ya kisiwa cha Pemba, ambapo ndani ya siku 30 tokea wawasili, wameshafika skuli
ya Msingi Makombeni wilaya ya Mkoani.
“Juzi
tulikwenda Makombeni skuli ya Msingi na tuliwafunza watoto lugha ya kichina
kwanza, kisha tukawapa elimu ya kujikunga na athari zitokanazo na ugonjwa wa
masikio, pua na koo”,anasema.
Kwa safari
ya skuli ya Makombeni, Dr. Chen anasema aliisababisha yeye baada ya kuwepo
uhusiano mzuri na mmoja wa madaktari wanaofanya kazi hapo, hadi kumuunganisha
na mwalimu Mkuu wa skuli hiyo.
“Wakati
tunakwenda Makombeni kutoa huduma hiyo, pia niliwachukulia zawadi wanafunzi hao,
ikiwa ni pamoja na penseli, mabuku kwa ajili yao”,anasema.
Mwalimu mkuu
wa skuli hiyo, Othaman Machano Mmanga, anasema anafurahia ujio wa madaktari hao
kwenye skuli yake, na hasa kuwafanyia vipimo wanafunzi wake.
Anasema,
hakuamini jinsi waliovyowaomba madaktari hao bila ya barua au kupita ngazi za
juu, na hatimae kuwafanyia vipimo wanafunzi wangu na kisha kuwapa na mabuku na
penseli.
Yeye anaona
timu zote 27 zilizoanza kuja hospitali ya Mkoa ya Abdalla Mzee Mkoani tokea
mwaka 1972, lakini hii ya mwaka 2017, ambayo ndio ya mwanzo itakayokuwepo kwa
mwaka mmoja, imefanya kitu tofauti.
“Yule Dr. Chen, alipofika skulini kwangu, kwanza alipenda mandhari, pili alikuwa karibu
sana na wanafunzi na wala hakutamani kuandoka na walichelewa kurudi, inaonekana
wanapenda sana kucheza na watoto”,ansema.
Dr. Chen
kwa sasa ndie mtaalamu pekee kwenye timu hiyo ya madaktari saba, akiwemo yeye
wa nane, kwa matibabu ya pua, koo na masikio na lengo lake hasa ni kuwa daktari
bingwa na mahasusi hapo baadae ”specialist”.
Anasema hata
alipokuwa hospital ya “Nan Jing Fisrt hospital” nchini China, ambayo
anayofanyia kazi, anakumbuka kumfanyia mwanamme mmoja matibabu ya giota, na
ndani ya siku 10, bila ya kuja juu.
“Siku hiyo
ndio pekee ambayo sitoisahau kwenye kazi yangu hii ya udaktari, maana
nilimfanyia mtu ‘operation’ ya goita, na siku 10 hajazinduka, lakini siku ya
11, alikuja juu na kuvuta puumzi”,anasema.
Anakumbuka
pia hata ndani ya Kisiwa cha Pemba, tayari alishamfia mwanamke mmoja, kuondoa
goita kwenye shingo yake, ingawa baada ya siku mbili tu, aliivuta pumzi na kuwa
na hali yake ya kawaida.
Kubwa
aliloligundua kwa wanafunzi wa skuli ya Msingi ya Makombeni pamoja na wananchi wengine wanaofika hospitali
ya Mkoa ya Abadalla Mzee Mkoani, anasema jamii ya Pemba, haina utamaduni wa
kuchunguuza afya zao.
Anasemna
lazima kwa wizara ya afya ya Pemba na Zanzibar ni kuhakikisha, inawapa elimu
wananchi juu ya umuhimu wa kuchunguuza afya zao, badala ya kwenda hospitali
wakiwa tayari wanaungua.
“Magonjwa
mengine ninayoyatibu hospitali, tayari yemeshakomaa, na pengine kama wahusika
wengekuwa na utamaduni wa kuchunguuza afya zao, basi kusingekuwa na tatizo
kubwa’,anasema.
Hivi
karibuni akiwakaribisha madaktari hao, Mganga mkuu wa hospital hiyo Dr.Mwita
Haji Mwita, aliwaambia madaktari hao kuhakikisha wanawapa uwelewa wa hali ya
juu madaktari wazalendo.
“Dr. Chen na
kundi lako, karibuni Zanzibar na karibuni kisiwa cha Pemba, jiskieni huru na
muwe nao madaktari wetu wa kizalendo, ili mkiondoka mmeshawapa
utaalamu”,aliwaambia.
Hopsitali ya
Abdalla Mzee Mkoani Pemba, tayari imeshapandishwa hadhi na sasa kuwa ya Mkoa,
baada ya huduma zake kuimarika kwa kuwepo kwa vifaa vya sasa.
Hospitali
hiyo, ambayo hivi karibuni ilifanyiwa ukarabati mkubwa na baadhi ya majengo
kujengwa upya na serikali ya watu wa China, pia ilipatiwa vifaa vya kisasa kama
vya kutibu mfupa bila ya kufanya upasuaji mkubwa.
Dr. Makame
Chirau, anauehusika na kitengo hicho kwa upande wa madakatari wazalendo,
anasema kwa sasa ule mpango wa kuwekea vyuma au pio pio kwa wanaovunjika,
umepungua baada ya kuwa na vifaa vya kisasa.
Vifaa hivyo
vya kisasa, vyenye thamani ya shilingi milioni 60, ambavyo kwa Afrika Mashariki
vipo kwenye hospitali hiyo pekee, vilitolewa na serikali ya watu wa China miezi
minne iliopita.
Dr. Chen Er
Dong, aliezwaliwa Disemba, mwaka 1975 kijijni kwao Nan Jing nchini China, ana
mke na mtoto mmoja, na kwasasa yeye ni daktari wa masikio, pua na koo akiwa
hospitali ya Mkoa wa Abdalla Mzee Mkoani Pemba.
No comments:
Post a Comment